"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, May 9, 2010

Jumapili Yenye Baraka!

Ni kweli majaribu uliyonayo ni "Ya muda tu"

Inawezekana ndoa yako inapita katika wakati mgumu na umefika Mahali unapata wazo hata la kujiua kwa kujinyonga au kunywa sumu au unatamani ardhi ingetoa shimo upotelee huko hata hivyo ukiwaangalia watoto wako unajihurumia na kujuta.

Unajiona maisha hayana maana kwani mtu uliyemwamini na kuyatoa maisha yako kwake hadi kifo amekusaliti na haoneshi dalili ya kubadilika.

Inahuzunisha, inaumiza, inakera, inakatisha tamaa, inatia uchungu, inakosesha usingizi, unajikuta huna hamu hata ya kula chakula na kila unapofanya jambo lolote inafika Mahali unachanganyikiwa hata unaogopa kutembea barabarani kwani unaogopa unaweza kugongwa na magari.

Umewashirikisha watu mbalimbali unaowaamini kwamba wanaweza kukusaidia kukupa ushauri na kukutia moyo hata hivyo huoni mabadiliko na unaona hali inazidi kuwa mbaya zaidi.

Japo wamejitahidi kukutia moyo kwa maneno kama vile;

Nafahamu kile unapitia, nayafahamu maumivu uliyonayo

Hata hivyo bado mwisho wa siku wameenda majumbani kwao na kukuacha kwako na huzuni ambayo inakufanya uzidi kuona duniani ni Mahali pasipofaa kabisa.

Ukweli ni kwamba yupo mmoja ambaye anaijua shida yako kwani na yeye alipata katika njia kama yako.

Yeye anaposema nitazame mimi ni kweli ni kitu halisi.

Yeye alikuwa mwanadamu halisi na Mungu halisi.

Anafahamu majaribu ni kitu gani.

Hata kama Unasema hakuna mtu duniani ambaye anafahamu kile unachopitia, yeye anafahamu hali halisi ya hayo magumu unayopitia.

Wakati huu yupo mkono wa kuume wa Mungu Baba akikuombea wewe kwa sababu yeye anaona kile unaona, anajisikia kile unajisikia, anasikia kile unasikia, anagusa kile unagusa, ana onja kila una onja na ananusa kile unanusa.

Linapokuja suala la mahusiano:

Hata kama wewe ni single

Kumbuka yeye alikuwa single na akaishia maisha matakatifu na akashinda.

Kama upo kwenye ndoa:

Yeye ni Bwana harusi na sisi kanisa ni Bibi harusi na anafahamu namna gani bibi harusi wake asivyo mwaminifu (cheating kwa kutenda dhambi) hivyo anafahamu vizuri maumivu ya kuwa na mwanandoa ambaye si mwaminifu.

Jina lake anaitwa YESU hivyo mtazame yeye.

Hilo jaribu ni la muda tu

MATHAYO 19:26

Lakini Yesu akawatazama, akawaambia,

“Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote yanawezekana

2 comments:

Anonymous said...

Bwana asifiwe kaka laz.Mimi nasema asante kwa kunitia moyo kwa maana ndivyo nilivyo.ubarikiwe na Bwana j.pili njema ek

Lazarus Mbilinyi said...

Pole sana dadangu,
Mungu ni mwaminifu hata katika giza nene bado yupo.

Ubarikiwe pia