"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, May 18, 2010

Kipi Sahihi!

Nini kinaruhusiwa kitandani kwa ndoa za kikristo?


Linapokuja suala la sex wanandoa wengi (Christians) hufanya tu kile ambacho wanaona kinakubalika kwao wakiwa chumbani.

Kama wamebarikiwa kuwa na uvumbuzi mkubwa wa vitu mbalimbali vinavyoweza kuwapa ridhiko, raha, ukaribu (closeness, intimacy) na hata kufikishana kileleni kuna uwezekano mkubwa wataendelea kusherehekea tendo la ndoa kwa raha zao, hata hivyo wapo ambao hata baada ya kupeana raha kiasi hicho hujikuta katika hatia ya kuhisi labda baadhi ya vitu walivyofanya vilikuwa dhambi.

Wanandoa wengi wa kikristo (au waliokoka) wanapenda kufahamu nini kinakubaliwa na kipi hakikubaliwi wakiwa kitandani, bahati mbaya zaidi ni kwamba hata makanisani hii topic ya sex haizungumzwi na pia vitabu vingi vya kanisani vinahusu masuala ya kiroho zaidi na si sex, hivyo kuna kutomfahamu hali ya juu kipi ni sahihi na kipi si sahihi.

Je, isingependeza kama wakristo wote tungekuwa na orodha ya vitu ambavyo vikifanywa wakati wa sex kwa mume na mke ni dhambi na orodha nyingine ikaonesha vitu ambavyo vikifanywa chumbani si dhambi?

Je, inawezakana kupatikana orodha kama hiyo na ikawa okey kwa kila Mkristo wa mjini na mashambani? Ulaya na Afrika?

Jibu la hilo swali kuna uwezekano mkubwa likawa HAPANA; haitawezekana kwani jamii nyingi za watu wa kanisani zinatofautiana mno katika uelewa kuhusu nini kinaruhusiwa wakati wa sex.

Naamini hakuna orodha ambayo ingeweza kukubalika na wakristo wote, NEVER, NEVER NEVER.

Hata hivyo kinachoweza kufanyika ni kutoa mwongozo ambao unaweza kukufanya ufurahie zawadi ya sex katika ndoa yako kwa kiwango cha juu kabisa.

Na ndicho naamini Mungu anapenda watoto wake tufahamu.

Pamoja na Ubunifu ambao Mungu aliufanya kuhusu sex na raha yake bado Mungu mwenyewe ameweka mipaka kupitia neno lake na hii ni kwa faida yetu ili kuweza kufurahia zaidi uumbaji wake.

Kwanza lazima tukubaliane kwamba kuna baadhi ya tabia na vitendo ambayo Biblia inavitaja wazi kabisa kwamba ni DHAMBI kama vile uzinzi (sex huku mmoja akiwa au wote wakiwa wameoa au kuolewa), uasherati (sex kabla ya kuoa au kuolewa), mapenzi kinyume na maumbile (Sodom), sex kwa ndugu wa karibu, sex jinsia moja (homosexual) na kufanya mapenzi na wanyama.

(Kumbukumbu la Torati. 18, Warumi 1:21-32, I Wathesolanike. 4:1-8, na I Wakorintho 6:12-20).

Pia kuna vitendo ambavyo Biblia haivitaji moja kwa moja, hata hivyo kwa kutumia msingi wa neno la Mungu tunaweza kutambua kwamba ni vitu visivyokubaliwa kwa mteule.

Vitu hivyo ni kama vile internet pornography na X rated movies, kufanya mapenzi kwa makundi (group sex), kubadilishana mume au mke (swinging).

Pia jambo la kuzingatia ni kwamba hakuna tofauti kati ya binadamu wa sasa na yule wa wakati wa uumbaji (Adam).

Wote tuna maumbile yale yake (anatomy), tuna homoni zilezile na uwezo wa akili ule ule, tamaa ile ile na mahitaji ya sex yale yale.

Ndiyo maana muhubiri anasema kwamba ‘hakuna jipya duniani

Ingawa tabia za zinaa katika jamii huelezea aina ya kizazi na nyakati za dunia.

Je, nini maoni yako kuhusu sex toys, vibrators? nk

No comments: