"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, May 31, 2010

Kukabiliana na Abuse

Namna ya kukabiliana na maisha ya abuse ya huko nyuma:

MOJA

Fahamu kwamba hata iweje kilichotokea katika maisha yako hapo zamani na kusababisha wewe kudhalilishwa huyu uliyeoana naye hana uhusiano nacho na wala hahusiki kabisa. Mara nyingi watu hulipa dhambi za matendo ya nyuma ya wazazi wao au ndugu zao hasa wanawake; kama wewe ni mwanamke ambaye ulikuwa abused Kumbuka kwamba huyo ambaye umeoana naye si baba yako au ndugu yako ambaye alikudhalilisha kimapenzi au kwa maneno.

Huyo ni mume wako, mwanaume anayekupenda wewe

MBILI

Kila unalojiambia mwenyewe ni muhimu sana (extremely important) katika kujikubali mwenyewe. Watu ambao huwa abused mara nyingi huificha ndani hiyo siri ya kuwa abused na kuendelea kuji-abuse wenyewe. Hukataa kuruhusu vitu ambavyo vingefanya wafurahie (enjoy) kwa kuwa wanajiona hawastahili na hawana thamani ya kupokea upendo na kufurahia.

Hivyo basi dumu katika kujisemea mwenyewe kila siku kwamba “Napendwa, Mungu ananipenda, mume wangu ananipenda, mchumba wangu ananipenda, watoto wangu wananipenda, ninastahili kupendwa na kupenda, mume wangu ananipenda na kunijali kama nilivyo, ananiheshimu kwa jinsi nilivyo, Bwana nisaidie kupenda kama unavyonipenda mimi” unaweza pia kusema haya maneno mbele ya kioo huku unatazama kwa macho yako ili kupata picha yako mwenyewe.

TATU

Fahamu kwamba upo katika safari. Mambo yaliyokupata ambayo yalitakiwa yasikupate ambayo wewe hukusababisha yataendelea kujirudia katika akili zako na mawazo yako katika nyakati tofauti. Kile kilitokea wakati mtoto kimesababisha kuwa na hofu na mashaka fulani katika maisha yako sasa. Namna unavyoitikia kihisia katika matukio tofauti tofauti leo ni matokeo ya abuse uliyopata wakati ukiwa mtoto.

Je, hii ina maana maisha kwako hayana maana?

HAPANA, hapana kubwa.

Unahitaji kufahamu kwamba kutakuwa na mabaki ya hizo hisia katika maisha na mtazamo wako mpya ni muhimu sana katika kukabiliana na hizo hisia zilizobaki.

NNE

Chagua kusema hapana kwa negativity. Kawaida usitunze kumbukumbu za mambo mabaya tu katika maisha yako. Kama kuna daftari umeandika mambo mabaya yaliyotokea katika maisha yako ni bora ukalitupa na kuandika daftari jipya ambalo utaandika mambo mazuri yaliyotokea katika maisha yako ili kuponywa haraka katika abuse yako.

Mawazo mabaya yanapojifunua kwako yafunike kwa mawazo ya vitu vizuri (positive), andaa orodha ya mambo mazuri ambayo umefanya katika maisha yako na yatunze na kuweka sehemu ambayo kila siku utayaona na kuyasoma. Kile unaona na kutunza katika akili zako ndicho kitakachotoka nje.

No comments: