"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, May 23, 2010

Kuna Hatari pia!


Ndoa mpya haiwezi kukosa kukutana na hatari ambazo zinaweza kusababisha mmoja au wote kuumia wakati wanaendelea na maisha ya ndoa.
Ni muhimu sana kwa wanandoa kuwa na ufahamu wa kutosha ili kuhakikisha penzi linakuwa hai siku zote.
Zifuatazo ni mojawapo ya hatari ambazo zinatakiwa kuepukwa.

Moja: Kujipa majukumu mengi kwa wakati mmoja:
Hili linawahusu sana wanandoa wapya, baada ya kuoana huamua kufanya mambo mengi wa wakati mmoja au kutimiza malengo mengi iwezekavyo kitu ambacho huwafanya wakirudi nyumbani mmoja au wote kuwa wamechoka bila mfano.
Anaweza kuamua kuanza masomo upya na wakati huohuo anafanya kazi full time, fungua business na kutaka kuisimamia, na kujenga nyumba, vyote kwa wakati mmoja.
Matokeo yake mke na mume wakikutana jioni kila mmoja hoi hata hawezi kuwa na muda na mwenzake.
Lazima utenge muda wa kukaa na mke au mume wako ili kujenga mapenzi na ndoa kuwa hai muda wote.

Mbili: Matarajio yanayopitiliza:
Wapo watu huingia kwenye ndoa wakiamini ndoa ni jibu la mambo yote na kwamba watakuwa na furaha ambayo haitashuka chini hata siku moja.
Wapo wanawake hutegemea waume zao kuwatimizia zaidi ya wao wenyewe wanavyoweza kuwatimizia waume zao.
Ikiwa na matarajio yanayopitiliza ukweli wa mambo unaweza kujikuta upo kwenye disappointment kubwa, frustration kubwa na kujikuta umeingia kwenye mtego kihisia.

Tatu: Ndugu:
Kama kuna mwanandoa ambaye hajatoka au hajaondoka kwa wazazi wake, au ambaye wazazi wake wakisema kitu anawasilikiza kuliko mke wake au mume wake basi ndoa inaweza kuingia kwenye mgogoro mzito na inaweza isifike mbali.
Pia wapo wanandoa ambao huruhusu hata ndugu zao ambao si baba wala mama kuingilia ndoa na kuwa na sauti kwa mke wa kwenye ndoa.
Wanandoa wanatakiwa kuwa pamoja na misimamo wa pamoja namna ya kushughulikia ndugu zao.

Nne: Kuvamia muda wa mwenzako:
Kawaida upendo ni kitu ambacho ni bure na huru.
Kila mwanandoa anahitaji nafasi ili kupumua, anahitaji kuwa na muda wake ambapo anatakiwa kuwa mwenyewe.
Wapo ambao huchungana hadi kupitiliza kiasi kwamba hata kama ni wivu “is too much”
Pia kuwa na wivu unaozidi kipimo wakati hakuna tatizo lolote huweza kumfanya mwenye wivu kutojiamini na kujiona yupo insecure.

Tano: Madeni na kugombana namna fedha zinatumika:
Kawaida katika maisha ukitaka kuepuka migogoro ya kifedha kwanza ni kununua kitu cash na si kukopa kama huwezi usinunue kabisa.
Kuna aina mbili za watu duniani, wa kwanza ni yule anajua kutunza fedha na yule anayejua kuzitumia fedha.
Wakikutana wote ni watumiaji wazuri basi moto utawaka kwani kunahitaji mmoja ambaye anajua kutunza au wote. Watumiaji ovyo wa pesa anaweza kupata mshahara wa mwezi mzima na kununua vitu ambavyo hata havikuwa kwenye bajeti na baada ya siku mbili familia haina fedha tena.

Sita: Ulevi na vyote vinavyofanana na hivyo:
Ikiwa kwenye ndoa ni muhimu sana kuepuka Ulevi kama plague.

Saba: kushindwa au kufanikiwa katika maisha
Kushindwa kwa business au maisha ni kitu ambacho huwaumiza sana wanaume kwani hujiona ni failure na loser katika maisha na huweza kuelekeza hasira zake kwa familia.
Pia mwanaume anapofanikiwa kimaisha au business huweza kumsahau mke na watoto.

Nane: Kuoana umri mdogo
Ndoa ambazo zimeanza na wanandoa wenye umri chini ya miaka 18 wengi huwa bado hata hawajajijua wenyewe na hivyo huwa na skills chache kuhusu maisha na matokeo yake ndoa hushindwa.

Tisa: Kutoridhishwa kimapenzi, upweke, na kuchepuka
Hii ni jumla inayotisha, inatakiwa kushughulikiwa ipasavyo.

No comments: