"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, May 24, 2010

Kuoa na Kuolewa

Ili kumpenda mtu (fall in love) unahitaji kumuona mtu au kukutana naye kupitia njia mbalimbali.

Lazima mtu awe “available”

Kuwa single lilikuwa tatizo maalumu kwa vijana walikuwa umri wa kuolewa miaka 30 iliyopita, na mtu ambaye ni single nyakati hizo alionekana ni mtu wa ajabu sana mbele ya jamii.

Leo hii wanawake na wanaume ambao wapo katika muda muafaka wa kuoa na kuolewa (marriageable) ni mara 4 zaidi ukilinganisha na hiyo miaka.

Kwa mfano nchini Marekani kwa sasa kila watu 5 ambao wapo umri wa kuwa ameoa au kuolewa 1 ni single.

Pia sasa si tatizo tena au ukiwa single unaonekana mtu wa kawaida tu na hakuna anayekushangaa.

Hata hivyo katika mazingira mengine kumpata partner wakati mwingine ni ngumu sana.

Inawezekana wewe ni mmoja ya wale ambao umefika umri wa kuolewa au kuona na umekuwa “available” tatizo hakuna unayokutana naye ili uweze kuoana naye.

Pia inawezekana una kuwa “available” sehemu ambazo si rahisi kukutana watu wengi na wageni kwako.

Je, umeshajaribu kwenda makanisani, shule (darasani), kujitolea shughuli za jamii, na mikusanyiko ya kijamii pia nk ili kukutana na watu.

Pia familia na marafiki wanaweza kukusaidia kukutana na watu wapya na wanaweza kukutambulisha pia.

Anyway, pia kuna mitandao mbalimbali kwa ajili ya kumpata mwenzi (ingawa inabidi uwe makini zaidi kwani huko ni rahisi kudanganywa.

+++++++++++++++++++++++++++

Pia kuna tatizo moja ambalo ni serious zaidi nalo ni kwamba baadhi ya jamii idadi ya wanawake ni kubwa zaidi kuliko wanaume, hivyo wanawake wanakuwa wengi kuliko wanawaume wanaoweza kuwaoa (surplus women).

Pia kuna jamii ambazo idadi wa wanawake (marriageable) ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wanaume hivyo kuna wanaume wengi ambao wapo umri wa kuoa na wanawake ni Wachache (surplus men).

Kwa mfano baadhi ya nchi kama Marekani na Tanzania idadi ya wanaume ni ndogo kuliko wanawake ambao wapo umri wa kuolewa.

Kwa mfano nchini marekani vijana wanapofika umri wa miaka 23 kuna kuwa na wanawake milioni 7 zaidi ya wanaume ambao wanatakiwa kuolewa.

Kituo cha sensa cha marekani kinaonesha kwamba kuna wanaume (single) 99 kwa kila wanawake (singles) 100 katika umri wa miaka 15-24, na kila wanaume (singles) 89 kwa kila wanawake (singles) 100 kwa umri wa miaka 25 – 34.

Kuna wanaume (singles) 67 kwa kila wanawake (singles) 100 katika umri wa miaka 35 – 45.

Kama mwanamke amepewa talaka akiwa na umri wa miaka 20 na kuendelea kuna uwezekano wa asilimia 75 kwamba anaweza kuolewa tena.

Kama akipewa talaka akiwa na miaka 30 na kuendelea ana asilimia 50 kuweza kuolewa tena na akiwa amepewa talaka akiwa na umri wa miaka 40 na kuendelea, basi ana asilimia 30 za kuolewa tena.

Pia data zinaonesha kwamba mwanamke ambaye hubaki single hadi miaka 40 uwezekano wa kuolewa ni mdogo sana.

Hata hivyo katika nchi za china na India hali ni tofauti kwani idadi ya wanaume ni kubwa zaidi kuliko wanawake.

Kwani kwa kila wanaume 119 kuna wanawake 100 wote wakiwa umri wa kuoa na kuolewa nchini china na inakisiwa kwamba kufikia mwaka 2020 kutakuwa na wanaume milioni 30 zaidi ya wanawake wenye umri wa kuoa nchini China.

Pia leo hii unapoongelea suala la surplus women ni pamoja na wanawake ambao wameenda shule sana hadi umri ukapitita kuolewa na wanaume kuwaogopa kuoa au kuchumbia.

No comments: