"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, May 26, 2010

Mume Akupende!

Haijalishi ni kazi gani mume anafanya anastahili kupewa appreciation!

Wanaume wakikutana wenyewe kwa wenyewe kama hawafahamiani swali la kwanza kuulizana ni “unafanya kazi gani?”
Sababu ya msingi ni kwamba wanaume wengi suala la kazi ni kitambulisho (identity)
Ndivyo walivyoumbwa na Mungu na hiki ni kitu wanachozaliwa nacho kujikuta ni mtu wa kwenda kuwinda, kulima, kufanya kazi kwa ajili ya familia yake.
Kufanya kazi ni jambo la msingi kwake.
Akipata ugonjwa anaweza kupigana na kuhimili kila aina ya msongo wa mawazo au mgandamizo wa damu hata hivyo linapokuja suala la kazi kwake huwa maumivu ni makubwa kiasi cha kuwa na stress au depression.
Mwanaume anaweza kusimama imara hata katika ugonjwa unaoleta mauti kama cancer lakini si suala la kupoteza kazi au business.
Mwanaume mmoja baada ya kufanya deal la uhakika kwa kutengeneza Mamilioni ya pesa, kwa furaha akaenda nyumbani kwa mke wake kumwambia hizo habari njema na mke wake akamjibu kwa mkato “sawa nimekusikia” then akaendelea na kazi zake pale nyumbani.
Mume alikatishwa tamaa na kuvunjwa moyo kiasi cha kutoa maamuzi kwamba kuanzia hapo hatamshirikisha mke wake jambo lolote au maamuzi yoyote kwani hakutegemea kama mke wake angejibu kwa mkato vile na kuonekana alichofanya hakina maana.
Wanawake wengi hawafahamu umuhimu ambao wanaume wameuweka katika kazi zao na kwamba ukimshukuru kwa kazi anayofanya basi anaweza kukuonesha upendo wa ajabu.
Fikiria wewe ni mwanamke sasa umegundua kwamba ni mjamzito na unaenda kumweleza mume wako naye anakujibu “sawa” then anaendelea kuangalia TV utajisikiaje?
Basi ndivyo mume wako hujisikia pale Unapokuwa hutambua kazi yake hata kama wewe unafanya kazi na kupata fedha kubwa zaidi.
Mwanamke anaweza kuamua au kuchagua kufanya kazi au kuwa nyumbani na kulea watoto, hata hivyo mwanaume anaweza kuchagua kufanya kazi au kwenda jela.
Ni kweli mwanaume mwema huolewa kwa sababu ya UPENDO na si FEDHA, hata hivyo mwanamke huyu mwema huwa na hekima na maarifa ya kufahamu sifa ya ndani ya huyu mwanaume kama anaweza kujenga kiota na kuhudumia vifaranga kwa chakula, mavazi na malazi maisha yao yote.
Je umewahi kumshukuru Mume wako kwa kazi anayofanya?
Kwa mwanamke ambaye anataka kuonesha respect kwa mume wake anaweza kujaribu kuandika hata message au note na kuiweka hata kwenye Lunch box yake na kumwambia “ mpenzi mume wangu nashukuru sana kwa namna unajituma kufanya hiyo kazi kwa ajili ya familia” au vyovyote unavyotaka wewe.
Pia unaweza kumshukuru kwa uhuru aliokupa wewe mwanamke kufanya kazi au kukaa nyumbani na yeye kufanya kazi.
Wapo wanawake ambao huwaza mara kwa mara kwamba wangewashukuru waume zao kwa kufanya kazi, hata hivyo kuwaza peke yake si lolote unachotakiwa kufanya ni kumshukuru au kumwambia.
Je, utajisikiaje mume ambaye anasema kwamba huwa anafikiri mara kwa mara kukwambia anakupenda na hajawahi kukwambia anakupenda!
Ukweli mahusiano ni two way street, mume anatakiwa kukwambia “ANAKUPENDA” na wewe unatakiwa siku moja kumwambia mumeo “Asante sana nashukuru kwa kazi unayofanya ambayo inatupa fedha na maisha
Nakuahidi atafanya mambo ya ajabu sana kuhusiana na kukupenda wewe kwa sababu ataamini wewe ni mwanamke ambaye unaamini katika yeye.
Mume wako anajiona unamshukuru kwa kazi anayofanya pale tu
Pale unapomwambia kwa maneno au maandishi kwamba kile anafanya kina maana kwako na familia.
Unaelezea imani yako katika taaluma yake.
Unasikiliza stories mbalimbali kuhusu kazi zake na taaluma yake, inaweza kuwa ni magari, ualimu, Computer, forestry, nk.
Kumsaidie kukamilisha ndoto zake kama wakati ule wa kuchumbiana.
Hulalamika kuhusiana na kazi zake

4 comments:

Anonymous said...

Inawezekana mume wako ni mlevi wa kazi kama mume wangu hata hivyo baada ya Kuamini na kumsifia na kumshukuru kwa kazi anayofanya akawa anajitahidi kutafuta muda wa familia kwani alijiona vizuri na yupo respected, hii ina maana kumsema sana haiwezi kusaidia, kukasirika haiwezi kusaidia na unaweza kuharibu mambo zaidi ila kumshukuru kwa kazi anafanya na kumsikiliza na kuchangia ndoto zake katika kazi zake huweza kumfanya aoneshe upendo zaidi.
BM

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli ndiyo maana ni muhimu sana kumshukuru na kuhakikisha anafamu kwamba una mwamini na kum-support, kwani anapoona unaithamini kazi yake na yeye atajitahidi kukuonesha upendo.

Anonymous said...

Jamani,hii kitu ni kweli kabisa kwani,mwanamke anapotambua mchango wako katika familia ,anakuwa anakutia nguvu hata kama mambo yanakua yanaenda mrama unajiona kwamba utajitahidi kupambana,mfano anaweza akakupigia simu kakwambia pole sana na kazi mapenzi,kwani leo upo busy sana,unajisikia vizuri na unajikuta moyo umepata nguvu zaidi,wanawake ninyi we acha tu.

Lazarus Mbilinyi said...

Upo sahihi kabisa, Pamoja na kwamba wanawake leo wanafanya kazi (tunawapongeza kwa hilo na Mungu awabariki sana) hata hivyo ni wanaume wachache hukubali mwanaume kufanya kazi wengine hukataa, so ni muhimu kwa mke kumshukuru Mungu kwa kumruhusu kufanya kazi na zaidi huwa wanaume tunajisikia raha sana na tunaweza kumpenda sana mwanamke ambaye anatambua mchango wa kazi zetu, ndoto zetu na taaluma zetu hata ili kupenda na kufurahia kile tunafanya basi tunajiona huyu mwanamke kweli ni rafiki wa kweli.

Pia dawa ya mwanaume busy ni kumsifia zaidi kwa kazi anafanya ndipo atastuka na kuona kumbe mke wangu anaipenda kazi yangu, ngoja na mimi nimdhihiridhie kwamba nampenda, matokeo yake ni kila kitu kibadilika.

Pia kama mume amekamatwa na kazi au ni mlevi wa kazi (workaholic) anaipenda kazi kuliko wewe, anaipenda laptop kuliko wewe na unajiona upo neglected dawa ni kmshukuru kwa kazi yake anayoifanya na kutokuwa critical. Hata kama unaona hastahili kupewa appreciation jambo la busara ni kumshukuru na kumpongeza kwa maneno na au maandishi ndipo utaona mabadiliko.

Kama mwanamke ambayo unapenda mwanaume anaposema "mke wangu umependeza, mke wangu nakupenda, mke wangu wewe ni mrembo kuliko wanawake wote on earth surface, sisi wanaume tunahitaji kusifiwa eneo la kazi zetu.

Upendo daima!