"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, May 4, 2010

Ndoa Imara


Mwanandoa imara siku zote hutazama (focus) kwenye uimara wa mwanandoa mwenzake na si katika udhaifu wake.
Hii ina maana mwenzake akifanya kosa (kumrushia neno linaloumiza, kufanya kile ambacho hakukipenda nk) pamoja na kuumia bado huanza kufikiria mambo mazuri kuhusu huyu mwenzi wake ambaye amemuumiza na kujisemeya moyoni kwamba “pamoja na kunirushia neno ambalo limeniumiza lakini ni mwanamke/mwanaume ambaye siku zote amekuwa akinipenda na kunijali” na huendelea kuikabili (suppress) ile hasira au uchungu wa kuumizwa kwa kuendelea kufikira positives zilizopo kwa mwenzake.
Kwa upande wa mwanandoa dhaifu au ndoa zisizo imara wanandoa huweka msimamo na mtazamo unaojikita katika kuangalia au kuona udhaifu (weakness/failures) wa mwenzake tu.
Ni ukweli ulio wazi na usiofichika kwamba hata ndoa imara ambazo tunaziona ni mfano wa kuigwa hukumbana na matatizo katika kila kona ya maisha iwe matatizo ya kifedha, ugonjwa, ndugu, watoto, kazi, mapenzi, nk hata hivyo system wanayotumia kupambana na hayo matatizo ni tofauti sana (model) na ndipo kwenye siri kufanikiwa kwa ndoa na kuzorota kwa ndoa.
KWA UFUPI
A. Ikitokea mwenzi wako amekuudhi kwa kitu fulani, fikiria (au tafuta) mambo mazuri 3 ambayo Anafanya katika ndoa yenu. (inaweza kuwa amekupa watoto/mtoto mzuri, anakujali kwa kukutimizia mahitahitaji mengine kama chakula, mavazi na malazi, anakuridhisha kimapenzi, amekufanyan uonekane wa maana hata kwa ndugu zako nk)
B. Badala ya kumshambulia mke wako au mume wako shambulia lile tatizo kwani lile tatizo ambalo limekufanya uumie ni vitu viwili tofauti na yeye.
C. Jiulize; “Hivi kwa namna nilivyo mtu mwenye akili timamu nitakasirika na kukaa na hii stupid issue moyoni hadi lini?” watu wote wenye busara huhakikisha jua halizami bila kumaliza hasira zao!
Kwa maelezo zaidi kuhusu ndoa imara soma hapa.

No comments: