"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, May 31, 2010

Ni Mpito, uwe makini!

Namna ya ku-handle maisha yanapokuwa tofauti na ulivyotegemea.

Kwa nini maisha ya ndoa ya watu ambao wapo katika umri wa makamo (midlife) huwa na crisis nyingi na wakati mwingine kuishi kwa kuachana au talaka?

Je, inawezekana ni kwa sababu ni wakati ambao familia huwa katika wakati wa mpito (transition) kwa maana kwamba familia ilizoea kuwa na baba, mama na watoto na sasa watoto wote wapo shule (vyuo) mama ana kazi yake au kubaki nyumbani mwenyewe na baba kwanza ndiyo anahaha kuongezewa cheo kazini au kupanda ngazi katika taaluma yake vitu kama kusoma Masters au PhD nk.

Suala hili (mabadiliko ya maisha kifamilia) huonekana ni dogo sana hata hivyo huweza kubadilisha dynamics za familia kwa namna ya ajabu sana.

Wapo wanawake ambao maisha yao asilimia kubwa tangu kuolewa huwa ni kuwa karibu na watoto, watoto huwa kila kitu kwao na wakati mwingine huenda mbali zaidi kwa kuwaweka waume zao pembeni na watoto hupewa first priority.

Matokeo yake mume huamua kujichimbia katika taaluma zake na kazi zake ambazo zinampa identity zaidi.

Pia huamua kuwa na maisha yake ambayo huko anaweza kutimiziwa mahitaji yake ya kihisia pia, kitu ambacho huwa hatari zaidi kwa ndoa yake.

Sasa watoto hawapo, wamebaki mke na mume wanatazamana, kibaya zaidi kila mmoja anamshangaa mwenzake kwani huvutii kama zamani, mume anamuona mke amekuwa jimama fulani maana kajazia huwezi amini kama ndiye yule ki-portable cha miaka 18 iliyopita. (Anyway mwanaume smart atakupongeza bila kujali una figure gani kwani kitendo cha kumzalia watoto ni sifa njema, hasa kama anafahamu nini hutokea huko kwenye chumba cha labour)

Mke naye anamuona mume ni mbabu fulani kwani ndo anagundua mzee kitambi kimeshuka ghafla na kuonekana amechuja hana jipya.

Wanajikuta hakuna tena kuvutiana kimwili.

Sasa nyasi kwenye nyumba ya jirani (yule mwanamke au yule mwanaume) huanza kuonekana za kijana zaidi ndipo utasikia sasa mwanaume anamtelekeza mke wake (miaka 20 kwenye ndoa) na kwenda kuoa kabinti kenye miaka karibu sawa na binti yake.

Inawezekana mke alikuwa ana mawazo kwamba siku moja yeye na mume wake watastaafu wakiwa ni watu kwenye legacy kubwa katika jamii hata hivyo ndoto zinayeyuka hivi hivi huku anaona kwa macho mawili yasiyo na upofu wowote.

Kwa kuwa kila mtu sasa ana ratiba yake inakuwa ngumu sana kwa wawili hawa kuwa na connection emotionally.

"THE GRASS IS ALWAYS GREENER ON THE OTHER SIDE OF THE FENCE"

AN AMERICAN PROVERB OF DISCONTENT

No comments: