"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, May 24, 2010

Ni mrefu sana

SWALI:

Kaka Mbilinyi naomba kuuliza swali.

Mimi ni binti wa miaka 22 tatizo langu ni mrefu sana kiasi kwamba kila Mahali ninapopita watu hunisumbua na kunipigia kelele za kunizomea.

Hii inanifanya nijisikie vibaya,

je nifanyeje?

NN

JIBU:
Dada NN,

Nashukuru sana kwa swali lako,

Ukweli naamini hukuomba uzaliwe mrefu; imetokea tu na hiyo ni identity yako, hivyo badala ya kujisikia vibaya wewe jisikie vizuri na ujivunie urefu wako ambao ni sifa njema na ni kitu kizuri kwani wengi wanatamani wangekuwa warefu na hawajabahatika.

Kwa wewe kuwa mrefu kuliko wengine maana yake una maisha bora zaidi mbele yako kama utaamua kutumia urefu wako kama baraka.

Kuwa mrefu ni kitu kizuri na unatakiwa kujivuna, kujisikia vizuri, kujipa kichwa na kumshukuru Mungu kwa kukupendelea.

Ni kweli watu hupenda kutania watu ambao ni warefu sana au wafupi sana; hata hivyo ili usiumie sana na wewe unatakiwa kuwajibu kwa utani “just to have fun” then unabadilisha topic.

Unaweza kuwajibu kwa kuwauliza vipi “vipi hali ya hewa ipoje huko duniani” then smile na furahia baraka zako za urefu wa kwenda juu.


Unatakiwa kujiamini kwani wewe genetically upo superior kuliko wengine na tembea kwa maringo kwani hiyo ni sifa na baraka.

Baadhi ya faida za kubarikiwa urefu wa kwenda juu ni kama ifuatavyo.

Kupendeza ukivaa nguo:

Kuna sababu za msingi kwa fashion models kuwa na urefu wa kiwango fulani hasa katika suala zima la mavazi.

Kawaida nguo hupendeza (fit better) kwa watu ambao ni warefu, hivyo mwanamke anapokuwa na sifa ya urefu, akivaa nguo hupendeza zaidi na kuonekana vizuri kwa wanao mtazamo pia kamera na picha.

Kujiamini:

Upende usipende kawaida watu waliobarikiwa kwenda juu huonekana ni strong na confident.

Hii ni kutokana na saikolojia za watu; hivyo kwa baraka zako za kuwa super tall watu huamini unajiamini basi wadhihirishie kwamba unajiamini na unajisikia special one.

Kipato Kikubwa:

Inaaminika kwamba watu warefu hutengeneza pesa nyingi kuliko watu ambao ni wafupi, sababu kamili sijajua ila naendelea kumfuatilia.

Pia wanawake warefu wamehusishwa na kuwa na intelligence kubwa zaidi kuliko wenzao ambao ni akina Andunje, hii inatokana pia na kujiamini kwao hasa wanapokutana na mabinti wengine ambao ni wafupi.

Usalama:

Wanawake ambao ni warefu kawaida hutembea kichwa juu na mabega kwenda mbele na nyuma kwa madaha na hatua za uhakika ili ku-support urefu wao hii husaidia kupunguza uwezekano wa kuvamiwa na vibaka (criminals) ukilinganisha na wanawake wafupi.

Criminals wengi si warefu sana hivyo wakiona mwanamke mrefu huhofia usalama wao.

Hii ina maana unapopita Manzese na Kariakoo vibaka huogopa kukuibia kwani wanahisi unaweza kuwazidi nguvu.

Matukio ya jamii:
Ukiwa mwanamke mrefu kawaida inakupa benefits fulani katika jamii.

Kukiwa na mkusanyiko wa watu mwanamke mrefu atakuwa na faida kubwa katika kuangalia na kuona kila kitu kuliko mwanamke mfupi, pia inaweza kusaidia kufikia vitu kirahisi.

Wewe mwanamke mrefu ukijipanga kwenye mstari ni rahisi sana kusalimiana na mgeni rasmi ikitokea watu wanamgombea.

Pia popote ulipo huna budi kutatizika uanze vipi kuongea na watu kwani watu wakikuona tu wanaanza kuongea wenyewe kwani urefu wako ndiyo ice breaker ya maongezi.

Hivyo unaweza kutengeneza marafiki chapchap na huwezi lala njaa popote.


Urahisi wa maisha:
Ukiwa mrefu inakusaidia kufanya baadhi ya vitu vizuri zaidi kama vile kufikia vitu vilivyo kwenye shelves za juu bila kuomba msaada au kuweka vitu vizuri juu ambapo wengi (wafupi) huhitaji msaada wa ngazi.

Ajira:

Kuna baadhi ya kazi huhitaji watu warefu kama vile Polisi, jeshi nk hivyo kubarikiwa kwenda juu ni kujirahisishia kupata kazi ambazo wengine ni tatizo.

Pia kuna uwezekano mkubwa wa mtu mrefu kupata kazi ukilinganisha na mtu mfupi kama sifa zingine wanafanana.

Michezo:

Kawaida mtu mrefu ana faida kubwa sana kwenye fani zote zinazohusika na sports. Ukitaka basket ball ni balaa, ukija soccer ni balaa, ndondi ndiyo kiboko maana kama wewe ni tall opponent atakuwa na kibarua za ziada kurusha masumbwi kichwani kwako kwani atahitaji ngazi kitu ambacho si rahisi.

Nimeamini ninyi mliobarikiwa kwenda juu lazima ukiamua utakuwa na kipato Kikubwa zaidi kwani faida zipo nje nje.

Mungu akupe nini!

Kumbukumbu:

Ukiwa tall ni rahisi sana watu kukukumbuka katika matukio mbalimbali ya jamii, kama unaongea na mtu kwenye simu na alikuwa amekusahau ukishamwambia “ni yule dada tall” basi pale pale atakukumbuka, hivyo kuwa tall ni faida sana katika masuala ya jamii hasa kama unafanya business nk.

Tatizo linakuja kwenye masuala ya mwenzi wa maisha kwani wanaume wengi huogopa mwanamke mrefu kuliko wao hii ni stigma tu ambayo ipo vichwani mwao kwani kuna message kwamba inawezana wewe mwanamke mrefu ni strong hivyo huhofia kudundwa au kuishi na tembo ndani ya nyumba.

Pia wapo wanawake hujisikia raha na salama pale mume wakiwa mrefu kuliko yeye kwa maana kwamba akiwa mwilini mwa mumewe anajiona hakuna kitu kinaweza kumuathiri kwani yupo protected na mtu anayeenea pande zote.

Pia tatizo lingine ni pale unapopanda ndege (angani) bila kuomba mapema kiti maalumu (exit row isle seat) kwani unaweza kujikuta umepewa seat ambayo inakubana miguu na safari kuwa ngumu hii ni pamoja na viti vya magari nk.

Ubarikiwe!

No comments: