"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, May 28, 2010

Ni Uamuzi wako!

Ni kawaida jua linapowaka na mionzi kutua juu ya siagi huweza kuifanya kuyeyuka na wakati huohuo mionzi ya jua ikipenya kwenye udongo wa mfinyanzi huufanya kuwa mgumu zaidi.

Joto la jua ndilo linaelekeza au kudhihirisha tabia za ndani za siagi na udongo wa mfinyanzi.

Tunapokuja kwenye suala la ndoa, maisha yetu hufanana sana na namna siagi na udongo wa mfinyanzi umeonesha tabia zake kutokana na mionzi ya jua.

Inawezekana partner wako anasumbua muda mwingi (irritant), hii hutokea, partner wako anakuhangaisha, anakufanya ujione kila kitu ni kichungu, anaudhi sana na unajisikia kutaka kumjibu kwa jeuri au kama inawezekana uandae power point presentation umwelekeza namna ambayo amekuwa boring kwako.

Hata hivyo mwanandoa mwenye busara huamua kufanya choice, kumjibu na kutenda kwa hekima ya kimungu au kumjibu jeuri na kutenda kwa kumkomoa (which is sinful way)

Ni rahisi mno kumlaumu mke wako au mume wako, pia mke wako au mume wako naye ana kila sababu za kukulaumu wewe.

Hata hivyo wewe ukiamua kutia njia ya kulaumiana (blame route) utaishia kuwa victim na kuharibu siku yako.

Unapoona mke wako au mume wako amewasha moto ambayo joto lake limeanza kupanda Kumbuka jambo moja na kujiambia mwenyewe kwamba:

Kwa kuwa mimi ni mtu mzima (mature person) mwenye uhuru wa ndani wa kuamua na kutoa maamuzi, nafahamu wazi kwamba uamuzi wangu ni wajibu wangu

Kuishi na kuwa na mtazamo wa aina hii si kawaida inahitaji hekima na busara na kujifunza kwani ni wanandoa wangapi huharibu siku kwa jambo dogo tu.

Kuijua hii siri ni rahisi kupenda na kujali mwenzi wako.

“Unaweza kuumizwa ila ni uamuzi wako kuamua kulaumu”

Mke wako au mume wako anaweza kukuudhi, kukusumbua, kukupigia kelele, kukuumiza na kukuhuzunisha hata hivyo unao uamuzi wa kuchagua kupita njia ya dawa ya moto ni moto au kumsamehe na kuendelea kufurahi na kumwangalia Mungu.

“Hakuna mtu anayeweza kukufanya usiwe na furaha hadi uamue mwenyewe”

No comments: