"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, May 2, 2010

Ni Ubongo tu!

Ni ubongo tu!

Wanawake hutambua hamu ya sex ni suala la hisia kwa miongo mingi.

Baada ya miaka mingi ya utafiti wanasayansi wamekubali (conclude) kwamba piga ua sex kwa mwanamke ni suala la ubongo kwanza na si vinginevyo.

Tangazo lilitolewa na watengenezaji wa Viagra (impotence drug) ambao wametelekeza shughuli ya kutengeneza Viagra ya wanawake.

Wamagundua kwamba namna Viagra inavyofanya kazi yaani kuongeza msukumo wa damu katika viungo vya uzazi (sexual organs) kitu ambacho ni kizuri kwa wanaume kwa wanawake haina matokeo yoyote katika kumpa hamu ya sex mwanamke.

Wanawake ni complicated zaidi kuliko wanaume linapokuja suala la sex.

Kuna tofauti kubwa kwa wanaume na wanawake linapokuja suala la kusisimka (arouse) na hamu ya kufanya mapenzi (desire).

Kwa wanaume kusisimka mara nyingi hupelekea hamu ya mapenzi, hivyo basi kwa kuimarisha uwezo wa kusimamisha (erection) hii moja kwa moja hupelekea Viagra kuwa na matokeo mazuri. Lakini kwa mwanamke kusisimka baada ya damu kujaa kwenye sexual organs hakuwezi kumpa hamu ya kufanya mapenzi.

Badala yake ubongo wa mwanamke ndio kiungo muhimu sana linapokuja suala la sex na mwanaume anayeweza kuweka sawa ubongo wa mwanamke (feelings) hufanikisha zaidi kuliko kidonge cha Viagra.

Huu ugunduzi wa kwamba Viagra haina matokeo muhimu kwa mwanamke katika kuwa na hamu ya sex ni pigo kubwa sana kwa kampuni ya Pfizer ambayo ingetengeneza mabilioni ya pesa hasa baada ya kufanya utafiti kwa miaka 8 na kwa wanawake 3,000.

Kwa nini imeshindikana?

Waligundua kwamba Viagra huongeza damu katika eneo la pelvic bado wanawake hawakujisikia kusisimka.

Hii ina maana kuna utofauti wa mabadiliko ya uke (genital changes) na mabadiliko ya ubongo (mental changes)

Hii tofauti haipo kwa wanaume, mwanaume akishamuona mwanamke naked anasisimka na atahitaji sex, kwa mwanamke kuhitaji sex huendana na factors nyingi na ubongo ni kiungo (sex organ) muhimu sana kumpa hamu ya kufanya mapenzi.

Matatizo ya hamu ya sex kwa wanawake ni complicated zaidi kuliko tatizo la wanaume kushindwa kusimamisha fimbo zao.

Utambuzi wa tatizo la sex kwa wanawake huhusisha kuchunguza mwili, hisia na matatizo ya mahusiano na hivi ni vitu complex na vinategemeana kitu ambacho si rahisi au ni kigumu sana kupima matokeo ya dawa yoyote.

Nini anahitaji mwanamke kitandani au kabla ya kuingia kitandani?

Anachohitaji mwanamke kitandani ni mume kumpa mwanamke “mashairi tu”.

Ni kitu kilichowaza kwamba wanaume husisimka mara moja (straight forward).

Wakati huohuo wanawake huhitaji kuridhishwa kwa undani zaidi huku kukiwa na romance na love kwa kiwango Kikubwa. Pamoja na kwamba wanaume wanahitaji romance na love bado hawapo programmed sawa na wanawake kiuhitaji.

Bottom line ni kwamba mwanamke huhitaji upendo (love & affections), mwanaume anayemwelewa (understanding) na kuridhika kihisia (emotions) na ndipo anaweza kuwa tayari kwa tendo la ndoa na si vinginevyo.

No comments: