"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, May 5, 2010

Nifanyeje Hataki?

SWALI

Kaka Mbilinyi hongera kwa kazi nzuri!

Swali langu ni kwamba, je utafanyeje kama umeoana na mwanamke ambaye ni mzuri, mkweli, mpole, mwema lakini likija suala la kitandani ni usumbufu usioelezeka, ni boring to death!

Nampenda sana mke wangu pia naamini na yeye ananipenda.

Tangu kuoana kwetu tulipanga kuwa ndoa inayompa Mungu utukufu (obeying Christian values) hata katika suala la tendo la ndoa, ingawa ni mwenzangu hakuwa comfortable kulizungumzia.

Sasa mke hapendi sex, hapendi kuongelea suala la sex (ukitaja tu neno sex anaanza kukunja sura kama ishara kwamba sipo tayari kuongelea hilo na tusipoongea hakuna linalofanyika au kurekebishwa).

Baada ya kumfuatilia nikagundua kwamba Amekulia kidini sana.

Naomba msaada nifanyeje?

JIBU

Kaka pole sana kwa shida iliyokukuta, hata hivyo Kumbuka hakuna jambo lisilo na mwisho.

Inaonekana kwamba watu ambao hukulia kwenye imani za dini ambazo zinakuwa na msimamo mkali kuhusiana na masuala ya mahusiano (sexuality) huzaa wanandoa ambao linapokuja suala la sex kuna kuwa na matatizo makubwa.

Zipo dini ambazo zinafundisha kwamba suala la sexuality lina uhusiano wa moja kwa moja na dhambi.

Wanafundishwa kwamba dunia na vyote vijazavyo ni vitu vya muda tu na binadamu anatakiwa kushinda majaribu yote ya dunia hii ili kuurithi uzima wa milele ambao ndio matazamio ya nafsi zilizopo duniani.

Na adhabu ya kushindwa kuyashinda majaribu ni kukosa uzima wa milele na moja ya majaribu makubwa ni suala la sex.

Wanaamini sex katika ndoa ni kwa ajili ya kuijaza dunia tu (reproduction) na sex inapotumika kama kupeana raha (recreation, pleasure) kati ya mke na mume ni dhambi.

Hivyo basi mwanamke anaruhusiwa kuwa mke na mama na si kujihusisha na sex kwa ajili ya kumridhisha mume au kupeana raha kati yake na mume wake.

Anapokuwa mke na mama nyumbani anakuwa amechukua picha kamili ya mama mtakatifu (siyo Bikira Maria tafadhari msije mkanipiga mawe) na anapojihusisha na sex kwa ajili ya raha na kuridhishana na mumewe anakuwa amechukua picha (image) ya Malaya mtaani (prostitute).

Hata hivyo kitu cha ajabu ni kwamba pamoja na hayo mapokeo na misimamo ya dini ambayo huwa kama malezi ya baadhi ya watu, haiwezi kuzuia hitaji la sex na zaidi hamu ya kuridhishwa kimapenzi katika ndoa.

Kuhitaji sex ni kitu kimeumbwa ndani yetu (genes) na Mungu mwenyewe, raha ya kufanya mapenzi ndiyo huchochea watu kuzaana katika level ya kawaida.

Mke wako inawezekana anajikuta kwenye wakati mgumu (guilt) pale unapomuhitaji kimwili, anapokubali kupeana raha ya mapenzi anajikuta inakuja picha ya kuonekana Malaya hasa kutokana na alivyolelewa (aliyokulia & fundishwa) na zaidi kufanya hivyo amefundishwa kwamba ni dhambi na anaweza kukosa ahadi ya milele ile ya kushinda majaribu hapa duniani hivyo hujiona afadhari awe mbali na wewe (kugoma sex zaidi ya suala la kuzaa watoto).

Ombi lako rahisi la kuridhishwa kimwili ni kitu kingine kabisa kwake kwani kwa mtazamo wake kukubali kupeana raha ya mapenzi huweza kuathiri roho yake na namna anajiona.

Anachohitaji mke wako ni uhuru au ruhusa ya yeye kuwa mtu wa kimapenzi (sexual) na kujifahamu kwamba kufurahia tendo la ndoa katika ndoa yake ni kitu kizuri na ni kiroho pia na zaidi si dhambi bali ni utakatifu pia kwani wewe na yeye ni mume na mke.

Hata hivyo ni ngumu sana kwa wewe kumueleza kwamba yupo huru na ajisikie raha kuhusiana na suala la sex bali ni kumpata kiongozi wa dini yake ambaye anao ufahamu wa kutosha kuhusiana na suala la sexuality katika ndoa na kwamba huyo kiongozi wa dini yake anafahamu kwamba tendo la ndoa si kwa kuzaa tu bali faragha ya Adam na Hawa wa sasa na ni jambo zuri kwa wanandoa kufurahia mapenzi kwani wanandoa wanaporidhishana vizuri wanakuwa na furaha na kanisa huanzia nyumbani.

Zaidi unaweza kuongea na wataalamu wa masuala ya mahusiano ya wanandoa (therapist & counsellors & wachungaji nk) ambao wanaweza kukusaidia wewe na mke wako na hata kulifahamu tatizo lake kwa undani zaidi na kuwasaidia.

Naamini haya maelezo yameweza kuwa msaada!

No comments: