"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, May 11, 2010

Nisikilize!

Kuna aina mbili za wanaume wa kwanza ni wenye HESHIMA na wa pili ni wale WASIO NA HESHIMA.

Usikubali kuolewa na mwanaume kabla hujafahamu tofauti hizi mbili, mwanamke unayemuona kwenye kioo chako cha kujitazama atakushukuru sana.

Mwanaume mwenye heshima atakulinda, atalinda moyo wako na hisia zako, atasimama imara kulinda kiroho chako na mwili wako, kumchagua mwanaume mwenye heshima ni kuchagua maisha bora katika ndoa.

Wewe mwanamke si gari; Ukikutana na mwanaume anayetaka kukujaribu kama gari (linamfaa), palepale mwelekeza kwa wanaouza magari, mwambie kwa heri na usigeuke nyuma.

++++++++++++++++++++++++

Ndiyo umekutana na mwanaume handsome, anaonekana ni mwema, mpole na anaonekana ana akili na shule imekubali na katika kuongea naye anakwambia ana mtoto na hana mpango wa kumtunza wala kumuona mama yake huyo mtoto;

Haraka iwezekanavyo mpeleke kwa mama wa huyo mtoto, USIANGALIE NYUMA anza mbele kwa kasi ya ajabu.

Usifanye kosa lilelile ambalo mama wa mtoto au alifanya.

Kwani kuna tofauti gani kati ya mama wa huyo mtoto na wewe, kwa taarifa yako wote ninyi ni wanawake!


Jipende mwenyewe kwanza!

Kama huwezi kujipenda mwenye na kufurahia maisha mwenyewe, nakwambia upo off the market; usifanye kosa, kama hujipendi mwenyewe hakuna MWANAUME ANAWEZA KUKUPENDA ... No matter how great the man is.+++++++++++++++++++++++++
Usiwahukumu wanaume wote kwa sababu ya kosa la mwanaume mmoja; labda kama unataka wanaume wote wakuhukumu wewe kwa kosa la wanawake wengine wasio na adabu.Je, unajikuta unawavutia wanaume ambao tabia zao ni kama mbwa?

Basi jichunguze aina ya perfume unatumia kwani wanaume walio mbwa huvutiwa na aina ya perfume mwanamke anatumia, serious!Usijidanganye!

Urembo wako, umbo lako, uwezo wako kitandani, ustadi wa kupika chakula, uwezo wa kutetetea wanawake wengine hata haiba yako inayovutia haitaweza kumfanya mwanaume abadilike; Never! Never! Never!


Kama mchumba wako anakuahidi kitu na hatimizi, weka rekodi, ukiona hii tabia inajirudiarudia, inawezekana anacheza na feelings zako, pia ni warning signs kwamba huna thamani yoyote kwake na inawezekana hakupendi na hakujali kabisa, Think twice.

+++++++++++++++++++++++++
Sawa, umekutana na mwanaume si mume wako anakutaka kimapenzi, huna haja kushangaa, huyo hakuheshimu, ni mbwa!


Unajiuliza;

“Kwa nini hanipigii simu, kwa nini hana muda na mimi, kwa nini haoneshi kama ananipenda?”

Jibu ni kwamba ni kweli hana mpango na wewe, na kama hutamwacha aende zake na wewe kuendelea na maisha yako basi unachofanya ni kuzuia mtu wa kweli kuja katika maisha yako na kupata penzi la kweli.Kuna baadhi ya wanaume hupenda kupiga wake zao haijalishi wamesoma au hawajasoma, wanapesa au hawana pesa, kwani kumpiga mke huwapa sense ya kujisikia kwamba wana power/control, na ukijipeleka mwenyewe kwa wanaume kama hawa wanaweza kukufanya wewe ni punching bag.

Ni muhimu sana ukiwafahamu tangu mapema ili uwaepuke.

Ubarikiwe na Bwana!

2 comments:

Anne said...

Ni kweli kabisa kaka Mbilinyi uliyoyasema,lakini moyo wa mwanadamu ni nani awezaye kuujua?

Watu huvaa ngozi za kondoo no matter how long utajipa muda wa kuwafahamu, ili tu ukisharidhika na kuona anafaa ,aje akuoneshe makucha ndani ya ndoa akijua itakuwa ngumu kwako kutoka;

Mi nafikiri sisi wasichana ni wakati muafaka (kama tunataka waume bora na si bora waume)kumwangalia,kumuamini na kumtegemea Mungu na kuvumilia ili yeye aichunguzaye na aijuaye mioyo ya wanadamu jer(17:10)awalete waume bora wanaomcha na kumuabudu katika ROHO na KWELI! na hapo ndoto zetu za kuwa na ndoa bora zitatimizwa ktk mapenzi ya MUNGU.
Asante kaka Mbilinyi na Mungu akubariki kwa mchango wako katika ksaidia eneo hili muhimu na lenye matatizo mengi katika jamii zote zo chini ya jua hili!!

Anne

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Anne,

Asante sana kwa kile umeandika kwani umeandika kitu cha uhakika na inaonesha una uzoefu wa kutosha na unaona mbali (you know the stuff).

Mwenye sikio na asikie......

Upendo daima