"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, May 31, 2010

Nitamwelezaje?

SWALI:

Kaka Mbilinyi kwa miaka 10 nimekuwa najizuia kuwa wazi kimapenzi kwa mume wangu kwa kuwa wakati mtoto nilikumbana na kudhalilishwa kimapenzi kitu ambacho hunifanya nisijiweke katika mazingira ya kuumizwa tena.

Sikupenda kuongelea sex wala kufanya mapenzi na mume wangu isipokuwa tu pale nilipojilazimisha kwa kuwa nilitamani kuwa na watoto (Mungu ametujalia kupata watoto wawili).

Baada ya kusoma makala mbalimbali kwenye blog yako nimejikuta naumia sana kwa namna nimekuwa namnyima mume wangu haki yake kwangu na naumia zaidi kwa kuwa amenipenda miaka yote acha historia ngumu ya maisha yangu.

Je, nawezaje sasa kuanza upya kushiriki tendo la ndoa bila kukumbuka za yale niliyopitia wakati mtoto na je, naweza vipi kumueleza mume wangu ambaye amekuwa anaonesha upendo mkubwa kwangu na nimekuwa namnyima haki yake kwa muda mrefu?

Dada Jane

JIBU:

Dada Jane kwanza hongera sana kwa ujasiri wa kutaka kurekebisha mambo sasa, kutokana na uzoefu wa mambo hatari uliyopitia na kustahimili ni kweli wewe ni mama jasiri kuanza kuyazungumzia tena ili kupata majibu ya kudumu na kuondoa mzizi wa jambo lenyewe.

Ndiyo maana mume wako anakupenda sana naamini ni kwa sababu wewe ni mwanamke mwenye moyo au mtazamo mzuri wa maisha hasa kutoridhika na zaidi kuhakikisha unaoleta tofauti.

Utaanzeje kumueleza mume wako?

Utaanza kwa kumuomba kama ana muda kwani unahitaji kuongea naye tena unaweza kumwambia mwende sehemu, sehemu ambayo kumetulia au mnaweza kwenda nje ya mazingira ya kawaida hasa siku za weekend (retreat) na itakuwa busara sana kumwambia mapema kabisa kabla ya kuondoka kwenda huko kwamba unataka mkaongee ili asije kukasirika kwa kudhani mnaenda kuenjoy kumbe unaenda kumweleza mambo mazito, kwa njia hii itamsaidia yeye kujisikia vizuri baada ya kuelezwa.

Mwambie unampenda sana na kwamba unajisikia hujamtendea haki kwa muda mrefu na sasa unatarajia kufanya mabadiliko, ndipo Mwangalie usoni, mshike mkono na mwambie

Mpenzi wangu, my honey naomba msaada wako”

Mwambie kila kitu, na tangu mwanzo mwambie kabisa kwamba maelezo yako yanaweza kuwa marefu kwa kuwa ni muhimu sana wewe kuongelea kila kitu na details zote kwa wakati mmoja ili akuelewe, na maliza maelezo yako kwa kuwambia, hii ndiyo sababu nimekuwa sipo wazi kwa sex kwa miaka yote kwani nilikuwa naogopa au nilikuwa na hofu ya kuumizwa tena, nilikuwa naogopa kupoteza kuaminiwa, nilikukosea”.

Je, unaweza kukusamehe?

Huo muda ambao mmeutumia pamoja, namna ulivyokuwa mkweli na wazi itamfanya huyo mwanaume kukubali kama ni kweli mumeo anakupenda na ana ubongo unaofanya kazi vizuri.

Namna ulivyomnyenyekevu na namna utakavyoongea kitu halisi kilichotokea katika maisha yako kama mwanamke mwenye hisia (sijasema ulie sana bali naamini utakapokuwa unamueleza naamini hutakwepa kutoa machozi na naamini mtakuwa na wakati mzuri kama wanandoa kuwa na connection ya kihisia kwa namna ya tofauti sana na mtaijenga ndoa kwa namna mpya kabisa.

Ni maombi yangu kwamba atakusamehe na mtaweza kuanza ukurasa mpya kimapenzi katika ndoa yenu.

3 comments:

Anonymous said...

"aisee ni ngumu sana,ila kuwa muwazi hasa kwa washauri wa maswala ya saikoloji na mahusiano i think itasaidia sana!!maana hapo hakuna penzi na ni sumu/bomu la baadae"

Anonymous said...

"ni kweli kabisa izi siri ata kama ni nzito kiasi gani,as long as zinakuhusisha na mtu/watu ni vyema kuzitafutia ufumbuzi,na sio kunyamaza kimya,,kweli ni bomu kubwa...wapo washauri waaminifu wa maswala ya ubakaji,ila wanawake tuna mizigo"

Anonymous said...

si kila mwanamme anakifua cha kusikiliza about your past, mimi mume wangu aliniambia tusizungumzie kabisa yaliyopita, uendelee na pendo letu, na sote tumetii hata kama tulikoseana hamna kukumbushana ya nyuma, ni kusamehe na kusahau, mara nyingi wanadam wakat flani hatuwezi sahau mpk Mungu tumuombe aingilie kati, huyo dada ana roho ya uchungu, Yesu akusaidie itoke.

ms gbennett