"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, May 10, 2010

Nithibitishie!

Love is a Choice!

Mume mmoja, mke mmoja:

Kuna neno moja ambalo ni neno la msingi na muhimu sana linapokuja suala la ndoa hasa katika lugha ya kingereza nalo ni loyalty.

Maana ya hili neno ni kuwa mtiifu, au mwaminifu kwa hali ya juu iwe katika biashara au mahusiano nk.

Ni neno linalofanana na neno allegiance, truth, faithfulness.

Mke wako anafahamu kwamba yeye ni mke wa mume mmoja, anajijua kwamba yupo committed kwako 100%

Lakini kuna wakati mke wako Hujiuliza maswali kama ni kweli wewe ni mume wa mke mmoja, hasa pale anapokuona unavutiwa na mrembo/warembo unaokutana nao mtaani au hata kwenye TV.

Ni kweli ulikubali kwenda mbele ya kanisa ili kukubali kwamba unataka kuwa na ndoa ya mke mmoja hata hivyo namna unaishi na yeye inampa wasiwasi kwamba wewe ni mume wa mke mmoja.

Mke wako amekuwa insecure kwenye eneo hili na anahitaji reassurance na si wewe kumtania au kuleta dhaka au kuleta mahoka au kufanya masihahara au kuleta mizaha au jokes au kuleta matani au kutumbuiza au kufanya Vichekesho au michezo.

Yupo serious anahitaji umuhakikishie kwamba wewe ni mume wa mke mmoja kama ulivyomuahidi hataukaamua kufunga naye ndoa takatifu ya mke mmoja na mume mmoja.

Je, umewahi kufikiria namna ilivyo ngumu kwa mke wako kukuamini kwamba wewe ni mume wa mke mmoja hasa kutokana na wanaume wengi wanavyo- cheat, dunia inavyopambwa na kila aina ya warembo, dunia ilivyojaa wanawake wanaoshawishi wanaume kwa kuvaa wanavyotaka wao, namna Tv, Radio na internet zinavyopotosha watu kuishi kwa uadilifu katika ndoa?

Unahitaji kumhakikishia kwamba wewe ni mume wa mke mmoja!

Ayubu alifahamu tatizo la kutokuwa mwaminifu si kwa mke wake tu bali hata kuharibu kiroho chake na akasema:

‘‘Nimefanya agano na macho yangu yasimtazame msichana kwa kumtamani”.

(Ayubu 31:1)

Wanaume wote tunahitaji kujifunza kutoka kwa Ayubu.

Mke anapokuwa na uhakika kwamba mume wake amefanya agano (covenant) na Mungu kwamba atajitahidi kumfanya Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maeneo yote ya maisha yake pamoja na ndoa yake mke hujisikia salama.

Mke anapokuwa na uhakika wa upendo na uaminifu wa mume wake kwake anajisikia kuwa na nguvu na kuhamasika kuhakikisha ndoa inakuwa bora zaidi.

Hii ni kutokana na namna Mungu amemuumba mwanamke na ndiyo maana agano la ndoa lina msingi wa kuaminiana (loyalty) hadi kifo kwa wawili (mke na mume) wanapooana.

Je, mke hujisikia mume anaonesha loyalty pale;

Anapomuongelea vizuri mbele za watu,

Anapojihusisha na mambo mazuri kuhusu mke wake,

Anapomsaidia kutoa maamuzi yanayohusiana na watoto wake,

Anapokuwa hamsahihishi mbele za watu.

Pale anapokuwa hawatamani wanawake wengine,

Pale anapofanya ndoa kuwa kitu cha kwanza,

Anapokuwa hamlalamikii (critical) mke mbele za watoto na watu wengine,

Pale anapohusishwa katika mambo ya jamii hata kama wengine wanaona aibu kwenda na wake zao,

Pale anapowaambia watoto wanatakiwa kumheshimu mama yao,

Pale anapoongea positively na si negatively.

NB:

Mke uliyenaye anakutosha kama huamini muulize king Solomon

4 comments:

Anonymous said...

Ni kweli mke hujisikia kuwa karibu na mume kama pete ilivyokaribu na kidole (Wimbo Uliobora 8:6)

Anonymous said...

Ring humkumbuka mke kwamba anapendwa na mume wake na ni yeye peke yake na kwamba duniani kuna mwanaume mmoja tu ambaye yupo loyal kwake maisha yake yote hadi kifo na si hadi talaka itakapowatenganisha.

Anonymous said...

Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma, bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata? (Mithali 20:6)

Lazarus Mbilinyi said...

Pia naamini kuwa loyal ni pamoja na kusimama na mume au mke wakati wote wa maisha duniani iwe bad times au good times, iwe kuzolota kwa afya, kufukuzwa kazi, kupoteza nyumba au business kushindwa, kukosa watoto, kupata ulemavu nk.