"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, May 12, 2010

Umri Je?

Umri ni namba tu!

SWALI:

Kaka Mbilinyi asante sana kwa kutuelimisha.

Swali langu je, Biblia inasema lolote kuhusiana na suala la Umri katika kuoana?

Ni mimi Simololi.


JIBU:
Dada Simololi,

Asante sana kwa swali na pia kwa kupita hapa ili kujifunza tips mbalimbali za maisha ya mahusiano.

Ni mara chache sana Biblia imezungumzia umri kama kigezo cha mahusiano (kumpata mke au mume).

Ila tunafahamu kwamba baba wa Imani Ibrahimu alikuwa amemzidi mke wake Sara miaka 10 (Mwanzo 17:17) na hakuna wanandoa wengine ambao kwenye Biblia tumepewa umri wao.

Pia unaweza kuona mfano wa Yusufu kwamba alikuwa na umri zaidi ya Mariamu (mama wa Yesu) na Biblia haitaji wazi ni umri kiasi gani.

Wengi wanasema “age is just a number” inawezekana ni kweli hata hivyo binafsi naamini umri ni jambo la msingi pia ingawa haliwezi kuzidi umuhimu wa suala la wokovu au kiroho cha mhusika, kufanana kwa imani na tabia.

Kuoana kwa kupishana miaka zaidi ya 20 wengi hupata maswali ingawa kupishana miaka chini ya 10 hakuna maswali.

Tahadhari kubwa kuhusiana na suala la umri katika kuoana; ni kutomkimbilia mtu hasa kutokana na tamaa, au kufuata pesa zake na mengine yanayofanana na hayo.

Jambo la msingi ni kuomba Mungu akupe hekima katika kumpata mke au mume ambaye utaishi naye maisha yako yote yaliyobaki hapa duniani.

No comments: