"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, May 27, 2010

Unachotaka ni Mwili tu

Ulikuwa unanisubiri mlangoni kwa hamu kubwa, leo mmmm!

Mume amesafiri kwa wiki nzima kwa ajili ya business.

Akiwa huko safarini anamkumbuka sana mke wake na anaamua kufupisha muda wa safari ili arudi nyumbani Ubungo Dar es Salaam na kuwa na muda na mke wake na watoto.

Na kuwahi kurudi kwake anapenda iwe surprise kwa mke wake hivyo kutua tu uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere anaamua kuwahi nyumbani kwani kichwani tayari anawaza namna atakuwa na muda mzuri na mke wake (romantic sexual evening).

Ile anafika nyumbani anakutana uso kwa uso na mke wake ambaye kwa mshangao anamuuliza

Unatafuta nini sasa hivi hata umewahi kurudi mapema hivi tena bila hata taarifa? Ok, kwa kuwa umewahi kufika kawachukue watoto shule, na pia tuna kikao cha Walimu na wazazi so inabidi muda ukifika uende, pia mwanao John inabidi uongee naye kwani Walimu wamepiga simu kwamba anasumbua wenzake na pia unaporudi kuwachukua watoto shule pitia dry cleaner nichukulie nguo zangu, tena nilitaka kusahau dada yangu atakuja hivyo nitatoka naye kwenda dinner so wewe utabaki na watoto

Imekuwa too much kwa mwanaume ambaye ameahirisha safari yake na kuwahi nyumbani kumpa mke surprise na romantic sexual evening, sasa ni watoto, vikao, kupitia mizigo na mke na dada yake.

Wote mume na mke wapo kwenye kikao cha wazazi na Walimu na mume anaonekana amekasirika na kuvunjika moyo kwa namna jioni yake ilivyoharibiwa na makujumu ya mke wake.

Wanaporudi nyumbani kwenye gari mke na mume wote wapo kimya, kila mmoja anawaza yake. Mke amekasirika kwa nini mume pamoja na kusafiri kwa wiki zima mume hamuulizi wiki nzima Ilikuwaje na mambo gani alikutana naye. Mume naye amekasirika kwa sababu anaona mke wake hajampa respect na yupo unreasonable kumpa makujumu yote hayo na kumthamini dada yake na watoto kuliko yeye mume.

Baada ya dinner ambayo haikuwa nzuri sana kwani kila mmoja alikuwa na donge moyoni, mke na mume Wanaingia chumbani kulala.

Mume anajitahidi kuyamaliza kwa kutumia mtindo ule ule wa wanaume wengi kwa kumgusa (rub) mke wake mgongoni kitu ambacho ni njia nzuri ya kuanzisha ile kitu.

Mke anaguna na kumwambia “Hapana, nimechoka” kwa hasira anageuka mgongo kwa mgongo na kulala huku akiugulia na ameumizwa bila kusema kitu.

Mke naye akifahamu fika kwamba mume wake amekasirika anamwambia

Huwezi hata kufikiria yaani Unachotaka kwangu ni sex tu, you are insensitive!”

Mume kwa mshangao anamwambia mke wake

Siamini kama unaweza kusema hivyo, nimesafiri wiki nzima, narudi nyumbani hata kunipokea huwezi, salaamu hakuna, unachokijua ni watoto na dada yako, ninapojitahidi kuwa karibu na wewe unaniambia umechoka na mimi ni insensitive”.

Sasa mke naye amekasirika na kuumia anamjibu,

Hukuniuliza namna gani nimeshinda na watoto kwa wiki nzima na nimekutana na mambo gani, muda tu ambao unakuwa interested na mimi ni wakati unapotaka sex

Mume naye anamjibu mke,

Ndiyo nimesafiri wiki nzima hata hivyo unakumbuka wakati ule tumetoka kuoana, nikisafiri ulikuwa hata unaniambia niahirishe kukaa huko nikuwahi kwani ulikuwa na hamu na mimi, ulinisalimia mlangoni kwa furaha na upendo huku ukitabasamu na tunapeana busu, leo ninaporudi unaniangalia usoni na kusema Kwa nini upo nyumbani mapema hivi, asante sana na nashukuru kwani sikufahamu upo hivi

Kama wewe ni mtaalamu wa mambo ya ndoa, Je tatizo lipo wapi?

3 comments:

Anonymous said...

Mimi naona tatizo ni mawasiliano kwa kila mmoja kumuelewa mwenzake ndiyo maana baada ya kukasirikiana kila mmoja anamvamia mwenzake kwa kutomuelewa.

Mwanaume ameshindwa kuwasiliana vizuri kufahamu nini kiliendelea wakati hayupo na mke ameshindwa kuelewa hitaji la mume wake na kuwa naye romantically pia suala la majukumu na ndugu limekuwa kichwani kwa mwanamke hadi hawezi kutambua umuhimu wa mume wake ambaye hata baada ya watoto kukua na kuondoka atabaki naye.

Mawazo yako

DM Dar es Salaam

Anonymous said...

Binafsi naona kwamba hawa wanandoa tatizo kubwa hakuna anaekubali kushuka chini na kunyenyekea,kwani kwa maelezo haya,kila mtu ana haki kulalaimika lakini unalalamika wakati gani?na je hasira ndio solution ya tatizo?mimi naona wanahitaji kutambuana zaidi kwani naamini ukimtambua mtu tabia yake unaweza kum handle,watambuane weakness zao,wataweza kuishi.Aunt Eve,Dar es salaam

Lazarus Mbilinyi said...

Asante kwa maoni mazuri hapo juu,
Ni kweli kuna sababu nyingi ambazo zimefanya hawa wanandoa wakasirikiane na hata kuwa na usiku mgumu.
Tukubaliane kwamba kuna tofauti kubwa sana katika kutafsiri maana ya message kati ya mume na mke na kama tukitambua tofauti zilizopo basi haina haja kukasirikiana (anger).
Kutokana na mfano hapo juu ni dhahiri kwamba wanandoa wamekosa skills za kutafsiri messages ambazo kila mmoja alikuwa anawasilisha kwa mwenzake.
Kwani mke na mume siku zote huwasiliana kwa "codes" na tatizo ni kwamba hawafahamu namna ya kutafsiri (decipher) ujumbe ambao mwenzake ametuma au amepokea.
Mume asipoelewa mke anaongea kitu gani matokeo yake huonekana ni careless, na mke hujiona mume hampendi (love) na hamjali kitu ambacho husababisha aanze kuwa critical na kutoa kila aina za complaints kitendo ambacho mume hutafsiri kwa kuona mke hamheshimu (respect) kitu kinachosababisha waendelee kuzunguka kwenye hilo dubwana la hasira kila siku hadi mmoja atakapoamua kushuka na kukubali kwamba nimekosa.
Kufahamu kwamba mawasiliano ni muhimu katika ya mke na mume haitoshi bali kufahamu namna mwanamke na mwanaume wanavyotafsiri ujumbe ndiyo jambo la msingi.

MFANO:
Asubuhi umefika mke na mume wanataka kuvaa nguo na kwenda kazini; mke anasema "sioni nguo ya kuvaa leo" maana yake hana nguo mpya.
Mume anasema "sioni nguo ya kuvaa leo" maana yake hana nguo safi.

Bila kufahamu tofauti ndipo migongano huanza na kuharibu siku.

Upendo daima