"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, May 6, 2010

Upendo wa kweli!

Upendo wakati mwingine hufananishwa na kupanda na kushuka kwa nyuzi joto.

Ni ukweli usiopingika kwamba upendo ambao hutokea wakati wa uchumba ni tofauti na ule wa kwenye ndoa.

Pia katika hatua ya uchumba wahusika wengi huwa na mtazamo wa kufurahishana ili kufahamiana kunakopelekea kuoana; wakati kwenye ndoa ni maisha, majukumu na kazi.

Wengi huamini kwamba kwa kuwa wanapendana sana kwenye uchumba basi safari ya ndoa yao itakuwa tambala kama mawindoni kitu ambacho si kweli kwani kitendo cha kuvalishana pete (hata kama dhahabu inatoka south pole au sayari nyingine) pamoja na kipande cha karatasi unachotia saini haviwezi kukufanya uwe mzuri kumpenda mke wako au mume wako ambaye umefunga naye ndoa.

“True love is a Process”

Unapokuwa engaged unajisikia raha sana (in your fantasy land) kwani zile hekaheka za mipango na maandalizi ya ndoa/harusi, matarajio ya honeymoon, furaha ya kumpata kiumbe ambaye ulikuwa unamsubiri miaka yako yote duniani hukufanya ujisikie raha na binadamu uliyebarikiwa.

Hata hivyo itafika siku wala si mbali hizo feelings hazitatosha kuifanya ndoa yako idumu na kudumu.

Utatakiwa (unatakiwa) kuendelea kuijenga ndoa hatua kwa hatua kila siku na kuendelea kumsoma mwenzi wako kufahamu ni vitu gani anavipenda na akivipata basi humfanya ajione anapendwa (mwanamke) na anaheshimiwa (mwanaume).

Je, unapompa mke wako au mume wako zawadi huwa unatafuta zawadi ambayo wewe unaipenda au anayoipenda yeye?

Je, unafahamu kwamba hata namna ya kuipokea zawadi kutoka kwa mpenzi wako ni vizuri kujua jadi yao?

Kuna wengine unapopokea zawadi bila kushukuru kwa kuruka ruka (excitement) huku ukamwambia kwa kumthibitishia kwamba umeipenda na ulikuwa unapenda sana kupata kitu kama hicho maishani mwako hata kama zawadi anayokupa haigusi moyo wako.

Watu kama hao usiporukaruka kuipokea watakwambia hujaipenda na vita kuu yab tatu ya dunia inaweza kuanza!

Wapo wengine akisafiri na siku amerudi ile kukutana mara ya kwanza lazima utoe machozi kuonesha ulimkumbuka (ulim-miss) bila kutoa machozi na kutengeneza kamsiba kakiana atahisi huna feelings na yeye na kwamba humpendi!

Kupenda ni kazi na kazi kubwa ni kumsoma mwenzako maeneo ambayo unaweza kumfanya ajisikia ana mtu bora duniani anayempenda na kumjali.

Mungu akubariki

God bless you

Gott segne dich

Que Dieu vous béniss

Må Gud välsigna er

神の祝福あれ

قد بارك الله فيك

No comments: