"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, May 5, 2010

Usizunguke!

"...Around the bush!"

Wanaume na wanawake ni tofauti na hilo halina ubishi, mwanaume hawezi kuwa mwanamke na mwanamke hawezi kuwa mwanaume jambo la msingi ni kusherehekea tofauti zilizopo na kujitahidi kufahamu hizo tofauti ili kuleta furaha katika mahusiano.

Moja ya tofauti ni kwamba wanaume kawaida hawapendi kukanganyisha (complicate) vitu.

Hawapendi kuzunguka, hawapendi maelezo mengi, hawapendi “to beat around the bush”, hawapendi maneno mengi na hawapendi kuzunguka kujibu swali au kuuliza swali badala yake wanapenda maelezo mafupi na yanayoeleweka.

Wanaume ni problems solvers au dissolvers, ukimuuliza swali hata kabla hajamaliza kujieleza na swali lako anakukatiza na kukupa jibu palepale na kukwambia “kwa nini usifanye hivi na hivi........”

Tofauti na wewe mwanamke ambaye unampomuuliza mwanaume swali unaamini kwanza atakusikiliza kwa makini pia atashirikiana na wewe kulijadili hilo swalia hata hivyo kwa mshangao anaanza kukujibu kabla haha hujamaliza kuuliza.

Mwanaume hayupo interested na kusikiliza yupo interested na kutoa solutions.

Hii ina maana gani?

Ina maana kwamba huwa hapendi namna unvyosogoa sana kuelezea jambo dogo tu.

Kwa maelezo zaidi soma hapa na hapa ni muhimu sana!

No comments: