"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, May 13, 2010

Wanadanganya acha!

Wanaume wanao cheat wanaamini kusema ukweli kuhusiana na cheating zao ni wazo baya sana.

Wanaume hawa hudanganya wake zao, washauri wao, wanaume wenzao, wachungaji wao, wazazi wao, ndugu zao na kila mtu anayopita katika anga zao.

Wanaume hawa hudanganya hadi wanahakikisha uwongo wao wote umeisha na hawana namna tena ya kudanganya ndipo hukubali yaishe.

Hii ina maana kwamba ukihisi kuna uwezekano kwamba anachepuka (cheat, astray) kwanza atakufunga kamba kwamba hachepuki nje na pili ikitokea ukamkamata, atakufunga kamba suala zima la kuchepuka kwake.

Kuna kisa kimoja cha mwanaume ambaye baada ya mke wake kumshukia kwamba ana mke nje na amesababisha maafa kwa familia walipelekana mahakamani.

Hata hivyo mwanaume alikataa kata kwamba huyo mwanamke (anayetuhumiwa naye au hawala yake) hamjui na tangu anazaliwa hajawahi kumuona.

Ndipo hakimu naye akampa drill ya uhakika kwa maswali bado mwanaume aliendelea kudanganya kwamba hamjui tangu anazaliwa.

Na hawala yake mwenye alipoulizwa kama anamfahamu huyo mwanaume yeye akasema ndiyo namjua na nashangaa kwa nini ananiruka kwamba hajawahi niona tangu nazaliwa wakati wiki iliyopita tulikuwa wote na ninamfahamu hadi nguo zake za ndani.

Bado mwanaume akakataa kwamba hamjui na akasema mke wake na huyo hawala wanamsingizia tu.

Ndipo ukaletwa mkanda wa video ambayo ulichukuliwa (taped) na private detective agent ambao mke wake aliwapa kazi ili wamnase mume wake na cheating zake.

Wakaona mwanaume wa watu jasho jembamba linamtoka, macho yakaanza kulengalenga na midomo imeshikwa na ganzi maana sasa kila mtu aliona upuuzi wake wote aliokuwa akifanya na huyo hawala yake.

Akiulizwa je, bado unaweza kuendelea kudanganya?

Ndipo akakiri kwamba alikuwa anadanganya kwa sababu hakujua kama wana video na picha hivyo anakubali yaishe.

Hivyo wanaume wa aina hii hudanganya hadi wanafika point hawawezi tena kudanganya ndipo hukubali yaishe vinginevyo hudanganya hadi mwisho.

Mwanaume anavyozidi kuwa msomi ndivyo na uwongo wake unakuwa wa kisomi zaidi kwani mwongo ni mwongo tu na baba yao ni mmoja anaitwa shetani.

Kawaida baada ya mwanaume cheater kusema ukweli kuhusu cheating zake hujiona maisha yameisha kwani hujiona ni loser na kuwa loser si kitu rahisi kwa mwanaume.

Hujiona uhuru wake ameshaupoteza na kwamba sasa kila hatua anayoipiga kutembea atakuwa anachungwa ni kama video camera itakuwa inamfuata kila anapenda.

Je, kwa nini wanaume cheaters ni waongo?

UHUSIANO WAO NA WAZAZI WAKIWA TANGU WATOTO:

Mtoto wa kiume anapokuwa katika mazingira ya nyumbani wazazi kumlazimisha kuonekana anafanikiwa kila eneo la maisha yake kama vile masomo, michezo, masuala ya jamii nk na inafika wakati anakuwa amechoka (saturated) na kuambiwa ajitahidi hivyo huanza kudanganya (white lie) kama vile anaweza kumfunga kamba mama yake au baba yake na kuwambia leo shuleni nimeongoza Hesabu, au leo nilifunga goli la ushindi kwa timu yangu shuleni kitu ambacho si kweli na hufanya hivi ili wazazi wajisikie vizuri na nyumbani kuwe na amani, ndo imetoka hivyo katoto kanakua huku ni kaongo.

KULINDA HADHI:

Mwanaume anapojifahamu kwamba kuna watu wanaomzunguka wanamtazama hulazimika kufunika au kuficha tabia ambayo anafahamu jamii inayomzunguka wanafahamu kwamba haikubaliki, kwa kuwa ana reputation kwenye hiyo jamii anaamini watu kufahamu kwamba siyo mwaminifu kwa mke wake na watoto atakuwa ana ruin reputation ambayo ameijenga kwa muda mrefu.

Hivyo anaamini kudanganya ndiyo permanent solutions!

KUEPUKA KUGOMBANA:

Kuna wanaume hufanya kila analoweza kuogopa confrontation kutoka kwa wake zao, wanaogopa kuwa na drama kubwa nyumbani wakati hajakamatwa au kufumaniwa. Hivyo kwa kuwa mke hana ushahidi wa kutosha kwa nini akubali ili waanze kugombana si afadhari adanganye kwa ustadi wa hali ya juu then yanaisha.

HUJISIKIA RAHA:

Kuna baadhi ya wanaume wao kufukuzia wanawake ni “to have fun and enjoying life” haijalishi wana umri gani, wana wadhifa gani katika jamii, au wamesoma kiasi gani au maskini au matajiri wao wakiona skirts tu suruali zao mikanda inalegea yenyewe. wanaopenda sana company ya wanawake nje ya ndoa zao na wakati huohuo hawataki kuwaacha wake zao.

Wanaume wa aina hii wanawapenda sana wake zao (siyo wote) na hawana mpango wa kuishi bila hao wake zao, wanaamini kuna kitu exciting huko wanakoenda (adrenalin boost)

Hawajali wake zao wanaume kiasi gani au watoto wao wanaumia kiasi gani wao ni kama mawe hawana feelings.

HAWATAKI LAWAMA:

Kuna wanaume wanafahamu kwamba wakikamatwa wake zao watawapa talaka na kwamba watapoteza mali na familia (lose the battle) hivyo hudanganya ili kukwepa hizo lawama.

WANAUME AMBAO NI CHRONIC

Hawa hudanganya kila kitu, watadanganya kipato, namna walivyo wazuri kufanya kazi, namna wanavyopenda familia zao ni ma-experts .

Wapo smart kudanganya na uwongo wao ni mtamu, kama talent vile, uwongo upo kwenye DNA, ni tabia yao ipo ingrained kwenye damu yao.

Yaani mke anafungwa kamba hadi anakuwa upande wake kumtetea.

Ni kama wana pepo la kudanganya!

NB:

Bila kuokolewa na Mwanaume Yesu hata magereza hayawezi kuwafanya waache uwongo wao.

Ufunuo 21:8

No comments: