"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 30, 2010

Wanafika kwa tofauti


Wanaume hufurahia sana kufika kileleni (orgasm).
Hata kama ni sekunde chache hata hivyo zinalipa zaidi kuliko raha ya hekaheka zote hadi kufika hapo.
Ni kweli kwamba mwanaume na mwanamke ni tofauti sana linapokuja suala la kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa.
Mwanamke anaonekana ndiye mwenye uwezo zaidi wa kuwa na wakati mrefu wa kukaa kileleni na pia ana uwezo wa kujirudia kufika kileleni zaidi ya mara moja.
Pia inaeleweka wazi kwamba ni rahisi sana kwa mwanaume kufika kileleni kuliko mwanamke kwani ni wanawake wengi ambao pamoja na kushiriki tendo la ndoa bado hawajawahi kufika kileleni wakati itakuwa gumzo ikitokea kwamba kuna mwanaume ameshashiriki tendo la ndoa na hajawahi kufika kileleni, hayupo!
Pia mwanamke anao uwezo wa kuthibiti kufika kileleni, hata kama mwanaume ataweza kuthibiti kumaliza mapema (ejaculate) kabla hajafikia point ya no return, hata hivyo akishafika hiyo point hawezi kusimama au kugoma asifike kileleni.
Wakati huohuo mwanamke anaweza kuwa alikuwa kileleni na akasikia mtoto analia, anaweza kuacha na kumhudumia mtoto na kuanza kila kitu upya.
Tofauti nyingine katika kufika kileleni kwa mwanaume na mwanamke ni wakati kwa maana kwamba kwa mfano mume amesafiri kwa wiki mbili kwa ajili ya business, mwili wa mwanamke huweza kujizima kiana kwa sababu hayupo sexual active na atahitaji muda zaidi kuupasha mwili kuwa tayari kwa sex na hatimaye kufika kileleni.
Mwanaume kwa upande mwingine ni kinyume na mwanamke, kama hakuwa na sex kwa wiki mbili basi mwili wake utajaza risasi za uhakika na siku akikutana na mke wake hatachukua muda kufika kileleni, kwanza ile kumuwaza mke wake tu tayari Mr. Happy anaanza kufanya vitu vyake (erections).
Jambo la msingi ni mume na mke kufahamu tofauti zilizopo na kuzifanyia kazi ili kusherehekea kitendo cha kuishi pamoja.

Tuesday, June 29, 2010

Je, Kuna Sababu?

SWALI:

Kaka Mbilinyi, kwanza nashukuru sana kwa elimu unayotoa hapa, mara nyingi napita hapa kujipatia tips kwa ajili ya maisha yangu ya mahusiano.

Nami leo nina swali ambalo linanitatiza kwani kawaida Mr. Happy wangu huwa hana tatizo kuwa na erections usiku nikiwa nimelala usingizi au ninapoamka asubuhi, hata hivyo ninapojaribu kufanya sex na mke wangu huyu jamaa ananiangusha mno hataki kuamka, je kuna sababu yoyote?

Jina kapuni

JIBU:

Kaka Jina Kapuni,

Asante sana kwa kupita hapa na kuchukua kile ambacho unaamini unaweza kujifunza.

Kawaida Mr. Happy huwa na erections asubuhi au katikati ya usiku kwa mwanaume yeyote na aina hii ya erections ni tofauti na ile ya Wakati wa sex (sexual erections).

Erections za usiku au asubuhi mwanaume anapoamka (hata watoto wa kiume au vijana wa kiume) ni sehemu ya asili ya mwili (natural body reflex), na hizi erections hutokea kila baada ya dakika 90 ukiwa umelala usingizi.

Unapotaka kufanya mapenzi (sexual erections) hutegemea sana ubongo, mishipa (nerves), mirija ya damu (blood vessels), stress, kuchoka, hofu, mashaka na wasiwasi hayo yote huweza kusababisha Mr. Happy kulegea badala ya kutabasamu na kusimama kukupa salute.

Hayo niliyotaja hapo juu hayana uhusiano wowote na zile erections za usiku na asubuhi unapoamka.

Pia wanaume huwa na kiwango kikubwa sana cha testosterones Wakati wa asubuhi ndiyo maana wanaume wengi hupenda sex asubuhi kuliko wanawake.

Habari njema kwako ni kwamba kama unapata erections usiku ukilala au asubuhi unapoamka maana yake huna tatizo la mishipa ya damu au hormones au nerves kila kitu kipo plugged vizuri kwenye system yako.

Uwezekano mkubwa wa wewe kukosa sexual erections itakuwa ni stress au situation zako kimaisha kama vile kazi, familia, au kukosa kuwa stimulated vizuri kimapenzi (kama umri wako umeenda sana).

Jichunguze kama kuna mgogoro wowote au jambo lolote linalokufanya ufikirie au kuumiza ubongo muda wote.

Pia unaweza kumuona daktari ambaye anaweza kukusaidia kukupa medications ambazo zinaweza kuongeza penile circulations.

Monday, June 28, 2010

Usiruke, Jadili

Mara nyingi ukisikiliza mazungumzo ya wanandoa watarajiwa (wachumba ambao wapo kwenye maandalizi ya harusi na ndoa yao) mara nyingi utasikia mambo mbalimbali yanayohusiana na maandalizi ya sherehe za harusi.

Watanunua kila kitabu kinachoelezea namna gani mavazi yanaweza kupendeza, watahangaika miezi karibu yote kuhakikisha wanapata rangi za harusi, mtindo wa nywele, vyakula vya waalikwa, ukumbi, magari ya kuwasafirisha maharusi na wageni waalikwa, namna ya kuhakikisha kila mgeni atashiriki vipi sherehe nk.

Inasikitisha sana kwamba ni wachache sana hutumia muda wao kuongea na wachumba wao kukaa na kila mmoja kuelezea matarajio yake hukusu sex itakuwaje.

Ngoja nikwambia kitu wazi na halisi, wiki tatu baada ya harusi yako, hakuna hata mtu mmoja atakuwa anakumbuka wewe bibi harusi ulishika ua gani mikononi siku ya harusi yako, hata hivyo issue ya matarajio yako kuhusu tendo la ndoa lita shape maisha yako na mwenzi wako na zaidi namna ndoa itakavyokuridhisha kwa zaidi ya miaka 20 au 30 au 40 na hata 50 ijayo.

Wewe ni mwanamke, inawezekana utakuja kushangazwa sana na huyo kijana ambaye ni mchumba wako kwani inawezekana kichwani mwake anatarajia wewe utaweza kumridhisha kimapenzi usiku na mchana na kila wakati anapokuhitaji kimwili na wakati huohuo wewe unaamini tendo la ndoa ni siku tu tena taa zikiwa zimezimwa na watu wote wakiwa wamelala fofofo mita 100 kuzunguka chumba chenu cha kulala.

Tafadhari sana kama unataka kuolewa au kuoa hivi karibuni ni muhimu sana kukaa chini na huyo mchumba wako weka kila kitu wazi kwa kila mmoja kuwa specific nini anatarajia kwenye ndoa kuhusiana na suala la sex tena ikiwezekana kuanzia siku ya honeymoon.

Muulize nini anahitaji na nini hakihitaji.

Sunday, June 27, 2010

Hata kwa Simu

Kama unaishi nchi zilizoendelea (mfano USA, Canada au Uholanzi), ukinunua gazeti (local news paper) kwenye hizi nchi unaweza kukutana na matangazo ambayo yana namba ambazo mwanaume hulipa zaidi ya dola 3 ili kumsikiliza mwanamke (kwa dakika moja) ambaye anaongea kimapenzi (wenyewe wanaita phone sex).

Bila shaka hii ni kuonesha namna dunia imelemewa na kwamba inaishia ukingoni, hata hivyo ili business kama hii iweze kudumu maana yake kuna kitu behind it. Kinachoshangaza inakuwaje wanaume huamua kupiga simu kwa kulipia ili kusikiliza hao akina dada wanaowaongelesha kimapenzi?

Msingi wa hili jambo unajikita kwenye uwezo wa maneno tunayoongea (power of words), wakati mwanamke anaongea kitu fulani mwanaume huwa na picha kamili (visualization) na hayo maneno yanaweza kumfanya mwanaume kufika kileleni (orgasm)

Je, unajua hao wenye business hii wanasemaje kuhusu aina ya wanaume ambao hutumia hii huduma au huamua kulipa dola zao ili kupata hiyo services ya phone sex kwa umbali wa maelfu ya miles (mwanaume anaweza kuwa British Colombia Canada na mwanamke yupo Las Vegas California USA)?

Ni wale wanaume ambao wake zao kila siku huwapa dose ya;

Naumwa kichwa, sijisikii vizuri, leo nimechoka, leo hapana, siyo hapa, utaamsha watoto, tumbo linaniuma, tutafanya kesho nk

Bottom line ni kwamba:

Maneno unayotumia chumbani na mke wako au mume wako si kwa ajili ya yeye kusikia tu bali hutunzwa, hufundisha na kuwekwa kwenye kumbukumbu, ukirusha neno gumu na la kuumia unaweza kushangaa namna mke wako au mume wako atakavyobadilika na kuwa mtu tofauti huko chumbani.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

Saturday, June 26, 2010

Wanawake tu, ... (mwisho)


Mama mmoja alikuwa anamuogesha mtoto wake wa kiume wa miaka 4 alishangazwa na maelezo ya huyo mtoto pale alipomwambia mama yake
“Mama Unajua nampenda sana mdudu wangu (ka Mr. Happy kake)”
Huku ameshika na kumuonesha mama yake bila wasiwasi.
Kwa aibu mama yake akaanza kutoa maelezo ya ziada zaidi kuhusiana na anatomy ya mwili wa binadamu kwa kumwambia mtoto
“Ni kweli Mungu ametuumba na ametupa mikono, vidole, magoti, masikio, pua na miguu na kila kiungo kina umuhimu na maana katika mwili”.
Yule mtoto hakujibu chochote wakati mama yake anaongea na baada ya mama kumaliza maelezo yake mtoto akaendelea kusisitiza kwamba
“Lakini mama, bado mimi napenda sana mdudu wangu”
Kuna vitabu vinaeleza kwamba “the man’s best friend is a dog, si kweli, ukweli ni kwamba rafiki wa kweli wa mwanaume ni Mr. Happy wake ambaye urafiki (bonding) huanza mapema tangu mtoto.
Na kila siku inayopita duniani ni lazima amshike kwa mikono yake si mara moja tu bali zaidi ya mara moja na si kushika tu bali kumuona kwa macho yake.
Sidhani kama kuna mwanaume ambaye kila akienda “for peeing” huwa hashiki au kumuona Mr. Happy wake.
Kama tunavyomwita Mr. Happy kwa maana kwamba yeye hufurahia kila siku na kutabasamu kila wakati bila kujali jana au juzi alihudumiwa vipi, kama ni mke au mke mtarajiwa lazima ufahamu kwamba unahitaji kuwa comfortable kuwa naye na si kuwa naye tu bali kumfahamu namna anatakiwa kuhudumiwa ili kumridhisha mume wako.
Hata kama kuna wanawake Wachache ambao siku ya kwanza ya kuona genitals za waume zao hukiri kwamba ni kweli hawajawahi kuona kitu ugliest katika maisha yao kama hapo kwenye residency ya Mr. Happy.
Hata kama ni kweli ni vizuri kuwa siri yako wewe mwenyewe mwanamke kwani na huko south pole kwako si kupo ugly pia.
Ngoma droo!
Kama mume wako ni kijana wa miaka ya 20+ au 30+ inawezekana Mr. Happy kila akikuona half naked au hata kupanda tu kitandani yeye hukuinulia salute kirahisi, ukweli ni kwamba namna mume wako anavyozidi kuongeza umri maana yake utahitaji kazi zaidi ili akupe the same salute haraka haraka.
Pia tukumbuke kwamba wanawake wengi wanapoolewa huwa hawapewi Manual au sexual instructions ya namna ya kumhudumia Mr. Happy ni vizuri sana kukumbushana.
Kwa wale wa darasa la kwanza ni vizuri kufahamu kwamba Mr. Happy ana maeneo tofauti ambayo huwa sensitive kuliko eneo lingine.
Maeneo ambayo yupo sensitive ni upande wa chini ya shaft na kichwa, ni vizuri sana kumpa attention ya ziada kwenye michirizi (ridge) ya chini ya kichwa kwani kuna eneo ni sensitive kuliko kawaida kama likihudumiwa vizuri (both manual and orally) kwani ukimpatia unaweza kuona mume wako anaruka na kugonga dali (ceiling).
Mr. Happy amezungukwa na sensors za kila aina, stroke tofauti kwenye shaft huweza kumpa mume feelings za ajabu kiasi cha kumfikisha kwenye msisimko wa uhakika. Unapojikita kwenye maeneo ambayo ni more sensitive maana yake anaweza kufika kileleni haraka zaidi. Mwanamke anayefahamu kumhudumia Mr. Happy anafahamu namna ya kumfanya Mr. Happy kusimama (aroused) bila kumfikisha kileleni.
Jambo la msingi ni kufahamu namna ya kumpandisha hadi karibu na kilele cha mlima na kumrudisha tena ground zero over and over kwa strokes tofauti, touch tofauti, caresses tofauti iwe polepole, haraka haraka, nyepesi au nzito vyote humpa uhondo mume wako.
Kuna wakati mume wako atahitaji direct stimulation na kuna wakati atahitaji indirect stimulation kwani ikienda kinyume chake anaweza kumaliza mapema na wakati mwingine Mr. Happy hufanya yale ambayo hakutumwa kama vile kuamua kwenda kulala mapema kabla ya muda.
\jambo la msingi ni wewe mke wake kufanya ugunduzi ili kufahamu namna mwili wa mume wako unavyofanya kazi, si mke tu ambaye hufurahia kukunwa mgongo au mguu au kichwani hata mume pia.
Ubarikiwe.

Friday, June 25, 2010

Wanawake tu, walioolewa


Mr. Happy
Mara zote yupo tayari, Mr. Happy huwa hafuati ratiba (schedule), ukweli Mr. Happy hajui hata ratiba ni kitu gani na hufanywa vipi pia Mr. Happy ana kumbukumbu ndogo sana (short memory).
MFANO:
Wewe na mume wako mlikuwa na wakati mzuri sana usiku wa jana (love making) na kila mmoja aliridhika na kujiona ametosheka. Asubuhi wewe mwanamke unaamka mapema na kuamua kufanya usafi chumbani huku mumeo bado amelala. Unaamua kuvaa tu T-shirt bila bra ndani na katika inama matiti yanaonekana kuchezacheza ndani ya T-shirt uliyovaa kiasi cha kumvutia mumeo ambaye anaamka kuamka na kuja kukupa hug kwa nyuma na unagundua bila shaka kwamba Mr. Happy wake ameshaanza kutroti na haoneshi dalili kwamba amelala.
Unajiuliza
“Tulifanya sex jana usiku tu, sijaoga bado, nimevaa ovyo, hivi mume wangu ana tatizo gani kunitaka tena asubuhi hii yote wakati anafahamu ninafanya kazi?”
Ukiongea na wanandoa ambao huridhishana watakwambia kuna kitu kinaitwa ‘spontaneity or quickies, chapuchapu, kimoja cha haraka nk”
Kwa kuwa mwanaume huvutiwa na kile anaona, ile kumuona mke wake na headlights, au katika chupi yake au akitoka kuoga na khanga yake kwa tukio kama hilo mume anaweza asijali atachelewa kanisani au kazini au mkutanoni kwani anakuwa ameshaigusa trigger na kwake kinachofuata ni kutoa risasi.
Wapo wanawake ambao wameamua kuwapa waume zao sex wiki mfululizo wakiamini kwamba itasaidia kuwafanya waume zao kupunguza uhitaji wa sex hata hivyo wiki inayofuata mume anakuwa na libido ya juu kuliko wiki iliyopita.
Hawajajua Mr. Happy yeye hana tatizo kwani huwa hatunzi kumbukumbu za nini kilitokea jana au wiki iliyopita anachojua yeye ni sasa na anatunza smile lake kila iitwapo leo.
Mwanaume ni mwanaume na atabaki mwanaume na moja ya sifa ya mume ndani ya ndoa ni ule uhitaji wa sex kwa namna ya tofauti.
Kama ulihitaji mtu ambaye atafanya mambo kama unavyohitaji wewe kimapenzi basi ulitakiwa kubaki single, lakini umeoana na mwanaume ambaye ana mahitaji tofauti na wewe na moja ya mahitaji muhimu kwake ni sex.
Pia ieleweke kwamba kuna siku mume anaweza kuamka akiwa na full erections, anaweza kuku-approach na wewe ukakataa, hata hivyo kukataa kwako hakuwezi kupunguza hamu yake ya kukuhitaji wewe kimwili.
Kuna wakati hitaji la sex kwa mwanaume huwa mfano wa kitu cha urgent, anahitaji sexual release, kama ni bunduki yake basi huwa inakuwa ipo loaded na risasi ya mwisho imeshawekwa kwenye chamber, na jicho limeshawekwa kwenye target huku trigger imeshavutwa nyuma ili iweze kuruhusiwa hivyo kukataliwa kwake huwa ni kitu frustrating na hujiona ni loser.
Nikupe Tips za kukuhakikishia wewe mwanamke unakuwa na moto wa mapenzi chumbani.
KWANZA
Panga kabajeti kadogo baada ya muda fulani kwa ajili ya kununua kivazi (lingerie) ambacho unaamini ukivaa kinaweza kumvutia mumeo chumbani
PILI
Angalau kwa mwaka mara moja nenda kwenye social event yoyote na mumeo huku hujavaa chupi, usimwambie mumeo hadi muwe mmeshaondoka nyumbani na mnong’oneze sikioni na mwambie “honey unajua leo sijavaa chupi” utamfanya akuwaze siku nzima huku wewe mwenyewe ukisisimka mara kwa mara ukikumbuka chini ni empty!
TATU
Baada ya siku kadhaa “have fun” na mumeo chumbani unaweza kuwa naked kwa muda unaotaka wewe kwa ajili ya kufurahia reaction yake inakuwaje.
NNE
Tafuta aina mpya ya perfume ambayo siku ukijiweka basi ni siku ambayo unakuwa na mahaba ya uhakika na mumeo hivyo basi kila mara ukitaka maana yake unahitaji mahaba pia.
TANO
Jaribu kitu kipya kimoja baada ya muda fulani kwa ajili ya kumsisimua mume wako.
SITA
Fanya mazoezi ya misuli ya PC
Tutaendelea....................
Nikutakie weekend njema

Thursday, June 24, 2010

Mwanamke kujiamini

Kwa mwanamke yeyote ni muhimu sana kufahamu kwamba mwonekano wako ni muhimu sana kwa mume wako pia ni secret weapon ya kuweza kumsisimua mume wako kimapenzi.

Jane ni mwanamke ambaye kifua chake ni flat (small breasted) na hushindwa kujiamini (poor self image). Kabla ya kurudi nyumbani anaamua kununua jarida linalohusu mambo ya wanawake, anapoendelea kulisoma anapitia matangazo yote ya biashara anakuta ni picha za wanawake (models) ambao hakuna anayefanana na yeye (kifua), anapoendelea na safari anajikuta kila alama za matangazo (billboards) anaona picha za warembo ambao wapo na wanaume aidha wakivuta sigara au kupata kinywaji au onesha gari hata hivyo hakuna anayefanana na yeye kifua kuwa flat.

Anapofika nyumbani jioni anawasha TV ili kutazama na anakutana na matangazo ya wanawake warembo headlights kubwa kubwa zikiwa nje nje.

Usiku anapenda kulala anavua nguo na kujiangalia namna matiti yake yalivyo madogo na kujisemea mwenyewe

kwa nini nisiongeze ukubwa kidogo wa haya matiti yangu

Tatizo ni kwamba anadhania, anafikiri kwamba mume wake hawezi kuwa turned on na hayo matiti yake madogo kwa sababu hafananani na wale wanawake kwenye matangazo, magazeti na TV.

Hafahamu kwamba mume wake pia hafanani na wanaume ambao wanapatikana kwenye magazeti, matangazo na TV.

Katika ulimwengu halisi (real world) huwezi kukutana na hao wanawake na wanaume wa kwenye matangazo, magazeti na TV, wengi ni wa kutengenezwa kwa kupakwa rangi, kusafishwa sura kwa teknolojia na Urembo wao si wa kweli.

Tatizo la Jane si kwa sababu ni kifua kuwa flat bali ni victim wa nguvu za kudanganya za mambo ya Urembo.

Hajiamini kiasi cha kujiweka huru kwa mume wake kimwili kwa kuogopa kwamba badala ya kumsisimua anaweza kumgandisha kwa baridi ya kile ataona.

Inawezekana umeshazaa watoto 2 au 3 au 5 na una stretch marks kiasi kwamba unaogopa kuwa huru kwa mumeo.

Inawezekana tangu uzae umeongeza uzito kila 10 nzima na unajiona completely unlovely kiasi kwamba mume wako akikwambia unamvutia unaguna na kujifunika zaidi asikuone sehemu za mwili wako.

Anakwambia mwili wako unamvutia na kumsisimua, wewe unakata na kuficha, kazi kwelikweli!

Unaacha kumsikiliza mume anayekupenda, unawasikiliza watu wanaotaka kuuuzia wewe products zao kwa njia ya matangazo.

NGOJA NIKUPE TIPS

KWANZA

Jikite kwenye uimara wako:

Je, unafahamu mume wako ni kitu gani anakipenda, au anavutiwa zaidi katika mwili wako, kama hujui tafuta au fanya utafiti.

Wanaume huvutiwa na mwanamke au mke wake in packets, yaani anaweza kuvutiwa na mguu wake, shingo, headlights (matiti & chuchu), nywele, macho, uso, kiuno nk.

Kama mume wako anavutiwa na matiti yako basi focus hapo hapo kwa kununua bra, au nguo ya usiku ambayo ukivaa ataacha shughuli zote na kubaki anatazama kifua chako.

Kama ni macho au lips basi fanya kila unaloweza kuhakikisha anapata raha yake na wewe utajisikia kujiamini zaidi.

“Use what you have to full effect and don’t worry about the rest

PILI

Shukuru Mungu:

Kumbuka hukutengezwa au kudundwa kiwandani na wafanyakazi waliokuwa wanafanya overtime siku ya Ijumaa, bali uliumbwa kwa ustadi (designed, crafted, molded & sculpted) na Mungu mwenyewe na ulipozaliwa alikuangalia kwa smile na kukiri kwamba “this is good”

Hivyo mshukuru Mungu kwa kukupa mikono ili uweze kutumia kumpenda mumeo.

Mshukuru Mungu kwa kukupa lips ili umbusu mumeo nk.

TATU:

Kaa mbali na mazingira ambayo huwezi kumudu.

Mpendwa kama unajiona ukivaa swimsuit unaonekana kituko kwa nini ujilazimishe (na swimsuit za siku hizi kwa wanawake ni balaa), kwa nini usivae shorts ili kufunika zaidi na kuendelea ku-enjoy kuogelea.

NNE:

Jifunze kuridhisha hisia zako (sensual)

Hapa si sex bali, kwenda Mahali patulivu wakati wa jua na kunywa soda yako baridi, kukaa na mume wako chumbani huku akikufanyia massage kwenye miguu yako baada ya mizunguko ya siku na maisha, kutumia muda wako siku ya baridi kali kuwa na hot bath nk.

Ni raha sana kuwa na mke sensual huku akiwa umeongeza kilo kadhaa kuliko kukaa na mke ambaye anajilinda na kuongeza uzito ila si sensual.

TANO:

Sex mara kwa mara

Watu ambao hufika kileleni mara kwa mara huweza kusababisha kuzalishwa kwa hormones ambazo huimarisha immune system katika mwili na kupunguza kuonekana mzee.

Utafiti wa watu 3,500 (Royal Edinburgh Hospital) ulionesha kwamba wale walioonekana ni wazee wakati umri wao ni sawa na wenzao walikuwa wanakwepa sex katika ndoa zao.

Have lots of sex

Unapojipa sex maana yake mume wako anafurahia na kukufurahia na anakupenda na matokeo yake utajiamini.

Wednesday, June 23, 2010

Wanapoongeza Umri!

Wanahakikisha wametumia kila kipande cha furniture ndani ya nyumba.

Kwa wanawake anapofika umri fulani huweza kufanya mabadiliko makubwa ya kuongezeka kwa umri kitaalamu menopause.

Kisaikolojia ni kama kuna kuwa na mstari ambao huchorwa kuelekeza kwamba sasa huwezi kuzaa tena.

Hata hivyo jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba mwanamke anapofika huo umri pamoja na kwamba hawezi kuzaa tena anaweza kujihusisha ukaribu wa kimapenzi na mume wake bila tatizo wala kuwaza kuhusu mimba.

Ingawa ni kweli wanawake wengi hujikuta wamepoteza kiwango cha hormone za estrogens bado wanaweza kuwa na libido kubwa kabisa na kuendelea kufurahia intimacy na waume zao.

Ingawa ni kweli kuna baadhi ya wanawake wakifika hii hatua hupoteza hamu ya tendo la ndoa hata hivyo kuwa wengine wameripoti kwamba baada ya kufikia hatua wa menopause hujikuta wakitumia kila kipande cha furniture ndani ya nyumba au kila chumba kuhakikisha kinahusika na adventures za mahaba.

Pia faida ya wanawake ambao wameshapita umri wa kuzaa wanakuwa hawapati siku hii ina maana wanapata nyongeza ya siku 3 au 5 ambazo walikuwa wanatumia kwa kupata siku na sasa zitakuwa free kwa ajili ya sex.

Ingawa kimwili aina hii ya wanawake wanahitaji kuwa makini na genitals kwani kupungua kwa kiwango cha homoni za estrogens husababisha kuta za uke kuwa nyembamba zaidi na kavu zaidi, atahitaji kutumia lubrication zaidi na pia mume muelewa kwani mnaweza kuishia kuumizana.

Pia jambo kubwa ambalo wanawake wengi wenye umri mkubwa (miaka 50, 60 au 70) hawaijui kwamba ili kuwa na maisha mazuri ya kimapenzi (sexual) wanahitaji kujihusisha na tendo la ndoa mara kwa mara (mara moja kwa wiki) utaweza kupata lubrication zaidi kuliko kutojihusisha kabisa.

Hapo ndo utasikia ule msemo kwamba;

“Use it or lose it”

Tuesday, June 22, 2010

Kuongezeka Umri

Huwezi kugoma kutozeeka, ni muhimu sana kutarajia mabadiliko jifunze kukabiliana na hiyo hali au tarajia mabadiliko kwani mwanamke mwenye umri wa miaka 29 hawezi kuwa sana na mwanamke mwenye miaka 40 na mwanaume mwenye miaka 28 si sawa na mwanaume mwenye miaka 45.

Inawezekana wewe ni mwanaume na umeanza kupoteza kwenye kichwani na inawezekana umeanza kujazia uzito wa ziada kwenye tumbo na una kakitambi ka kiana.

Ulizoea kuruka kirahisi sasa ni mzito huwezi kuruka tena, hapo sijakuuliza masuala chumbani na huyo Mr. Happy wako ana behave vipi.

Inawezekana wewe ni mwanamke na umri ni kweli unaenda na huamini namna gravitational force inavyokuvuta kila kitu kushuka chini ya sakafu.

Unashangaa matiti yanashuka chini na kulala tofauti na zamani, uso nao unainama na kuweka wrinkles, unashangaa nywele zinakuwa ngumu na kuanza kupotea zenyewe bila taarifa, chini kunagoma kuwa wet hata baada ya kusisimuliwa kama ilivyokuwa kawaida yako kwani kwa maongezi tu kila kitu chini kulijibu.

MABADILIKO YA KAWAIDA KIMAPENZI KWA MWANAUME ANAPOONGEZEKA UMRI:

Kumbuka ulipokuwa teenager (siyo wote) ile kusoma gazeti ambalo ni romantic ulikuwa unasisimka (erection), ile kumpita mwanamke mrembo mwili ulikuwa unasisimka.

Mwanzo wa ndoa yako, ukiona mke wako kapanda kitandani tu ulikuwa unasisimka na kuwa tayari kwa Mr. Happy wako alikuwa tayari kashajinyosha na anakugusa ceilings.

Inawezekana kutokana na mwili wako kusisimka kimapenzi haraka kumejenga tabia fulani kwako na kwa mke wako na siku mambo yakiwa tofauti mnaanza kuhaha kudhani kuna tatizo limejitokeza kumbe ni kawaida kwani ni kuongezeka kwa umri.

Inawezekana hata namna ya kuandaana ilikuwa ni one sided kwa maana kwamba mwanaume ndiye alikuwa anasisimuliwa kwa muda mrefu zaidi na mwanamke kwa muda mfupi.

Sasa umri umeongezeka na usipoandaliwa vizuri unaweza kujikuta Mr. Happy anabaki soft muda wote bila kuleta mabadiliko yoyote kama kawaida yake.

Maana yake mwanaume anapoongezeka umri anahitaji direct penile stimulation kuliko zamani.

Ukweli ni kwamba mwanaume anapokuwa kijana hadi kuwa mzee ni mfano wa godoro jipya, ukilinunua huwa gumu na baada ya miaka kadhaa utaona kasheshe yake.

Pia mwanaume anapoongezeka umri anaweza kushangaa anamaliza sex bila kukojoa (ejaculate) kitu ambacho haikuwa kawaida yake, kwani older men kawaida hawahitaji kufika kileleni kama young men.

Hata hivyo hiyo ina faida kwa mwanamke kwani sasa mwanaume anaweza kufika mbali katika kumridhisha mke wake ndiyo maana umri unavyoongezeka mwanaume huwa mzuri zaidi kimapenzi.

Kama ni mwanamke Kumbuka kwamba si kushindwa kwako kama ukiona mume wako wa 40+ amemaliza nusu saa bila kufika kileleni, wala haina maana kwamba humvutii au hupendeza bali ni kuonesha kwamba mwili wake unazeeka.

Inawezekana ilikuwa kawaida yake akimaliza mara ya kwanza baada ya dakika 2 au 3 anaweza kurudi na kuanza upya kukupa mahaba wewe mke wake na sasa hawezi tena.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

Monday, June 21, 2010

Alisahau Kwamba Ameoa

Kaka Mbilinyi Swali langu ni kama ifuatavyo:

Baada ya kurudi honeymoon, mimi nilikuwa na siku mbili off na mume wangu yeye aliripoti kazini siku inayofuata.

Kwa kuwa mume wangu alienda kazini na nilikuwa na muda nilipanga kuwa na dinner ya uhakika kwa maana kwamba niandaa chakula na vikolombwezo kibao (candlelight dinner, mwenyewe nikavaa dress ya uhakika na mengine najua unafahamu...)

Mume wangu alitakiwa kuwepo nyumbani saa kumi na moja kamili, hata hivyo hakurudi nyumbani hadi saa nne usiku bila taarifa yoyote.

Wakati huohuo nilikuwa nimeshasubiri na kuchoka (nililala usingizi mezani namsubiri kwa ajili ya dinner), chakula kikapoa, candles zangu zikawa zimeishia, simu yake ilikuwa inaita tu bila majibu.

Nilipomuuliza alikuwa wapi, aliniambia eti alisahau kama alikuwa ameoa, na kwamba simu aliisahau kazini na alipotoka kazini alienda moja kwa moja nyumbani kwa wazazi wake, alikuwa anatazama Tv World Cup kwani nyumbani kwa wazazi wake huwa kunakuwa na watu wengine ambao huwa wanaangalia hizo mechi na hutokea hivyo kila kunapokuwa na World Cup au Ligi kuu Uingereza.

Anasema baba yake alimuuliza;

Hivi wewe si ulitakiwa kuwa nyumbani kwa ajili ya dinner kwa mkeo?”

ndipo akakumbuka kwamba yupo nyumba siyo yenyewe.

Je, inaweza kutokea mwanaume akasahau kwamba ameoa?

Je hii si ina maana kwamba ananiona mimi sina umuhimu katika maisha yake?

Dada J.

Dada J,

Pole sana na yaliyokupata,

Ni kweli una haki ya kujisikia vile unajisikia kutokana na kile kilichotokea.

Kama mume wako hana tatizo la kusahau (Adult Attention Deficit Hyperactivity Disorder - AADHD) basi kwao ni mtoto wa mwisho kuzaliwa (last born) kwa maana kwamba kwa wazazi wake yeye bado ni mtoto na jambo kubwa unapooana na mtoto wa mwisho kuzaliwa (special kid) uwe tayari kwa adventures.

Pia kama ni kweli ni mtoto wa mwisho kwa wazazi wake tegemea adventures zingine kwani hizo ndo zao na unatakiwa kuwa strong kama watoto wa kwanza kuzaliwa wanavyokuwa controlling ila kama na wewe ni mtoto wa mwisho kuzaliwa basi hapo mmekutana wote ni comedian.

Pamoja na jambo kubwa (blunder) aliyofanya bado kwake anaweza kuona ni kitu cha kawaida sana, ingawa kwako ni ngumu sana Kuamini kwamba mtu anaweza kuoa na akasahau kwamba ameoa.

Hujawahi sikia mwanamke analalamika kwamba mume wake hakustahili kuwa ameoa?

Ukweli ni kwamba kuna wanaume ni big kids, tall kids ambao mwanamke unatakiwa kuwachukulia na usiumize sana kichwa au kuweka matarajio makubwa sana.

Kama umewauliza wazazi wake na wakakubali kwamba ni kweli kijana wao (special kid wao) alikuwa nyumbani kwa wazazi wake akiangalia hiyo mechi ya World Cup, basi haina haja wewe kuwaza na kufika mbali sana kwani inawezekana ni kweli alisahau kwamba ameoa na baada ya kutoka kazini aliendelea kutumia uzoefu wake wa kila siku ambao aliuzoea katika maisha yake yaani kazini na kurudi nyumbani ambako ubongo wake bado unaamini ni kule kwa wazazi wake hadi alipokumbushwa kwamba aende kwa mke wake na baba yake.

Pia Kumbuka wanaume ni tofauti na wanawake kwa maana kwamba mwanaume hufanya jambo moja kwa wakati wake bila kuhusanisha na mambo mengine.

Anapokuwa kazini anakuwa kazini hana wazo lolote kuhusu dinner wala nyumbani, anapoangalia mechi za kombe la dunia ana-concentrate kuangalia hizo mechi bila kuwaza kitu chochote zaidi ya hicho.

One thing a time!

KWA UFUPI

Ndiyo inawezekana mwanaume anaweza kusahau kama ameoa kwa dakika fulani au muda fulani inatokana na mzunguko wa kazi zinazomkabili ile siku na kukomaa kiakili.

Si kweli kwamba anakuona huna umuhimu kwa sababu tu alisahau kwamba ameoa, Kumbuka huyu ni mwanaume ambaye ni mara yake ya kwanza kuishi na mwanamke, maisha yake yote alikuwa anaishi na wazazi wake hivyo itamchukua muda ili ajifahamu vizuri kwamba na yeye ana mji wake.

Hakikisha unampa respect mume wako huyo pamoja na vituko vyake kwani ili akuoneshe upendo na wewe unahitaji kumpa respect na kumpenda kwa upendo wa kweli.

Ndoa ni kazi