"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, June 6, 2010

Akachungulia kwenye Friji!

Baada ya ndoa kanisani na sherehe za uhakika za harusi (reception) maharusi walipelekwa moja kwa moja kwenye hotel moja huko Bagamoyo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ili wakapumzike na kuelendelea na honeymoon.

Walibahatika kupata chumba maalumu cha maharusi (bridal suite) na bila kupoteza muda mume akaamua atangulie kwenda kuoga kabla ya mke wake kwani huo ni usiku special kwao hivyo mume akaenda bathroom kuoga ili baadae ampishe bibie naye akaoge na waendelea na ratiba yao hao wawili wanaopendana.

Kumbuka huo ni usiku ambao walikuwa wanauota, wanaongojea, wanahamu nao kwani ni siku ya kwanza kujuana kama mke na mume na kuanza safari mpya ya maisha ya ndoa.

Wakati mume akiendelea kuoga mke katika angalia angalia huku na huko akafungua friji, du akaona chupa iliyopambwa kwa maandishi yanayosema:

Special for you our beloved new weds in your memorable honeymoon; enjoy

Kwa mwanamke ilikuwa mara ya kwanza kuona chupa ya aina ile hasa kutokana na malezi na mazingira hivyo akaona ni kitu halali kwake na who care usiulize ulize wewe kula na kunywa.

Akamiminina kwenye glass na kuonja akajisikia kuongeza zaidi ndipo akashika chupa nzima nzima na kuigigida yote ikabaki empty.

Kumbe ilikuwa ni wine na dakika ileile ikaanza kumpiga kiuhakika yule binti ambaye alikuwa hajawahi kuingiza kilevi cha aina yoyote kwenye damu yake tangu azaliwe. Baada ya muda akaanza kuona chumba kinazunguka.

Ile mume kutoka bathroom akasikia harufu kama ya “after shave lotion’ halafu bibi harusi (ambaye sasa ni mke) anachonga si kawaida, amelewa hoi, anaongea mbovu mbovu, na anaikanyaga keki kwa miguu na anafanya vituko vya ajabu na chumbani ni vurugu.

Bwana harusi (ambaye sasa ni mume) alijitahidi kumtuliza lakini wapi, amelegea mwili mzima utadhani ni hydra.

Ikabidi mwanaume usiku mzima anahangaika kumtuliza na mke alilala usiku mzima hajitambui huku mume akishangaa namna siku yake na ndoto yake ya kufurahia mke kwa mara ya kwanza ikatoa mabawa.

Kwa kuwa hotel ilikuwa kwa usiku mmoja tu; hata asubuhi mwanamke alikuwa bado amelewa hivyo mwanaume akatafuta usafiri wa kurudi nyumbani na mwanamke aliendelea kuwa amelewa kwa siku mbili mfululizo na mwanaume hakuambulia kitu kuhusiana na suala la kujuana.

Hawa maharusi sasa ndoa yao ina miaka 10 ukiwauliza honeymoon ni kitu gani watakwambia..............................

2 comments:

Anonymous said...

Ahahahaha macho ni sumu jamani tamaaa hii ilimponza fisi

Lazarus Mbilinyi said...

Tatizo ni uelewa wa mambo na kuwa smart katika mazingira mapya.

Kazi kwelikweli