"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, June 10, 2010

Akaenda kulala sebuleni!

SWALI:

Kaka Mbilinyi pole na kazi;

Kwanza najisikia vibaya kuelezea hili, kabla ya kuoana na mke wangu huyu niliyenaye sasa niliwahi kuwa na mwanamke ambaye tulifanya sex zaidi ya mara 5.

Baada ya kuoa niliamini kwamba nimeshasahau kila kitu kuhusu huyo mwanamke.

Hapa juzi wakati tunaendelea na tendo la ndoa na mke wangu na wakati nafika kileleni bila kujitambua nilitaja jina la yule mwanamke wa zamani badala ya jina la mke wangu wa sasa.

Unajua nini kilitokea?

Kila kitu kilisimama na mke wangu alikasirika, akaondoka chumbani na kwenda kulala sebuleni na hadi leo hataki kuongea na mimi,

Je, nimeshaharibu ndoa yangu?

JIBU

Kaka Pole sana kwa yaliyokukuta;

Ni kweli wakati mwingine wanaume huonekana ni wajinga na wapuuzi (stupid) na wewe umetuhakikishia kweli wakati mwingine wanaume ni stupid. Yaani ulizama kwenye mahaba na mke wako halafu unajisahau upo na nani?

You will pay the price my brother!

Hata kabla hujamuomba msamaha kwa mke wako (unatakiwa kuomba msamaha haraka sana), unatakiwa kujiuliza na kujihoji kwa nini hilo jina lilikutoka kinywani.

Je, ni kweli ulijisahau upo na nani?

Je, huyo mwanamke wako wa zamani bado ni muhimu katika maisha yako na sasa?

Je, ni kweli ilitokea kwa bahati mbaya na huna feelings kabisa na huyo mwanamke wako wa zamani?

Unatakiwa kuwa makini sana na maneno yako kwani maneno ni sumu mbaya sana katika mahusiano na huweza kuharibu ndoa na kuwa vipande vipande.

Kwa mwanamke, ni ngumu sana kutoa mwili wake kwa ajili ya sex kuliko mwanaume hii ni kutokana na walivyoumbwa na namna wanajiamini na miili yako sasa kitendo cha wewe kutaja jina la mwanamke mwingine wakati muhimu kama huo kwa kweli hilo kosa inabidi utubu kwa kujieleza vizuri hadi aridhike.

Hivyo basi nenda ukaombe msamaha haraka, mwambie ni kweli wewe ni mwanaume mjinga na mwambie unampenda sana, na elezea vizuri kwa nini hilo jina la huyo mwanamke lilikutoka kinywani mwako bila kujikanyaga na usidanganye eleza ukweli kwani wanawake wana talent ya kufahamu kama anachoambiwa anadanganywa au la. Jitahidi kutengeneza mambo haraka iwezekanavyo na ukiwa mkweli wanawake ni rahisi kusamahe.

Pia kama unaendelea kuwasiliana na yule mwanamke inabidi kuanzia sasa uachane naye na usiwasiliane naye kwa njia yoyote.

Kama kweli unataka kuponya ndoa yako ni muhimu sana kuachana naye kuwasiliana kwa simu, email, facebook, rafiki zako nk (electronically &traditionally).

Achana naye kabisa.

Hata ukienda kumnunulia zawadi ya thamani haitasaidia, kitakachokusaidia ni wewe kuwa mkweli, kuthibitisha kwamba wewe ni mume wa mke mmoja ambaye ni yeye, upendo wako kwake, nia njema kwake na pia muda, kwani hatakuamini hadi yeye mwenyewe ahakikishe ni kweli maneno yako na matendo yako vinaendana.

Kuanzia sasa unatakiwa uwe unamuwaza mke wako tu usiku na mchana hata kujizoesha kulitaja jina lake mara kwa mara na likija wazo lolote kuhusu yule mwanamke Jitahidi kufuta kwa kuwaza kitu chochote kuhusu mke wako.

Pia mkiwa chumbani na mke wako ni vizuri kuwa na aina ya mahaba ambayo ni aina ya pekee (modes operand/rhythm) kati yako na mke wako tu.

Jambo lingine, kaka unatakiwa kuwa tayari kuchunguzwa kila mwenendo wa maisha yako kuanzia simu yako ya mkononi, emails, mifuko ya suruali au kupigiwa simu ofisini au hata mke kuja kukutembelea ghafla ofisini kwako ili ajue kama kweli upo ofisini au gelesha na lengo lake inaweza kuwa anataka kujua kama kweli wewe ni msafi au bado unaendelea kuchafuka na yule mwenye lile jina umelitaja ile siku chumbani wakati unaogelea kwenye kisima chake cha mahaba.

Ana haki ya kufanya hivyo kwani analinda territory yake.

Kama ukiwa mkweli na ukadumu katika kuwa mwaminifu kwake basi ndoa yako haitaharibika ila suala ni muda.

Kazi kwako!

1 comment:

Anonymous said...

Hapa ni utata mtupu nimecheka hadi kulia machozi.

yaani hadi leo nacheka tuu kati kati ya utamu unasikia linatajwa jina mtu mwingine hivi kweli hata kama ulikuwa unataka kup...............z itatoka kweli???? hii ni kwa wote haijalishi wanaume au wanawake.
Kazi kwelikweli.