"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, June 21, 2010

Alisahau Kwamba Ameoa

Kaka Mbilinyi Swali langu ni kama ifuatavyo:

Baada ya kurudi honeymoon, mimi nilikuwa na siku mbili off na mume wangu yeye aliripoti kazini siku inayofuata.

Kwa kuwa mume wangu alienda kazini na nilikuwa na muda nilipanga kuwa na dinner ya uhakika kwa maana kwamba niandaa chakula na vikolombwezo kibao (candlelight dinner, mwenyewe nikavaa dress ya uhakika na mengine najua unafahamu...)

Mume wangu alitakiwa kuwepo nyumbani saa kumi na moja kamili, hata hivyo hakurudi nyumbani hadi saa nne usiku bila taarifa yoyote.

Wakati huohuo nilikuwa nimeshasubiri na kuchoka (nililala usingizi mezani namsubiri kwa ajili ya dinner), chakula kikapoa, candles zangu zikawa zimeishia, simu yake ilikuwa inaita tu bila majibu.

Nilipomuuliza alikuwa wapi, aliniambia eti alisahau kama alikuwa ameoa, na kwamba simu aliisahau kazini na alipotoka kazini alienda moja kwa moja nyumbani kwa wazazi wake, alikuwa anatazama Tv World Cup kwani nyumbani kwa wazazi wake huwa kunakuwa na watu wengine ambao huwa wanaangalia hizo mechi na hutokea hivyo kila kunapokuwa na World Cup au Ligi kuu Uingereza.

Anasema baba yake alimuuliza;

Hivi wewe si ulitakiwa kuwa nyumbani kwa ajili ya dinner kwa mkeo?”

ndipo akakumbuka kwamba yupo nyumba siyo yenyewe.

Je, inaweza kutokea mwanaume akasahau kwamba ameoa?

Je hii si ina maana kwamba ananiona mimi sina umuhimu katika maisha yake?

Dada J.

Dada J,

Pole sana na yaliyokupata,

Ni kweli una haki ya kujisikia vile unajisikia kutokana na kile kilichotokea.

Kama mume wako hana tatizo la kusahau (Adult Attention Deficit Hyperactivity Disorder - AADHD) basi kwao ni mtoto wa mwisho kuzaliwa (last born) kwa maana kwamba kwa wazazi wake yeye bado ni mtoto na jambo kubwa unapooana na mtoto wa mwisho kuzaliwa (special kid) uwe tayari kwa adventures.

Pia kama ni kweli ni mtoto wa mwisho kwa wazazi wake tegemea adventures zingine kwani hizo ndo zao na unatakiwa kuwa strong kama watoto wa kwanza kuzaliwa wanavyokuwa controlling ila kama na wewe ni mtoto wa mwisho kuzaliwa basi hapo mmekutana wote ni comedian.

Pamoja na jambo kubwa (blunder) aliyofanya bado kwake anaweza kuona ni kitu cha kawaida sana, ingawa kwako ni ngumu sana Kuamini kwamba mtu anaweza kuoa na akasahau kwamba ameoa.

Hujawahi sikia mwanamke analalamika kwamba mume wake hakustahili kuwa ameoa?

Ukweli ni kwamba kuna wanaume ni big kids, tall kids ambao mwanamke unatakiwa kuwachukulia na usiumize sana kichwa au kuweka matarajio makubwa sana.

Kama umewauliza wazazi wake na wakakubali kwamba ni kweli kijana wao (special kid wao) alikuwa nyumbani kwa wazazi wake akiangalia hiyo mechi ya World Cup, basi haina haja wewe kuwaza na kufika mbali sana kwani inawezekana ni kweli alisahau kwamba ameoa na baada ya kutoka kazini aliendelea kutumia uzoefu wake wa kila siku ambao aliuzoea katika maisha yake yaani kazini na kurudi nyumbani ambako ubongo wake bado unaamini ni kule kwa wazazi wake hadi alipokumbushwa kwamba aende kwa mke wake na baba yake.

Pia Kumbuka wanaume ni tofauti na wanawake kwa maana kwamba mwanaume hufanya jambo moja kwa wakati wake bila kuhusanisha na mambo mengine.

Anapokuwa kazini anakuwa kazini hana wazo lolote kuhusu dinner wala nyumbani, anapoangalia mechi za kombe la dunia ana-concentrate kuangalia hizo mechi bila kuwaza kitu chochote zaidi ya hicho.

One thing a time!

KWA UFUPI

Ndiyo inawezekana mwanaume anaweza kusahau kama ameoa kwa dakika fulani au muda fulani inatokana na mzunguko wa kazi zinazomkabili ile siku na kukomaa kiakili.

Si kweli kwamba anakuona huna umuhimu kwa sababu tu alisahau kwamba ameoa, Kumbuka huyu ni mwanaume ambaye ni mara yake ya kwanza kuishi na mwanamke, maisha yake yote alikuwa anaishi na wazazi wake hivyo itamchukua muda ili ajifahamu vizuri kwamba na yeye ana mji wake.

Hakikisha unampa respect mume wako huyo pamoja na vituko vyake kwani ili akuoneshe upendo na wewe unahitaji kumpa respect na kumpenda kwa upendo wa kweli.

Ndoa ni kazi

No comments: