"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 8, 2010

Anachagua mno!

SWALI
Kaka Mbilinyi naomba msaada,

Mke wangu ni picky (anachagua sana) linapokuja suala la sex, atataka mbishane wapi mfanyie, lini iwe na muda gani na mengine mengi tu ambayo yananifanya nichanganyikiwe.

Niliamini suala la sex kwenye ndoa ni kitu simple, sasa naona mambo yanazidi kuwa complicated.

Je hili ni tatizo langu peke yangu au kuna mwanaume mwingine anayepata shida kuvutana na mke linapokuja suala la sex kama mimi?

Msaada jamani!

MAJIBU:

Kaka pole sana kwa shida unayokutana nayo ni kweli wanawake ni picky, hilo lazima uiweke ndani ya ubongo wako kwamba wanawake ni tofauti na wanaume na kwamba hata huyo mwanamke mmoja kila siku anakuwa tofauti kuhusiana na wapi, lini na namna gani sex ifanyike.

Na kazi yako wewe mume ni kufahamu majibu ya hayo maswali na hatimaye kumfanya mke wako akufurahie hasa kutokana na ulivyo smart kupata majibu ya maswali yake.

Hiyo ni challenge yako mwenyewe na ukifanikiwa basi unaweza kumfahamu vizuri mke wako na unaweza kuvumbua mystery ya yeye kuwa picky.

Hata hivyo Usifikirie ni kazi rahisi kwani wanawake hubadilika all the time.

Inaonesha mke wako ni moja ya complex creature kuliko wewe. Inaonesha leo anaweza akalipenda busu lako na kesho akasema no, leo anaweza kupenda namna unavyomgusa kwenye mguu wake na kesho akasema no, leo anaweza kupenda hiki na kesho akasema no; hata hivyo kazi kubwa kuziangalia signs na kuzijua kwa kumuuliza ili kupata ufahamu wa majibu ya hayo maswali yake.

Usijidanganye kwa Kuamini kwamba kile ambacho kilikuwa kinamsisimua miaka 5 iliyopita au sehemu alizokuwa anazipenda miaka 5 iliyopita au namna ulikuwa unafanya miaka 5 iliyopita basi na leo itafanya kazi au itamfanya ajisikie kusisimka kimapenzi, Si kweli.

Wanawake wana hormones nyingi kuliko sisi wanaume na matokeo yake wao hubadilika badilika emotionally kila wakati.

Pia Kumbuka kazi yako si kusoma nilichokiandika na kufanyia kazi neno kwa neno bali soma nilichoandika na tafuta namna mke wako anapenda, hakuna mtu anaweza kukufanyia isipokuwa wewe mwenyewe, ni mke wako na suala ni muda tu ukiwa makini utamfahamu vizuri na ukishamfahamu ni mafanikio makubwa sana.

Kila mwanaume hukutana na matatizo yake kwa mke wake hata hivyo mwanaume smart hugundua haraka tofauti zilizopo na kuzifanyia kazi na kuendelea ku-enjoy maisha kama kawaida na kufurahia ndoa.

JAMBO LA MSINGI

Sehemu ya kujifunza namna ya kumpenda mke au mume ni pamoja na kumfahamu, ulipokuwa unaoa au kuolewa naye ulichagua kumpenda mke wako au mume wako maana yake ulimweka namba moja kwa kila kitu iwe katika kuwaza au kutenda, ulichagua kumpa heshima kwa ajili ya mawazo yake au hisia zake na uliahidiana naye kwamba mtasaidiana kuhakikisha ndoa yenu inaridhisha.

Siku mnapeana viapo hukuwa unaona matatizo aliyonayo kwa sababu hukuwa unaona fine prints za ndoa yako, lakini yalikuwepo.

Hivyo Jitahidi kumfahamu ili ujue namna ya kupenda.

No comments: