"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, June 12, 2010

Bado Yupo Kichwani!

Ujana ni kama moshi pia ni kazi na mtego!

Kwa nini James na Jane bado wapo akilini mwako?

Binadamu yeyote aliyezaliwa na mwanamke akifikia umri wa ujana (teenager) anakuwa yupo katika kipindi ambacho huitwa ni hatari (very critical years) kwa sababu kamili.

Hii ni miaka ambayo kila kosa unalofanya huweza kuathiri maisha yako yote.

Kosa moja kwenye tairi unaweza kupoteza maisha kwa ajali ya kutosha ya gari.

Kitendo cha kujaribu unga kidogo unaweza kujikuta unaji-overdose na kuharibu maisha forever.

Sex siku ya kwanza na mara moja unaishia kupata mimba na kuharibu malengo ya maisha yako.

Pia inawezekana umeoana na huyo mume wako au mke wako kwa sababu mlipeana mimba wakati wa ujana na baba yake alikutishia kwa bunduki na ukaamua kuyamaliza kwa kuoana hata hivyo baada ya kuoana kila mtu amekuwa anapepesa macho nje kwa kasi ya ajabu na ndoa haina ladha tena.

Unapoanza ujana ni miaka ambayo hormones hukimbia kwa speed ya ajabu hadi watu kufanya vitu vya ajabu na maamuzi ambayo hujutia baadae.

Inawezekana kuna swali ambalo hujajiuliza ambalo ni Je, kama nipo happy na ndoa yangu sasa, mambo niliyoanya huko nyuma yanaweza kuniathiri katika ndoa yangu.

Inawezekana una miaka 2 tangu umeoana na huyo partner wako na ghafla inatokea siku moja mkiwa chumbani (lovemaking) unajikuta sura ya mpenzi wako wa zamani inajitokeza au unatamka jina la yule mwanamke au mwanaume.

Je, hii ina maana humpendi mke wako au mume wako?

Si kweli bali ina maana kwamba yale mambo ulifanya huko nyuma yapo imprinted kwenye akili (ubongo).

Hii ina maana kwamba unapofanya sex unajihusisha zaidi ya ukaribu wa kimapenzi (intimacy) na kuunganishwa na yule unakuwa naye (connections), ni njia ya tofauti na ndani sana ya kumjua mtu na sex si mwili tu bali akili na namna ulivyo.

Uwe unafahamu au hufahamu, maumivu na vidonda vya mahusiano yaliyopita (maneno, sex, mwili nk) tayari umeshaathirika navyo na vinamuathiri yule umeoana naye. Kwa kuwa ubongo wako ni kitu kinachotunza kumbukumbu kuliko computer.

Je, unawezaje kuondoa haya mawazo?

Kwanza inabidi uamini kwamba kile kilitokea huko nyuma ni kitu cha huko nyumba hata kama kinaathiri wakati huu. Pia unao uamuzi wa kuchagua kuendelea kuathirika na hiyo hali au kuikataa. Na uchaguzi ni sasa, na unaweza kubadilisha hizo taswira za zamani kwa kuweka taswira mpya za yule unaishi naye sasa.

“What you think, you become”

Kwa maelezo zaidi soma hapa

No comments: