"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, June 20, 2010

Funga Mlango!

Wapo wanandoa ambao (hasa wanaume) huendelea na tendo la ndoa bila kujali kama mlango upo locked au la.

Pia wapo ambao mlango huwa wazi kabisa eti watoto huwa wamelala usingizi.

Hata hivyo mtoto ni mtoto na anaweza kuamka na kwenda chumbani kwa wazazi muda wowote.

Hata hivyo mwanamke ndiye huathirika zaidi ya suala la mlango kuwa wazi na wakati mwingine huweza kuwa focused kwenye mlango badala ya love making.

NIKUPE KISA HIKI:

James na Jane ni wanandoa wanene sana na vipande vya watu kila mmoja ana pack mwilini zaidi ya kilo 200, kama ulidhani watu wanene likija suala la sex wapo nyuma unajidanganya sana.

Katika kutafuta variety (mambo mapya na tofauti ili kuimarisha joto chumbani kwao) wakaamua kujaribu love making position mpya.

Si unajua mambo ya adventures, to have fun mke na mume!

Haieleweki ilikuwa ni style ipi, hata hivyo inaonesha ilikuwa tricky kidogo kwani katikati ya hizo hekaheka au harakati wote waliishia kudondoka chini kutoka kitandani kitu ambacho kilisababisha kishindo na nyumba kutikisika mithili ya terrorist attack.

Na hii ilitokea wakati walisahau ku-lock mlango so watoto wao (teenagers) walikimbia mbio chumbani wa wazazi kuangalia na kushuhudia nini kimetokea, na kuwakuta baba na mama katika utukufu wao tangu wanazaliwa kila mmoja akijifunika kwa viganja sehemu za siri wasizione.

Ndiyo; hata kama una watoto wakubwa na kama wanandoa mna haki ya kufanya experiment za vitu vipya hata hivyo kukumbuka kufunga mlango (lock) ni jambo la busara zaidi.

5 comments:

Anonymous said...

Pia kuna wakati uki-lock mlango unakaribisha wagonga mlango, hivyo jambo la msingi kama una watoto ni vizuri kuwafundisha kwamba wakiona mlango upo locked haina haja kuendelea kuomba kufunguliwa na badala yake waendelea kufanya vitu vingine, ni baba na mama wanajadili masuala ya familia.

Anonymous said...

Inanikumbusha mbali sana,
Kuna mtoto mmoja alipoingia chumbani bila hodi kwa kuwa haukufungwa (locked) na yeye akaomba kama anaweza akafanya mieleka na wazazi wake kama wanavyofanya!

Anonymous said...

Naamini ni wazo zuri kwa wanandoa kuhakikisha mlango unakuwa na uwezo wa kuwa locked hasa watoto wakifika umri fulani ambapo wanaweza kuingia chumbani bila taarifa.

Anonymous said...

Je, watu siku hizi hawawafundishi watoto kugonga kwanza kabla ya kuingia chumbani kwa wazazi wao haijalishi mlango unaweza kuwa locked au hapana. Ni vizuri kuwafundisha watoto tabia njema na kuweka mipaka tangu mapema.

Anonymous said...

kufunga mlango ni muhimu mimi mwenyewe niliwahi kuingia chumbani kwa mama yangu mdogo nikawakuta,nilistuka,nikaogopa kwa sababu nilikuwa mdogo,lakini huwezi amini inanigharimu hadi leo nashindwa kusahau,fikiria tangu nikiwa na miaka 7,hadi leo 27,picha iko palepale,tuwe makini tunawaumiza watoto kwa kuwalazimisha kuona vitu ambavyo hawakutarajia kuviona.