"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 16, 2010

Fungwa kamba...

Kila mmoja amesikia tetesi au fununu kwamba wanawake hudanganya kwamba wamefika kileleni (faking orgasm).

Ni kweli hili jambo lipo; wanawake wengi wameshawahi kuwafunga kamba wanaume zao zaidi ya mara moja na wengine ni kamchezo kao ka mara kwa mara, hata wewe unayesoma hapa inawezekana usiku ulimdanganya kwamba umefika kileleni kumbe usanii mtupu.

Swali la kujiuliza hivi kwa nini wanachukua uamuzi wa kudanganya kwamba wamefika kileleni wakati si kweli?

Lazima kutakuwa na sababu za msingi kwani wanaume ni viumbe wanaojua kupenda kuliko wanaume na kama kuna sababu za msingi hii ina maana hawastahili kulaumiwa.

Pia tumesikia kwamba mwanaume ukiwa na wallet nzito mwanamke hufika kileleni haraka zaidi tena kwa kelele utadhani ni vuvuzelas za World cup 2010 huko bondeni kwa mzee Madiba.

Katika dodosa dodosa akina dada wengi na akina mama wengi sababu kubwa zinazopelekea wawadanganye wanaume zao kwamba muziki umejibu kwanza ni kitendo cha kutopenda waume zao wajisikie kuwa discouraged kwani wakati mwingine wao wanawake huwa wanakuwa wamechoka na wanapenda love making sessions iishe na njia sahihi ni kuonesha kwamba wamefika kileleni.

Kama wewe ni mwanaume upo kwenye ndoa fikiria umejitahidi kufanya kila unaloweza kumfanya mke wako ajisikia kupenda sex (umemsaidia kazi, na umefanya kila unaloweza ili ajisikia unampenda) ile mnaenda kitandani mke wako anakwambia:

Mimi nimejichokea hivyo fanya tu, ukimaliza niambie

Utajisikiaje?

Kuna tofauti gani kati ya ku-romance jiwe na mwanamke ambaye anakukabidhi sex organ na yeye analala usingizi?

Si afadhari akufunge kamba kwamba yupo na wewe na amefika kileleni haraka kumbe ni fake?

Naamini umepata jibu!

Pia wapo wanawake ambao wanakiri kwamba waume zao huwa hawaridhiki kimapenzi hadi mke afike kileleni, hivyo faking ni njia sahihi ya kumfanya mume aridhike na mwanamke asichoke.

Sababu nyingine ni kwamba mwanamke anapomuhitaji mume wake kwa sex si mara zote anahitaji kufika kileleni, wakati mwingine mke huhitaji ukaribu wa kimapenzi (intimacy), hata hivyo wanawake wengi huamini kwamba kuwa na mtazamo kama huo inaweza kumfanya mwanaume asijisikie vizuri na njia sahihi ya kumfanya mwanaume wa aina hii afurahi ni kumdanganya kwamba amefika kileleni.

Pia wapo wanawake ambao si kawaida yao kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa inawezekana ni skills kidogo kutoka kwa waume zao au namna walivyo.

Wanawake hawa hupenda sana waume zao wajisikia wanaweza na wanawaridhisha na hakuna njia nyingine zaidi ya faking.

Kama mwanaume atakuwa na focus kubwa kwa ajili ya kumfanya mwanamke afike kileleni badala ya kumpa raha ya mapenzi, basi uwezekano wa mwanamke kudanganya huongezeka.

Mwanamke hujiona amempa mume disappointment kubwa mno kama hajafika kileleni kwani anaona juhudi ya mume wake, hivyo faking is the true name of the game.

Kudanganya kwamba amefika kileleni huweza kuwa sanaa nzuri sana kwa mwanamke smart ambaye anafahamu namna ya kucheza iana hii ya maigizo.

Atambana mwanaume wa watu (kwida kabisa), atatoa miguno wa kimahaba, atapumua kwa ndani, atabadilisha sura na uso, atajivuruga kwenye pillow kisanii na kijiografia hadi mwanaume aingie mjini.

Wanawake wataendelea kudanganya tu kwamba wanafika kileleni na wanaume hawawezi kufanya chochote zaidi kwa kuendelea kufurahia tu.

Kama ukigundua kwamba mke wako anakudanganya kwamba amefika kileleni jambo la msingi si kulaumiana bali kuzungumza au kujadiliana na kufahamu sababu zinazofanya mfungane kamba kiasi hicho na kama inawezekana nini kifanyike ili kuwa na kitu halisi.

Mapenzi ni sanaa na kwenye sanaa kuna actors.

4 comments:

Anonymous said...

Mara nyingi mimi nina kuwa sina mood na sex na mume wangu anakuwa hana mood ya kunipa romance so jibu ni kudanganya kwamba nimefika kileleni, no questions.

Anonymous said...

Wanawake ni kweli wanapenda sex na pia wanapenda ku-fake kufika kileleni, wanaume tupende tusipende!

Anonymous said...

Ni kweli asilimia 75 ya wanawake hudanganya kwamba wamefika kileleni na hii inawezekana unachangiwa sana na skills za mwanaume, kuna wanaume wanaamini mwanamke ili afike kileleni ni in and out kwa kwenda mbele.
Pia Kumbuka ni asilimia 25 tu ya wanawake huweza kufika kileleni kwa njia ya uke (in and out)
Kufanganya kutakuwepo tu!

Anonymous said...

Nilikubaliana na mke wangu asiwe ananidanganya kwamba amefika kileleni hata hivyo wakati wa tendo la ndoa aliniambia amefika kileleni hata hivyo baada ya kumaliza akasema hakufika, so wanawake kwenye hili eneo la kudanganya wengine wameshazoea.
BMM