"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 15, 2010

Hakuna Jipya!

SWALI

Mimi ni dada mwenye miaka 30 sasa naishi Sinza na mume wangu hata mwezi hatujamaliza tangu tufunge ndoa.

Tulipokuwa honeymoon (Zanzibar) wiki mbili zilizopita, tulitegemea sex ingekuwa kitu cha kutupa raha (excitement) ya juu sana, hata hivyo tumejikuta ni kitu cha kawaida tu tofauti na matarajio yetu.

Je, ni kweli kwamba kama kabla ya kuoana mlipeana mwili mkienda honeymoon kunakuwa hakuna jipya linapokuja suala la sex?

MAJIBU

Suala si kweli au kweli jambo la msingi ni kwamba suala la kupeana miili kabla ya kuoana ni dhambi inayoitwa Uasherati.

Hivyo ni kweli kunakuwa hakuna jipya kabisa kwani kuna sababu nyingi tu hebu tujadili kidogo.

Hivi ulifikiri ni tofauti kiasi gani sex ingekuwa kwa kuwa mpo Zanzibar (honeymoon) na mkiwa nyumbani Sinza kabla hamjaoana?

Ukweli ni kwamba ninyi wawili hamkubadilika kitu chochote, kitu ambacho mlibadilika ni kupewa kipande cha karatasi kanisani kinachoonesha ninyi ni mume na mke na kwamba sasa mna jina moja ya ukoo.

Kitendo cha kupeana miili kabla ya kuoana kimeondoa maana halisi ya ukaribu wa kimapenzi ambao ungefanya honeymoon kuwa na raha, kumbukumbu, vicheko, msisimko, moto, ukaribu, utamu, mshangao na uzoefu ambao ungefungua siri ya kuaminiana na kuwapa kitu kipya katika safari mpya ya ndoa yenu.

Kama ulitegemea honeymoon kuwa na jipya wakati mlishapasha moto wa mapenzi mashuka yenu kabla ya kuoana ni sawa na mbwa anayeubwekea mti.

Kitu ambacho wengi hawafahamu hasa kizazi cha leo ambacho hujiona kinajua mambo (lakini kimejaa ujinga mtupu) ambacho kijana (kike na kiume) akiwa bikira hadi siku ya harusi huchekwa hakijui kwamba shetani ni smart kuliko wanavyodhania.

Swali la kujiuliza kwa nini sex kabla ya ndoa inaonekana kama njia sahihi na so exciting na baada ya kuona hao hao waliokuwa wanadanganyana kupeana miili wanajikuta hawapendi sex tena wakati ndiyo haki yao?

Usijidanganye, ukitaka kuwa na exciting honeymoon kama ni kijana wa kike bana malinda yako na kama ni kijana wa kiume kaza mkanda wa suruali yako.

Fikiria wewe ni binti na umeamua kumpa mwili huyo mwanaume ukiamini eti kwa kufanya hivyo basi ataamini unampenda, unaamua kumvutia nguo zako moja baada ya nyingine, kwa ujasiri unaamua kumvulia hadi chupi yako, ukiwa na akili timamu na huku unafahamu kwamba ni kitu kisichoruhusiwa na nafsi yako unaamua kumpa mwili wako; anaanza kuchezea matiti yako, chuchu zako, masikio, tumbo, kifua, kiuno hata uchi wako.

Mnaamua kupeana busu kama ulivyofanya, huyo mwanaume anauona mgongo wako ulivyo na mabaka meusi, anaona matiti yako yalivyolala, anaona mapaja yako yalivyo meusi, anaona huko chini south pole kulivyo na msitu au kichaka, anaona makalio yako yalivyo, anasikia sauti unayetoa wakati wa mahaba, anauona uso wako unavyokuwa na ndita wakati unafika kileleni, ili kumridhisha eti akupende zaidi unaamua kumuonesha style na milalo yote unayoijua. Siku ya kwanza, ya pili, ya tatu hadi mwaka unapita.

Mnaamua kuona na kwenda honeymoon huku mkidanganya eti muwe na honeymoon ambayo itakuwa na exciting sex experience.

Utapataje excitement wakati mlishafika mbali kiasi hicho?

Anajua ladha yako, sauti yako, uchi wako nk na hakuna jipya hapo!

Kwa nini uite honeymoon badala ya vacation?

Anyway, maisha yenu ya kimapenzi hayatakiwi kuwa boring, hivyo kaeni pamoja na kuzungumza na kuona ni namna gani mnaweza kuimarisha au kuipa ndoa excitement mpya kimapenzi.

Maelezo zaidi soma hapa

No comments: