"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, June 14, 2010

Hana Hamu tena!


Kaka Mbilinyi kwanza pole sana kwa kazi ya kutuelimisha, nami nina swali linalonitatiza.
Mwaka jana mume wangu alipoteza kazi.
Amefanya kazi katika hiyo kampuni kwa muda wa miaka 12 na alikuwa anaipenda kazi yake vizuri sana hata hivyo tangu aachishwe kazi mambo hapa nyumbani hayaendi sawa.
Kuna wakati anakaa tu Mahali kwenye giza bila matumaini.
Pia ni kama vile kuachishwa kwake kazi kumechukua hamu yake ya tendo la ndoa.
Mimi nina kazi yangu na sioni kwa nini amekuwa hivyo kwani kama ni mahitaji ya familia yanatimizwa na kazi ninayofanya.
Je, nitawezaje kuishi naye kama amekuwa hivi?
Mama Anna
Mama Anna,
Kwanza pole sana na tatizo lililopo jambo la msingi Kumbuka kwamba “No situation is permanent
Pia unatakiwa kufahamu kwamba wanaume na wanawake ni tofauti sana.
Wanaume huweza kujitambua na kuwatambua wengine kutokana na kazi wanazofanya. Wanawake wanaweza kufanya kazi nje ya nyumbani (kama vile kuwa Nurse, Daktari, Mwalimu nk) hata hivyo huwa hawajitambulishi kutokana na kazi zao kama wanaume wanavyofanya.
Kazi kwa mwanaume ndiyo yeye (identity).
Hii ina maana mume wako alipoachishwa kazi alipoteza identity yake, ndani ya moyo wake kuna kitu kinamwambia
Wewe si mwanaume tena, huwezi hata kuwa na kipato kwa ajili ya kutunza familia”.
Pia kitendo cha wewe kuwa na kazi ambayo inafanya kila kitu kiwe sawa hapo nyumbani kinaweza kuchangia kwa yeye kujisikia ovyo zaidi kama hujaonesha ushirikiano hasa respect hujiona hana thamani tena na humuhitaji tena na hujiona ni failure na loser na matokeo yake anaenda kujificha kwenye giza.
Na anapokuwa kwenye hilo cave lake lenye giza ndiko hupoteza uwezo (physically, emotionally na sexually) na matokeo yake ni Mr. Happy kushindwa kabisa kusimama (ED- erectile dysfunction).
Mume wako anachohitaji ni wewe kumuhitaji yeye na hii ndiyo challenge kubwa kwako. Huu ni wakati ambao unatakiwa kuwa creative.
Maneno unayotumia kuongea na mume wako ni muhimu sana kwake katika wakati huu.
Atafurahi sana kusikia unamwambia
mpenzi, wewe ni Nambari one kwangu, na tutavuka hili tatizo lako la kukosa kazi pamoja, mimi na wewe, nina imani kubwa sana na wewe”.
Mume wako anahitaji kuhakikishiwa kwamba unampenda kama alivyo na unampa heshima kama mume hata kama hachangii chochote.
Ajione bado unamuona yeye ni Hero!
Kama ataendelea kuwa depressed kwa muda mrefu zaidi bila mabadiliko basi inawezekana hilo ni tatizo ambalo ni clinical zaidi na anahitaji msaada wa physician ili aweze kumpa msaada zaidi.
Kumbuka hata kama mume wako hataonesha ushirikiana kila wakati, unachotakiwa kufanya ni kuwa karibu naye kimwili na kihisia. Kilichotokea ni kwamba amepoteza sehemu kubwa sana ya yeye mwenyewe.
Ni wakati ambao unatakiwa kuwa na focus kwa mume wako tu na achana na mambo mengine ambayo hayana umuhimu mkubwa katika maisha yenu.
Naamini haya maelezo yametakupa tips za kukabiliana na hili tatizo.
Kwa maelezo zaidi kuhusu mwanaume na kazi soma hapa

No comments: