"Marriage is our last, best chance to grow up."

Sunday, June 27, 2010

Hata kwa Simu

Kama unaishi nchi zilizoendelea (mfano USA, Canada au Uholanzi), ukinunua gazeti (local news paper) kwenye hizi nchi unaweza kukutana na matangazo ambayo yana namba ambazo mwanaume hulipa zaidi ya dola 3 ili kumsikiliza mwanamke (kwa dakika moja) ambaye anaongea kimapenzi (wenyewe wanaita phone sex).

Bila shaka hii ni kuonesha namna dunia imelemewa na kwamba inaishia ukingoni, hata hivyo ili business kama hii iweze kudumu maana yake kuna kitu behind it. Kinachoshangaza inakuwaje wanaume huamua kupiga simu kwa kulipia ili kusikiliza hao akina dada wanaowaongelesha kimapenzi?

Msingi wa hili jambo unajikita kwenye uwezo wa maneno tunayoongea (power of words), wakati mwanamke anaongea kitu fulani mwanaume huwa na picha kamili (visualization) na hayo maneno yanaweza kumfanya mwanaume kufika kileleni (orgasm)

Je, unajua hao wenye business hii wanasemaje kuhusu aina ya wanaume ambao hutumia hii huduma au huamua kulipa dola zao ili kupata hiyo services ya phone sex kwa umbali wa maelfu ya miles (mwanaume anaweza kuwa British Colombia Canada na mwanamke yupo Las Vegas California USA)?

Ni wale wanaume ambao wake zao kila siku huwapa dose ya;

Naumwa kichwa, sijisikii vizuri, leo nimechoka, leo hapana, siyo hapa, utaamsha watoto, tumbo linaniuma, tutafanya kesho nk

Bottom line ni kwamba:

Maneno unayotumia chumbani na mke wako au mume wako si kwa ajili ya yeye kusikia tu bali hutunzwa, hufundisha na kuwekwa kwenye kumbukumbu, ukirusha neno gumu na la kuumia unaweza kushangaa namna mke wako au mume wako atakavyobadilika na kuwa mtu tofauti huko chumbani.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

No comments: