"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 29, 2010

Je, Kuna Sababu?

SWALI:

Kaka Mbilinyi, kwanza nashukuru sana kwa elimu unayotoa hapa, mara nyingi napita hapa kujipatia tips kwa ajili ya maisha yangu ya mahusiano.

Nami leo nina swali ambalo linanitatiza kwani kawaida Mr. Happy wangu huwa hana tatizo kuwa na erections usiku nikiwa nimelala usingizi au ninapoamka asubuhi, hata hivyo ninapojaribu kufanya sex na mke wangu huyu jamaa ananiangusha mno hataki kuamka, je kuna sababu yoyote?

Jina kapuni

JIBU:

Kaka Jina Kapuni,

Asante sana kwa kupita hapa na kuchukua kile ambacho unaamini unaweza kujifunza.

Kawaida Mr. Happy huwa na erections asubuhi au katikati ya usiku kwa mwanaume yeyote na aina hii ya erections ni tofauti na ile ya Wakati wa sex (sexual erections).

Erections za usiku au asubuhi mwanaume anapoamka (hata watoto wa kiume au vijana wa kiume) ni sehemu ya asili ya mwili (natural body reflex), na hizi erections hutokea kila baada ya dakika 90 ukiwa umelala usingizi.

Unapotaka kufanya mapenzi (sexual erections) hutegemea sana ubongo, mishipa (nerves), mirija ya damu (blood vessels), stress, kuchoka, hofu, mashaka na wasiwasi hayo yote huweza kusababisha Mr. Happy kulegea badala ya kutabasamu na kusimama kukupa salute.

Hayo niliyotaja hapo juu hayana uhusiano wowote na zile erections za usiku na asubuhi unapoamka.

Pia wanaume huwa na kiwango kikubwa sana cha testosterones Wakati wa asubuhi ndiyo maana wanaume wengi hupenda sex asubuhi kuliko wanawake.

Habari njema kwako ni kwamba kama unapata erections usiku ukilala au asubuhi unapoamka maana yake huna tatizo la mishipa ya damu au hormones au nerves kila kitu kipo plugged vizuri kwenye system yako.

Uwezekano mkubwa wa wewe kukosa sexual erections itakuwa ni stress au situation zako kimaisha kama vile kazi, familia, au kukosa kuwa stimulated vizuri kimapenzi (kama umri wako umeenda sana).

Jichunguze kama kuna mgogoro wowote au jambo lolote linalokufanya ufikirie au kuumiza ubongo muda wote.

Pia unaweza kumuona daktari ambaye anaweza kukusaidia kukupa medications ambazo zinaweza kuongeza penile circulations.

No comments: