"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 2, 2010

Je, Kwa nini Unanipenda?

Kama mtu akikuuliza swali lifuatalo;

Kwa nini unampenda mke wako au mume wako au mchumba wako,

utampa jibu gani?

Wanaume wengi (siyo wote) katika kujibu hili swali wanaweza kujikuta wanajibu nampenda mke wangu kwa sababu ana sura nzuri, au ana mguu wa nguvu, au ana macho mazuri au ana umbo zuri au ana nywele nzuri au ana kifua kizuri (matiti) au kwa sababu ni mwimbaji mzuri au kwa sababu wazazi wake ni matajiri, au anapika vizuri nk.

Wanawake nao wanaweza kujikuta wanajibu kwa kuwapa sifa za uhakika waume zao kama vile ninampenda kwa sababu amesoma, nampenda kwa sababu ni handsome, nampenda kwa sababu ana kazi nzuri au ana fedha au kwa sababu amesoma au kwa sababu anakuwepo pale ninapomuhitaji.

Je, utakuwaje kama baada ya miaka mingi kupita na mume wako au mke wako akabadilika vile vitu ambavyo vilikuwa ndiyo msingi wa wewe kumpenda?

Je, utaendelea kumpenda?

Kutokana na ulivyojibu swali hapo juu, Na Kama una akili timamu (logically) jibu linatakuwa huwezi kumpenda tena mke wako au mume wako kwani msingi wako wa kumpenda umeshatoweka.

Kama sababu za kumpenda mume wako au mke wako zina msingi katika qualities ambazo baada ya muda zinaweza kubadilika au kupotea hii ina maana msingi wa kumpenda pia hupotea (love will be over)

Ukweli ni kwamba njia sahihi na kamili ya kupenda mke au mume ambayo huweza kudumu maisha yote ni kumpenda kama alivyo (unconditional love) au kuchagua kumpenda kama alivyo.

“Love is not a feeling; it is a choice and commitment”

Kuna aina tatu muhimu za upendo ambazo huweza kusaidia wawili wanaopendana kudumu; nazo ni upendo wa Agape (true love), pili ni (Phileo) upendo wa urafiki na tatu (Eros) upendo wa kimahaba.

Hata hivyo upendo wa msingi ambao huwawezesha mke na mume kuishi pamoja miaka yote na kushinda yote katika hali zote ni upendo wa Agape.

Upendo wa urafiki (phileo) na upendo wa kimapenzi (Eros) ni muhimu katika ndoa hata hivyo kama ndoa yako ina msingi au imesimamia katika aina hizi mbili (Phileo & Eros) au kufurahia urafiki na mapenzi (sex life) tu basi ndoa au mahusiano yako yamejengwa juu ya mchanga.

Upendo unaojenga ndoa ni ule usio na ubinafsi, usio na sababu au masharti (selfless/unconditional) ambao ni Agape.

Huu ni upendo ambao kuchakaa kwa mwili au kubadilika kwa hali za maisha hakuwezi kutikisa ndoa.

Huu ni upendo ambao huweza kuwapitisha wanandoa katika ugonjwa na afya njema, umaskini na utajiri, katika mazuri na katika mabaya, katika giza na katika nuru ni upendo ambao ni true love.

Ni upendo ambao hata mume akiota kitambi bado mke atampenda, ni upendo ambao hata mke akinenepa na kuwa na kilo 300 bado mume atampenda na kujiona fahari nk.

Ikitokea mume akamwambia mke wake “sina feelings na wewe tena” hii ina maana anasema kwamba “sikukupenda kama ulivyo, bali wakati nakuoa nilikupenda kwa sababu ulikuwa na sura nzuri na sasa umesinyaa usoni ndiyo maana sikupendi, nilikupenda kwa sababu ulikuwa na matiti mazuri na sasa yamelala ndiyo maana sikupenda, nilikupenda kwa sababu ulikuwa portable na sasa umenenepa kama elephant ndiyo maana sina feelings na wewe.

Upendo wake ulikuwa na msingi wa feelings na circumstances na si commitment, hakuchagua kumpenda mke wake bali alijisikia kupenda kutokana na mwonekano au Urembo na si kuchagua kumpenda kama alivyo.

Naamini ukiulizwa kwa nini unanipenda hutajibu;

Nakupenda kwa sababu.....,

bali Nakupenda kwa sababu nimechagua kukupenda kama ulivyo

3 comments:

Anonymous said...

Ni kweli Agape ndiyo upendo wa kweli ambao ni wa kimungu. Kwani Mungu anatupenda si kwa sababu tupo lovable bali anatupenda kwa sababu yeye ameamua kutupenda hii ina maana hatuwezi kufanya kitu chochote ili atupende bali ameamua kutupenda kama tulivyo.
Mungu amemchagua kutupenda.
Nasi tunaweza kupenda au kuchagua kupenda kwa sababu yeye alitupenda kwanza.
Ndoa inaweza kusimama na kudumu kama kuna hii ina ya upendo.

Lazarus Mbilinyi said...

Asante kwa comments, pia ieleweke kwamba ili kuwa na unconditional love, true love ni muhimu sana kuruhusu upendo wa Mungu kuwa ndani yetu, hii ina maana kwamba upendo wa kumpenda mke au mume hautoki ndani yetu bali hutoka kwa Mungu na kukaa ndani yetu na ndipo tunautoa kwa wale tunawapenda.
Kibinadamu hatuwezi ila tukimruhusu Mungu katika maisha yetu hapo tutaweza kuwapenda wake zetu au waume zetu kwa upendo wa Agape ambao asili yake ni Mungu.

mohamadhanif said...

cat-and-girl.blogspot.com


Nice info, keep blogging