"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 9, 2010

Kulaumu!

Kama kuna kitu kinachoweza kuua sex kwenye ndoa haraka iwezekanavyo si kingine bali ni kuishi na mtu ambaye ana jicho la lawama au kulaumu (critical).

Kulaumiana kunapoingia kwenye ndoa mara moja hali ya hewa huanza kubadilika kwani huondoa maana ya unconditional love yaani kumpenda mtu kama alivyo.

Wana ambao hutoa lawama kwa partners wao mara nyingi ni watu wanaojijali wenyewe tu, hawana nerves za kufahamu wengine wanachukulia vipi criticism zao.

Hakuna anayependa kulaumiwa au kupewa lawama kila mara kwani mtu wa lawama hukata na kuharibu msingi imara wa ndoa, huharibu upendo na heshima kati ya mke na mume.

Ikitokea mume ametoa lawama (criticize) kwa mke wake mezani wakati wa chakula cha usiku (dinner), basi moja kwa moja mke hataweza kuwa tayari kimahaba wakiingia chumbani kwa kuwa criticism umeharibu mood ya mke hufurahia ukaribu na tendo la ndoa.

Hataweza kufurahia kwa kuwa taa moja imezimwa na mwili mzima utazima.

Kwa upande wa mwanaume hali ni mbaya zaidi kwani pamoja na kwamba mwanaume huonekana ni kiumbe imara kwa nje bado kwa ndani mwanaume ni mtoto mdogo kabisa. Mume akipata criticism kutoka kwa mke na kama hilo neno limemuua sana basi hukimbilia kwenye cave lake hata mwaka mzima bila kutoka nje. Haijalishi mke atasoma kitabu gani au pokea ushauri gani hakuna kitakachotokea hadi siku moja wakae chini na mke akiri kwamba alikosa na anaomba wasameheane.

BOTTOM LINE:

Kulaumu humomonyoa misingi ya ndoa, na hakuna kingine zaidi ya kumkalia mwenzako na si asili ya upendo.

Unaweza kutokukubaliana na mwenzi wako katika maeneo mengi katika ndoa hata hivyo tatizo si kile unaongea bali namna unavyoongea. Pia badala ya kumshambulia mwenzi wako ni vizuri kulishambulia tatizo lenyewe.

1 comment:

Anonymous said...

Kuna rafiki yangu (mke mwenzangu) amenisimulia namna mume wake amemkasirikia sasa ni mwaka wa 5 katika ndoa yao na hataki kumsamehe kwa sababu baada ya kurudi honeymoon mwanaume alifanya kitu ambacho mke hakufurahi na mke akatoa maneno ya kulaumu kwa kutamka kwamba "Ndiyo maana ulichelewa kuoa" na ni kweli mume wake alichelewa sana kuoa na wamepishana miaka zaidi ya 15.
Hata hivyo huyu mwanaume bado amekasirika kutokana na hiyo sentensi ya siku moja na mwanamke sasa ina m-cost kwani ni kama kila mtu anaishi kivyake.

Ni muhimu sana wanandoa kujihadhari na namna tunaongea, namna tunaongea huweza kuweka sumu kwenye ndoa.

Ubarikiwe!