"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, June 22, 2010

Kuongezeka Umri

Huwezi kugoma kutozeeka, ni muhimu sana kutarajia mabadiliko jifunze kukabiliana na hiyo hali au tarajia mabadiliko kwani mwanamke mwenye umri wa miaka 29 hawezi kuwa sana na mwanamke mwenye miaka 40 na mwanaume mwenye miaka 28 si sawa na mwanaume mwenye miaka 45.

Inawezekana wewe ni mwanaume na umeanza kupoteza kwenye kichwani na inawezekana umeanza kujazia uzito wa ziada kwenye tumbo na una kakitambi ka kiana.

Ulizoea kuruka kirahisi sasa ni mzito huwezi kuruka tena, hapo sijakuuliza masuala chumbani na huyo Mr. Happy wako ana behave vipi.

Inawezekana wewe ni mwanamke na umri ni kweli unaenda na huamini namna gravitational force inavyokuvuta kila kitu kushuka chini ya sakafu.

Unashangaa matiti yanashuka chini na kulala tofauti na zamani, uso nao unainama na kuweka wrinkles, unashangaa nywele zinakuwa ngumu na kuanza kupotea zenyewe bila taarifa, chini kunagoma kuwa wet hata baada ya kusisimuliwa kama ilivyokuwa kawaida yako kwani kwa maongezi tu kila kitu chini kulijibu.

MABADILIKO YA KAWAIDA KIMAPENZI KWA MWANAUME ANAPOONGEZEKA UMRI:

Kumbuka ulipokuwa teenager (siyo wote) ile kusoma gazeti ambalo ni romantic ulikuwa unasisimka (erection), ile kumpita mwanamke mrembo mwili ulikuwa unasisimka.

Mwanzo wa ndoa yako, ukiona mke wako kapanda kitandani tu ulikuwa unasisimka na kuwa tayari kwa Mr. Happy wako alikuwa tayari kashajinyosha na anakugusa ceilings.

Inawezekana kutokana na mwili wako kusisimka kimapenzi haraka kumejenga tabia fulani kwako na kwa mke wako na siku mambo yakiwa tofauti mnaanza kuhaha kudhani kuna tatizo limejitokeza kumbe ni kawaida kwani ni kuongezeka kwa umri.

Inawezekana hata namna ya kuandaana ilikuwa ni one sided kwa maana kwamba mwanaume ndiye alikuwa anasisimuliwa kwa muda mrefu zaidi na mwanamke kwa muda mfupi.

Sasa umri umeongezeka na usipoandaliwa vizuri unaweza kujikuta Mr. Happy anabaki soft muda wote bila kuleta mabadiliko yoyote kama kawaida yake.

Maana yake mwanaume anapoongezeka umri anahitaji direct penile stimulation kuliko zamani.

Ukweli ni kwamba mwanaume anapokuwa kijana hadi kuwa mzee ni mfano wa godoro jipya, ukilinunua huwa gumu na baada ya miaka kadhaa utaona kasheshe yake.

Pia mwanaume anapoongezeka umri anaweza kushangaa anamaliza sex bila kukojoa (ejaculate) kitu ambacho haikuwa kawaida yake, kwani older men kawaida hawahitaji kufika kileleni kama young men.

Hata hivyo hiyo ina faida kwa mwanamke kwani sasa mwanaume anaweza kufika mbali katika kumridhisha mke wake ndiyo maana umri unavyoongezeka mwanaume huwa mzuri zaidi kimapenzi.

Kama ni mwanamke Kumbuka kwamba si kushindwa kwako kama ukiona mume wako wa 40+ amemaliza nusu saa bila kufika kileleni, wala haina maana kwamba humvutii au hupendeza bali ni kuonesha kwamba mwili wake unazeeka.

Inawezekana ilikuwa kawaida yake akimaliza mara ya kwanza baada ya dakika 2 au 3 anaweza kurudi na kuanza upya kukupa mahaba wewe mke wake na sasa hawezi tena.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

5 comments:

Anonymous said...

Niseme ukweli na wazi kabisa kwa mtu amabaye yuko serious na kusoma hii blog basi lazima maisha yake yatakuwa yamebarikiwa kama mimi.
Yaani kila iitwapo leo ndoa yangu ni faraja tupu Mungu akubariki zaidi na zaidi ili uweze kupata muda wa kutoa masomo zaidi.
Ubarikiwe wewe na mke wako Gloria na watoto wako Emmanuel na Karen.

AM

Anonymous said...

kweli leo nimejifunza kitu hii haimaanishi kwamba kaka huwa sijifunzi ila kila siku napata kitu kipya,unajua nimewahi kujihusisha kimapenzi na mtu mzima miaka tangu akiwa na miaka 45 hadi sasa ana 50,kweli nilimpenda kwa sababu ya ujuzi mwingi aliokuwa nao sasa somo hili limenifunza kitu cha ajabu sana,pole sana kipindi hicho nilikuwa na miaka 22 saizi ni 27 nimeachana nae lakini hii imenipa fundisho kwangu,naamini nitakuwa kuwa mzuri kwenye ndoa yangu,usijali ni maisha tu,Mungu amenisamehe nimeokoka siku hizi sitembei na mume wa yeyote,kweli mungu si athumani kwani nami amenipa wangu natarajia harusi hivi punde.asante kaka.unajua huwa naingia humu kubeba maujuzi na umenisaidia pasipo wewe kujua,mume wangu akitoka nje,itabidi nijiulize imekuwaje kwani pamoja na material yote haya!hawezi lakini wote tumeokoka si unajua ukiokoka maisha yako ya zamani yanakuwa historia tu,ndio hivyo tena.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Asante sana kwa ushuhuda wako, umenifundisha jambo kubwa sana na nimebadirikiwa sana kwa namna umeweza kufanya mapinduzi na kuwa na mtazamo mpya katika maisha yako.

Ni kweli tukizijenga ndoa zetu tutaweza kumtukuza Mungu katika ndoa zetu na zaidi tutakuwa na ridhiko la uhakika katika mahusiano.

Ubarikiwe sana sana