"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, June 3, 2010

Mawe Hadi Chumbani!

Mara nyingi wanawake katika ndoa ndiyo huonekana baridi (frigid) linapokuja suala kitandani.

Je, unafahamu kwamba asilimia 15 ya wanaogeuka kuwa mawe chumbani ni mwanaume?

Kuna wanandoa ambao mara nyingi wao hutoa sababu kedekede wanapoingia chumbani na waume zao au wake zao, mara utasikia ooh najisikia nimechoka au nina stress au sijisikii kushiriki au naumwa kichwa.

Wanaweza kuwa ni mwanaume au mwanamke tena wakiwa katika business world ni watu wanaofanya vizuri sana, huko nje ni watu wanaoaminika na kila mmoja anaamini huyu mtu huko chumbani na mkewe au mumewe mambo ni super, hata hivyo pamoja na mafanikio makubwa huko nje wakiingia ndani (chumbani) wanakuwa jiwe.

Haya mawe huja katika category mbili

KWANZA

Ni wale ambao huko nyuma waliwahi kudhalilishwa kimapenzi (sexual abused) na wana mawazo negative kuhusiana na sex, hivyo hufanya kila wanaloweza kukwepa sex kwa nguvu zote.

PILI

Ni wale ambao wanatoka katika malezi ya itikadi ya conservative, wanaamini kwamba sex ni uchafu na kitu kibaya sana hata katika ndoa hii ni pamoja na sexual organs.

Aina hii ya mawe ni yale ambayo linapokuja suala la sex mtazamo wao ndiyo huongea na anaweza ndiyo tufanye ila fanya haraka tumalize basi!

Haya mawe mara nyingi ndiyo husababisha yule anayenyimwa kuanza kupepesa macho nje na inaweza kuleta hatari kubwa sana kwa ndoa yao kuwa na mtu wa tatu (emotional affair).

Kutokana na mmoja kukosa hitaji la kuridhishwa kimapenzi mara kwa mara ndoa hujengwa gap kubwa ambalo unaweza kupitisha gari kubwa (semi trail truck) likapita bila tatizo.

Awe mwanamke au mwanaume kuwa jiwe ni kitu kigumu sana kuishi nacho kwani nani anaweza kulipa mahaba jiwe?

Kawaida inapotokea mwanandoa mmoja anakuwa jiwe hii husababisha hatari kubwa katika kuridhika kwa ndoa.

Ni jambo la busara sana kama hali imekuwa mbaya zaidi kumtafuta mshauri wa uhakika ili aweze kupiga gia ya reverse ili ndoa iwe kwenye mstari maana huumiza sana mwanandoa anapoishi na jiwe.

KUMBUKA

Kukiwa na nia, kuna njia na kama hakuna nia kunakuwa na sababu na mara nyingi sababu huwa “najisikia nimechoka au kichwa kinaniuma au sijisikii kufanya nk” hata hivyo wajibu wako kama mwanandoa ni kuchunguza kwa nini mwingine anaonesha tabia za kuwa jiwe.

No comments: