"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, June 5, 2010

Moyo

MOYO NI KITU GANI?

Ni kitambulisho (identity) chako.

Moyo ni sehemu muhimu ya kuonesha wewe ulivyo, ni kituo cha uhai wako, moyoni ndipo ulipo wewe halisi au unapoishi.

Moyo hutoa reflection ya mtu ulivyo.

Ni chemichemi ya maisha yako.

Kama uso uonekanavyo kwenye maji, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo”.

(Mithali 27:19)

Ni kituo.

Moyo wako upo katikati ya mwili na hufanya kazi ya kusukuma damu inayoupa mwili uhai.

Neno “moyo” limekuwa likitumika kwa centuries nyingi sana likiwa na maana ya kituo cha mawazo, imani, jadi, ari na hatia nk.

Ni makao makuu.

Moyo wako ni ikulu, white house, pentagon ya shughuli zako za kila siku (operations). Kila eneo la maisha yako lina athari na mwelekeo wa moyo wako.

KWA NINI SI SAHIHI KUUFUATA MOYO WAKO?

Moyo wako ni mjinga (foolish).

Watu wa dunia (mataifa) hufuata msemo usemao “Fuata moyo wako” hii ni philosophy ya new age, ni mawazo wa waimbaji wa nyimbo za duniani (pop, romantic novels, vitabu, Tv, Radio nk).

Tatizo ni kwamba kufuata moyo wako ina maana kwamba kukimbilia kila ambacho unajisikia sawa katika hisia zako bila kujali ni sahihi au si sahihi.

Ina maana kujirusha kwenye upepo unaovuma ili kutimiza hamu ya moyo wako bila kujali kama hilo jambo kwa kutumia akili (logic) na ushauri wa watu wengine ni sahihi.

Biblia inasema:

Yeye ajitumainiaye moyo wake mwenyewe ni mpumbavu, bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama”.

(Mithali 28:26)

Moyo wako unapotosha.

Watu hawafahamu kwamba emotions na feelings ambazo zipo moyoni ni kitu shallow na huweza kubadilika muda wowote.

Hisia zilizopo kwenye moyo hubadilika kutokana na circumstances.

Kuna watu wametelekeza kazi zao, wachumba, wake zao, waume zao, wamepoteza akunti zao bank, wametapeliwa pesa zao mitaani nk kwa sababu ya kufuata vile wanajisikia moyoni kwa wakati ule.

Wapo walioachana wake zao au waume zao na kwenda kuoana na partners ambao wanaonekana wanavutia lakini wameshaachwa zaidi ya mara 2 kwenda ndoa zao za kwanza.

Kile kinachoonekana ni kitu kizuri sana ndani ya emotions na feelings moyoni mwako sasa, baada ya muda au miaka kadhaa huweza kuwa ni tatizo kubwa ambalo ni chungu.

Kwa nini mtu ambaye unampenda inafika siku unajikuta humpendi?

Kwa sababu ulimpenda kwa kutumia moyo (emotions na feelings) na hukutumia akili (logic)

Moyo wako ni mharibifu:

Ukweli ni kwamba mioyo yetu ni selfish na sinful.

Biblia inasema:

“Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, ni mwovu kupita kiasi.

Ni nani awezaye kuujua?”

(Yeremia 17:9)

Pia Yesu alisema:

“Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio”.

(Mathayo 15:19)

Hadi mioyo yetu ibadilishwe na Mungu, ndipo haitaweza kuendelea kuchagua vitu visivyo sahihi.

No comments: