"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, June 24, 2010

Mwanamke kujiamini

Kwa mwanamke yeyote ni muhimu sana kufahamu kwamba mwonekano wako ni muhimu sana kwa mume wako pia ni secret weapon ya kuweza kumsisimua mume wako kimapenzi.

Jane ni mwanamke ambaye kifua chake ni flat (small breasted) na hushindwa kujiamini (poor self image). Kabla ya kurudi nyumbani anaamua kununua jarida linalohusu mambo ya wanawake, anapoendelea kulisoma anapitia matangazo yote ya biashara anakuta ni picha za wanawake (models) ambao hakuna anayefanana na yeye (kifua), anapoendelea na safari anajikuta kila alama za matangazo (billboards) anaona picha za warembo ambao wapo na wanaume aidha wakivuta sigara au kupata kinywaji au onesha gari hata hivyo hakuna anayefanana na yeye kifua kuwa flat.

Anapofika nyumbani jioni anawasha TV ili kutazama na anakutana na matangazo ya wanawake warembo headlights kubwa kubwa zikiwa nje nje.

Usiku anapenda kulala anavua nguo na kujiangalia namna matiti yake yalivyo madogo na kujisemea mwenyewe

kwa nini nisiongeze ukubwa kidogo wa haya matiti yangu

Tatizo ni kwamba anadhania, anafikiri kwamba mume wake hawezi kuwa turned on na hayo matiti yake madogo kwa sababu hafananani na wale wanawake kwenye matangazo, magazeti na TV.

Hafahamu kwamba mume wake pia hafanani na wanaume ambao wanapatikana kwenye magazeti, matangazo na TV.

Katika ulimwengu halisi (real world) huwezi kukutana na hao wanawake na wanaume wa kwenye matangazo, magazeti na TV, wengi ni wa kutengenezwa kwa kupakwa rangi, kusafishwa sura kwa teknolojia na Urembo wao si wa kweli.

Tatizo la Jane si kwa sababu ni kifua kuwa flat bali ni victim wa nguvu za kudanganya za mambo ya Urembo.

Hajiamini kiasi cha kujiweka huru kwa mume wake kimwili kwa kuogopa kwamba badala ya kumsisimua anaweza kumgandisha kwa baridi ya kile ataona.

Inawezekana umeshazaa watoto 2 au 3 au 5 na una stretch marks kiasi kwamba unaogopa kuwa huru kwa mumeo.

Inawezekana tangu uzae umeongeza uzito kila 10 nzima na unajiona completely unlovely kiasi kwamba mume wako akikwambia unamvutia unaguna na kujifunika zaidi asikuone sehemu za mwili wako.

Anakwambia mwili wako unamvutia na kumsisimua, wewe unakata na kuficha, kazi kwelikweli!

Unaacha kumsikiliza mume anayekupenda, unawasikiliza watu wanaotaka kuuuzia wewe products zao kwa njia ya matangazo.

NGOJA NIKUPE TIPS

KWANZA

Jikite kwenye uimara wako:

Je, unafahamu mume wako ni kitu gani anakipenda, au anavutiwa zaidi katika mwili wako, kama hujui tafuta au fanya utafiti.

Wanaume huvutiwa na mwanamke au mke wake in packets, yaani anaweza kuvutiwa na mguu wake, shingo, headlights (matiti & chuchu), nywele, macho, uso, kiuno nk.

Kama mume wako anavutiwa na matiti yako basi focus hapo hapo kwa kununua bra, au nguo ya usiku ambayo ukivaa ataacha shughuli zote na kubaki anatazama kifua chako.

Kama ni macho au lips basi fanya kila unaloweza kuhakikisha anapata raha yake na wewe utajisikia kujiamini zaidi.

“Use what you have to full effect and don’t worry about the rest

PILI

Shukuru Mungu:

Kumbuka hukutengezwa au kudundwa kiwandani na wafanyakazi waliokuwa wanafanya overtime siku ya Ijumaa, bali uliumbwa kwa ustadi (designed, crafted, molded & sculpted) na Mungu mwenyewe na ulipozaliwa alikuangalia kwa smile na kukiri kwamba “this is good”

Hivyo mshukuru Mungu kwa kukupa mikono ili uweze kutumia kumpenda mumeo.

Mshukuru Mungu kwa kukupa lips ili umbusu mumeo nk.

TATU:

Kaa mbali na mazingira ambayo huwezi kumudu.

Mpendwa kama unajiona ukivaa swimsuit unaonekana kituko kwa nini ujilazimishe (na swimsuit za siku hizi kwa wanawake ni balaa), kwa nini usivae shorts ili kufunika zaidi na kuendelea ku-enjoy kuogelea.

NNE:

Jifunze kuridhisha hisia zako (sensual)

Hapa si sex bali, kwenda Mahali patulivu wakati wa jua na kunywa soda yako baridi, kukaa na mume wako chumbani huku akikufanyia massage kwenye miguu yako baada ya mizunguko ya siku na maisha, kutumia muda wako siku ya baridi kali kuwa na hot bath nk.

Ni raha sana kuwa na mke sensual huku akiwa umeongeza kilo kadhaa kuliko kukaa na mke ambaye anajilinda na kuongeza uzito ila si sensual.

TANO:

Sex mara kwa mara

Watu ambao hufika kileleni mara kwa mara huweza kusababisha kuzalishwa kwa hormones ambazo huimarisha immune system katika mwili na kupunguza kuonekana mzee.

Utafiti wa watu 3,500 (Royal Edinburgh Hospital) ulionesha kwamba wale walioonekana ni wazee wakati umri wao ni sawa na wenzao walikuwa wanakwepa sex katika ndoa zao.

Have lots of sex

Unapojipa sex maana yake mume wako anafurahia na kukufurahia na anakupenda na matokeo yake utajiamini.

6 comments:

tongchen@seattle said...

Greetings from USA! I love your blog.
Please visit me at:
http://blog.sina.com.cn/usstamps
Thanks!
-Tong

Anonymous said...

Habari kaka L.Mbilinyi!pole na majukumu ya familia na maisha kwa ujumla
Tatizo la kutokujiamin kwa wanawake ni kubwa sana kiasi kwamba mtu hajikubali na kila siku kujiona amepungukiwa,mimi napenda niwape msisitozo wanawake wenzangu kuwa Mungu haumbi mtu mara mbili na wala hakukosea kukuumba jinsi ulivyo,ni madhumuni yake uwe hivyo,katika kutokujiamini ndio maana wanawake wengi sasa hivi wanajichubua,wanatumia dawa za kichina kubadilisha shape,haisaidii kwani bado kujiamini ndio kila kitu,tujivunie jinsi tulivyo,nasisitiza Mungu HATOKURUDIA TENA KUUMBA,Jiamini ni hayo tu ,kazi njema and stay blessed

Anonymous said...

mh!kweli tumetofautiana,yaani mimi mwenyewe nina matiti madogo sana,kiasi kwamba hata nikisema nivae bra huwa inashuka na inanikera,lakini wasichana wenzangu huwa wanayapenda matiti yangu madogo,mchumba wangu yeye si mtu wa kusifia vitu ndivyoa alivyo hivyo hata sielewi ni kitu gani huwa kimemvutia,ingawa nikimuuliza anasema kuwa nanipenda jinsi nilivyo,nina miaka 27 lakini maziwa yangu ova nina miaka 14 nsio kwanza nimetoka kubalehe juzi,wanasema eti nikizaa yatakua sijui ndi nasubiri hivo nione itakuwaje,lakini nafurahi mungu alivoniumba

Anonymous said...

mh!kweli tumetofautiana,yaani mimi mwenyewe nina matiti madogo sana,kiasi kwamba hata nikisema nivae bra huwa inashuka na inanikera,lakini wasichana wenzangu huwa wanayapenda matiti yangu madogo,mchumba wangu yeye si mtu wa kusifia vitu ndivyoa alivyo hivyo hata sielewi ni kitu gani huwa kimemvutia,ingawa nikimuuliza anasema kuwa nanipenda jinsi nilivyo,nina miaka 27 lakini maziwa yangu ova nina miaka 14 nsio kwanza nimetoka kubalehe juzi,wanasema eti nikizaa yatakua sijui ndi nasubiri hivo nione itakuwaje,lakini nafurahi mungu alivoniumba

Anonymous said...

TUNASHUKURU MUNGU HII BLOG YAKO INAMAMBO MENGI SANA MAZURI HONGERA SANA KWA KUELIMISHA WANANDOA JAPO SIJAFIKIA HUKU BUT NAJIFUNZA MAMBO MENGI.

Lazarus Mbilinyi said...

Ni kweli;
Wanawake wengi hawaridhiki na namna walivyo ndiyo maana utaona wengi wanajichubua, wengine wanafanya upasuaji ili kuongeza size za matiti, hips nk ili waonekana vile wanataka wao, jambo la kukumbuka ni kwamba Mungu aliridhika na namna ulivyo na akaona umekamilika pia mume wako au mchumba wako anakupenda kama ulivyo na ameridhika na anaona upo beautiful, usibabaike na wanaoza magazeti au products mbalimbali.
Sijasema usipendeze wala kujipamba bali nasema jiamini na mshukruu Mungu kwa namna alivyokuumba mwanamke mzuri na mrembo wa asili.

Mwanamke ukijiamini unakuwa na nguvu kama ya sumaku kumvutia mume wako.
Kujiamini ni urembo wa kweli.

Ubarikiwe