"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, June 10, 2010

Natamani kumzaba vibao!

SWALI:

Kaka Mbilinyi nashukuru sana namna unatuelimisha kuhusu mahusiano na hasa sisi tulio katika ndoa.

Najisikia furaha na ndoa yangu, pia nampenda sana mume wangu hata hivyo ananiudhi sana kwani hupenda sana kuangalia wanawake wengine tukiwa mtaani au kwenye hotel tunakula chakula kila mwanamke anayeingia na kutoka yeye ni kumkodolea mimacho hadi natamani kumzaba kibao,

Hivi hawezi kunitazama mimi tu?

Hivi ana matatizo gani?

JIBU:

Dada pole kwa tatizo linalokusumbua na nakiri wazi kabisa wewe si mwanamke wa kwanza kuuliza swali hili.

Tatizo kubwa la mume wako ni kwa sababu alizaliwa mwanaume.

Wanaume huvutiwa na kile wanaona (kwa mwanamke).

Mahali popote mwanamke anayependeza (mrembo) akipita Mahali basi mwanaume naturally hujikuta akimtazama zaidi ya mara moja, why? Ndivyo ilivyo ni mother nature.

Ikitokea baba yako, mchungaji mwanaume, au mtu unayemwamini sana ambaye ni mwanaume wote wawe sehemu wamesimama kwenye kona halafu akapita mwanamke mwenye umri wa miaka 28 mrembo ambaye anavutia, nakuhakikishia hizi pillars za zitafanana kwa kitu kimoja nacho ni macho yao yatamsindikiza huo dada kwa sekunde au dakika kadhaa. Hata hivyo kitendo cha kumwangalia huyo mwanamke haina maana kwamba wanawashwa na tamaa bali ni namna mwanaume alivyo kwani kuangalia ni kitu kingine na kuchukua ni kitu kingine.

Jambo la msingi kwako ni muhimu sana mume wako akafahamu namna unajisikia kutokana na kitendo chake cha kukazia macho kila mwanamke anayemuona Mahali popote hasa akiwa na wewe.

Inaonekana ni eneo sensitive sana kwako hivyo anatakiwa kukuheshimu na ajitahidi kuachana na hiyo tabia ya kuangalia wanawake wengine hadi unatamani kupiga makofi.

Nikupe mfano:

Jane yupo katika ndoa ya pili na mume wake James (sijajua sababu za yeye kuwa katika ndoa ya pili) na yupo sensitive sana na mume ambaye anapenda kuwatazamana wanawake mitaani au Mahali popote wakiwa pamoja kwani mume wake wa kwanza aliwahi kutoka nje ya ndoa yao.

Alichokifanya kwa Jane ni kumwambia ukweli mume wake James kwamba “Mpenzi, ukweli ni kwamba sipendi kabisa tabia ya mwanaume kuwatazama wanawake hasa tukiwa mimi na wewe, sijisikii vizuri kwa kuwa mume wangu wa kwanza alinisaliti kwa kutoka nje ya ndoa, huwa inanisumbua sana ninapokuona unawatazama wanawake wengine wakati upo na mimi iwe mtaani au kwenye hotel tunapokula chakula, je unaweza kupendekeza njia muafaka na ya kudumu ambayo itasaidia?”

Wakakubaliana wakiwa hotelini wanakuwa wanakaa meza iliyoukutani na James atakuwa anaketi kutazama ukuta ambako Jane atakuwa anaketi na wao wawili watakuwa wanaangaliana.

James hufurahia kufanya hivyo kwani anampenda Jane na anafahamu Jane hujisikia vibaya kwa kitendo chake (naturally) kujikuta anakodolea macho kila mwanamke.

Wanakiri kwamba si tu inamsaidia James kutoangalia kila mwanamke anayeingia na kutoka bali imesaidia kuimarisha mawasiliano yako wakiwa wawili kwani sasa kila mmoja huelekeza katika kumtazama mwenzake, hapo ni problem solving as team.

Haina maana na wewe ufanye kama wanavyofanya Jane na James bali unaweza kujadiliana na mume wako kuangalia ni namna gani awe ana behave katika nyakati kama hizo.

Kumbuka katika ndoa hakuna kitu kinaitwa “Hili ni tatizo lake” bali “Ni tatizo letu” na kama wote mtasaidiana kutatua tatizo pamoja mnaweza kupata muafaka.

“Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili”

(Efeso 5:16)

No comments: