"Marriage is our last, best chance to grow up."

Saturday, June 19, 2010

Upepo Unavyovuma!

Leo nilitembelewa na rafiki yangu Likoho (siyo jina kamili) ambaye alinilalamikia kwamba mke wake siku zingine wakiwa chumbani haoneshi msisimko linapokuja suala la mahaba na yeye rafiki yangu amekuwa anajitahidi kufanya kitu kilekile kila siku ili kuhakikisha mke wake anasisimka na kufurahia. Hata hivyo tulimaliza mazungumzo yetu kwa kuulizana maswali kwanza.

Unaweza kujifunza kitu, karibu na wewe!

Mbilinyi: Hivi wewe na mke wako unahisi ni nani mwenye nguo nyingi?

Au Nikupe muda uende nyumbani ukahesabu na kunipa jibu:

Likoho: Sihitaji kwenda nyumbani ili kuhesabu na kufahamu mke wangu ana nguo kiasi gani kwani hilo nalijua kwa kichwa na ukweli ni kwamba yeye ana nguo nyingi kuliko mimi.

Mbilinyi: sawa! Je, viatu?

Likoho: Anazo kama pair 20 hivi na mimi ninazo pair tatu tu.

Mbilinyi: Umejibu vizuri inawezekana ili kuhesabu nguo na viatu alivyonavyo utahitaji calculator wakati wewe utahitaji kutumia vidole vyako vya kwenye mikono na ukawa umemaliza kuhesabu nguo na viatu unavyomiliki.

Je, unadhani hii inakufundisha kitu gani?

Likoho: Hii inanifundisha kwamba mke wangu anapenda sana kununua nguo na viatu.

Mbilinyi: Sawa kabisa, swali langu nilimaanisha linapokuja suala la tendo la ndoa kutokana na maelezo yetu hapo juu, hii ina maana gani?

Likoho: Nahisi hana nguo zinazomfanya kuwa sexy (kuvutia kimapenzi) kama nimekuelewa.

Mbilinyi: Rafiki yangu Likoho, ninachotaka kukwambia ni kwamba mke wako inaonekana anapenda vitu tofauti (variety) kuliko wewe.

Hapendi kuvaa nguo ile ile moja Jumatatu, Jumanne, Jumatano na Ijumaa. Hapendi kuvaa kitu kimoja kila siku anapenda kubadilisha, kuwa na kitu tofauti kila siku.

Sisi wanaume tupo tofauti kwa maana kwamba wakati mwingine tunachukulia sex ni kama mchezo wa soka tunapoanza lazima mpira uwe katikati na mchezaji aanze kwa kumpa pasi mwenzake karibu na kuendelea na mfumo ni ule ule hakuna siku mechi ikaanza kwa kuamua golikipa wa timu moja ndo ataanza.

Kama maisha yetu ya kimapenzi na wake zetu yatakuwa katika mfumo wa kuweza kutabiri na kujua kwamba wapi unaanzia na wapi unamalizia basi husababisha mke kuwa bored na hiyo routine.

Ikifika Mahali mke akafahamu hata kuweza kutabiri kwamba sasa utaanza na upstairs kwenye mwili wake na kuishia down stairs kwenye mwili wake maana yake ni routine ambayo ni boring kwani anahitaji variety.

Likoho, mke wako hawezi kuwa sawa au kujisikia sawa Jumatatu usiku kimapenzi kama ilivyokuwa Jumamosi usiku, usiku mmoja anaweza kujisikia kukurukia (adventurous) na kesho akawa anahitaji just to hold her, wiki hii anaweza kupenda kila kitu kuwa slow na wiki ijayo akawa anapenda kurukia kila anachokiona kina move ndani ya nyumba yako pamoja na wewe mwenyewe.

Kazi yako kama mume smart ni kufahamu upepo wa mke wako unavuma kuelekea wapi kila siku ambayo ipo duniani kwani mwanamke ni mtu wa vitu tofauti tofauti.

No comments: