"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, June 28, 2010

Usiruke, Jadili

Mara nyingi ukisikiliza mazungumzo ya wanandoa watarajiwa (wachumba ambao wapo kwenye maandalizi ya harusi na ndoa yao) mara nyingi utasikia mambo mbalimbali yanayohusiana na maandalizi ya sherehe za harusi.

Watanunua kila kitabu kinachoelezea namna gani mavazi yanaweza kupendeza, watahangaika miezi karibu yote kuhakikisha wanapata rangi za harusi, mtindo wa nywele, vyakula vya waalikwa, ukumbi, magari ya kuwasafirisha maharusi na wageni waalikwa, namna ya kuhakikisha kila mgeni atashiriki vipi sherehe nk.

Inasikitisha sana kwamba ni wachache sana hutumia muda wao kuongea na wachumba wao kukaa na kila mmoja kuelezea matarajio yake hukusu sex itakuwaje.

Ngoja nikwambia kitu wazi na halisi, wiki tatu baada ya harusi yako, hakuna hata mtu mmoja atakuwa anakumbuka wewe bibi harusi ulishika ua gani mikononi siku ya harusi yako, hata hivyo issue ya matarajio yako kuhusu tendo la ndoa lita shape maisha yako na mwenzi wako na zaidi namna ndoa itakavyokuridhisha kwa zaidi ya miaka 20 au 30 au 40 na hata 50 ijayo.

Wewe ni mwanamke, inawezekana utakuja kushangazwa sana na huyo kijana ambaye ni mchumba wako kwani inawezekana kichwani mwake anatarajia wewe utaweza kumridhisha kimapenzi usiku na mchana na kila wakati anapokuhitaji kimwili na wakati huohuo wewe unaamini tendo la ndoa ni siku tu tena taa zikiwa zimezimwa na watu wote wakiwa wamelala fofofo mita 100 kuzunguka chumba chenu cha kulala.

Tafadhari sana kama unataka kuolewa au kuoa hivi karibuni ni muhimu sana kukaa chini na huyo mchumba wako weka kila kitu wazi kwa kila mmoja kuwa specific nini anatarajia kwenye ndoa kuhusiana na suala la sex tena ikiwezekana kuanzia siku ya honeymoon.

Muulize nini anahitaji na nini hakihitaji.

No comments: