"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 30, 2010

Wanafika kwa tofauti


Wanaume hufurahia sana kufika kileleni (orgasm).
Hata kama ni sekunde chache hata hivyo zinalipa zaidi kuliko raha ya hekaheka zote hadi kufika hapo.
Ni kweli kwamba mwanaume na mwanamke ni tofauti sana linapokuja suala la kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa.
Mwanamke anaonekana ndiye mwenye uwezo zaidi wa kuwa na wakati mrefu wa kukaa kileleni na pia ana uwezo wa kujirudia kufika kileleni zaidi ya mara moja.
Pia inaeleweka wazi kwamba ni rahisi sana kwa mwanaume kufika kileleni kuliko mwanamke kwani ni wanawake wengi ambao pamoja na kushiriki tendo la ndoa bado hawajawahi kufika kileleni wakati itakuwa gumzo ikitokea kwamba kuna mwanaume ameshashiriki tendo la ndoa na hajawahi kufika kileleni, hayupo!
Pia mwanamke anao uwezo wa kuthibiti kufika kileleni, hata kama mwanaume ataweza kuthibiti kumaliza mapema (ejaculate) kabla hajafikia point ya no return, hata hivyo akishafika hiyo point hawezi kusimama au kugoma asifike kileleni.
Wakati huohuo mwanamke anaweza kuwa alikuwa kileleni na akasikia mtoto analia, anaweza kuacha na kumhudumia mtoto na kuanza kila kitu upya.
Tofauti nyingine katika kufika kileleni kwa mwanaume na mwanamke ni wakati kwa maana kwamba kwa mfano mume amesafiri kwa wiki mbili kwa ajili ya business, mwili wa mwanamke huweza kujizima kiana kwa sababu hayupo sexual active na atahitaji muda zaidi kuupasha mwili kuwa tayari kwa sex na hatimaye kufika kileleni.
Mwanaume kwa upande mwingine ni kinyume na mwanamke, kama hakuwa na sex kwa wiki mbili basi mwili wake utajaza risasi za uhakika na siku akikutana na mke wake hatachukua muda kufika kileleni, kwanza ile kumuwaza mke wake tu tayari Mr. Happy anaanza kufanya vitu vyake (erections).
Jambo la msingi ni mume na mke kufahamu tofauti zilizopo na kuzifanyia kazi ili kusherehekea kitendo cha kuishi pamoja.

5 comments:

Anonymous said...

Ndiyo, kuna kitu nimejifunza hapa, pia ni kweli kazi kubwa ya mwanaume ni kujilinda na kujitahidi asifike kileleni mapema kuliko mke wake wakati huohuo ni muhimu kwa mwanamke kujitoa na kujishughulisha kuhakikisha anafika kileleni na siyo kulala tu na kumwachia mume kila kitu.

Pia naamini si busara sana kwa wanandoa wakiwa chumbani kuulizana "je, umefika kileleni" maneno kama hayo huweza kufanya mwingine a-fake kwamba amefika au kukatishwa tamaa au kujiuliza kwa nini sifiki na matokeo ni kwua frustrated. Pia si kila wakati tunapokuwa chumbani tunahitaji kufika kileleni kwani wakati mwingine sex ni just for bonding!
Maoni yangu tu!

Anonymous said...

samahani kaka mbilinyi lakini naomba kusaidiwa,yaani mimi nina mchumba ambaye tunafikiria kuoana kwani tuna miaka kama miwili na nusu katika uhusiano,sasa tatizo langu kubwa,linapofika eneo la sex mimi ananiudhi sana,kwani anaweza kunipigia simu na kuniambia nakuja kukusalimu lakini nikukuteuchi hujavaa nguo hata moja,usipofanya hivyo mi narudi kwangu,hivi ni halali kweli?mi naona nafanywa kama malaya vile,halafu akifika anaweza kukushikashika kidogo,atapitisha ulimi kidogo ukimshika tu mr happy wake tayari kosa au ukionesha ishara kwamba unaienjoy anainuka na kukuletea mr happy mdomoni na kusema nyonya, haya zamisha yote,sasa mimi anakuwa ananikera sana kwani kuna siku nakuwa katika mood lakini siku nyingine sijisikii kabisa na hasa hizo staili zake mimi ndio zinanikera.hivi hali hii uchumba naomba unisaidie tu nijue huko niendako ili nijue nipambambanaje kwenye ndoa maana ndio tunaiangalia sasa.

Lazarus Mbilinyi said...

Dada asante sana kwa swali zuri.
Mbona makubwa, yaani ninyi ni wachumba na mnachambuana kama karanga kiasi hicho, dadangu mbona unajiuza kwa bei rahisi hivyo?
Ni kweli wewe anakuona ni malaya fulani na anakutumia tu kutimiza tamaa zake na siku anakupiga chini na kwenda kuoa mwanamke mwingine.

Uchumba wa kweli au wachumba wa kweli hujilinda na kulindana kuhakikisha wanajitunza na kusubiri sex hadi wakioana.

Mchezo mnaocheza ni hatari sana na ni tiketi ya moja kwa moja ya kusababisha ndoa isifungwe na ndiyo maana sasa ni miaka 2 na nusu ba bado hamjaoana.

Huyo mwanaume anakutumia tu hana mpango wa kukuoa bali kukutumia tu.

Hivi huwa inakuwaje hadi unakubali kujirahisisha hivyo (kuwa uchi) kwa ajili yake wakati ni wachumba tu?

sex ni kwa ajili ya ndoa na si wachumba hivyo mwambie huyo mwanaume asiye na adabu na heshima kwamba akuoe kwannza ndipo akupigie hizo simu vinginevyo ni dhambi na laana kwa ndoa yenu kwani hamtaaminiana hata siku moja na hakuna dini inayokubali huo upuuzi.

Hata kama unampenda kaisi gani, kujirahisisha namna hiyo dadangu ni hatari mno, kumbuka hajakuoa na anaweza asikuoe na mwili wako ameshauchezea kiasi hicho.

Ikitokea mmeoana na anaendelea na hiyo tabia yake ya kujitanguliza yeye basi kaa naye chini na mwambie kile wewe unapenda kuhusiana na sex, mapenzi ni teamwork, na kila mmoja kumtanguliza mwenzake kwanza. yeye anahitaji kuwa na lengo la kukuridhisha wewe kwanza ndipo na wewe umridhishe yeye, sex ni two way street na huwezi kufanya kile ambacho yeye hapendi na yeye hawezi kufanya kile ambacho wewe hupendi.

Kama kweli anakupenda basi ukikaa naye na kumwabia kile unahitaji katika mahusiano yenu atakusiliza na kama hatakusiliza huyo ni mwanaume bomu na hatari kabisa kuishi naye. Kumbuka kama mwanaume ni rafu kabla ya kuoana basi mkioana atakuwa rafu mara 7.

Pole sana, dada jitunze kwani heshima ya mwanamke ni kubana malinda kabla ya kuolewa na si kujiweka rahisi hivyo, naamini unadhani unafanya jambo la maana sana kwa huyo mwanaume, kumbuka hajakuoa na anaweza kukuacha tu kwani huna jipya.

Jitunze, jitunze, jitunze ........ tafadhari sana.

Anonymous said...

Habari kaka Mbilinyi ,japo umepotea muda sasa kwali likizo inaonekana imeisha lakini hatukuono tena.
Samahani mimi sijui kama nilisha wahi fika kileleni. kwani m'ke akifika kileleni anakuaje? naomba msaada wako.

Lazarus Mbilinyi said...

Pole sana dadangu,
Ni kweli likizo inaonekana imeisha ila imekuwa tamu sana kiasi kwamba nimeamua kuongeza mwezi mmoja zaidi.

Kuhusu swali lako la mwanamke kufika kileleni inakuwaje nitakujibu kwa makala kamili kwani ni complex na kila mwanamke ni tofauti.

Ubarikiwe