"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, June 23, 2010

Wanapoongeza Umri!

Wanahakikisha wametumia kila kipande cha furniture ndani ya nyumba.

Kwa wanawake anapofika umri fulani huweza kufanya mabadiliko makubwa ya kuongezeka kwa umri kitaalamu menopause.

Kisaikolojia ni kama kuna kuwa na mstari ambao huchorwa kuelekeza kwamba sasa huwezi kuzaa tena.

Hata hivyo jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba mwanamke anapofika huo umri pamoja na kwamba hawezi kuzaa tena anaweza kujihusisha ukaribu wa kimapenzi na mume wake bila tatizo wala kuwaza kuhusu mimba.

Ingawa ni kweli wanawake wengi hujikuta wamepoteza kiwango cha hormone za estrogens bado wanaweza kuwa na libido kubwa kabisa na kuendelea kufurahia intimacy na waume zao.

Ingawa ni kweli kuna baadhi ya wanawake wakifika hii hatua hupoteza hamu ya tendo la ndoa hata hivyo kuwa wengine wameripoti kwamba baada ya kufikia hatua wa menopause hujikuta wakitumia kila kipande cha furniture ndani ya nyumba au kila chumba kuhakikisha kinahusika na adventures za mahaba.

Pia faida ya wanawake ambao wameshapita umri wa kuzaa wanakuwa hawapati siku hii ina maana wanapata nyongeza ya siku 3 au 5 ambazo walikuwa wanatumia kwa kupata siku na sasa zitakuwa free kwa ajili ya sex.

Ingawa kimwili aina hii ya wanawake wanahitaji kuwa makini na genitals kwani kupungua kwa kiwango cha homoni za estrogens husababisha kuta za uke kuwa nyembamba zaidi na kavu zaidi, atahitaji kutumia lubrication zaidi na pia mume muelewa kwani mnaweza kuishia kuumizana.

Pia jambo kubwa ambalo wanawake wengi wenye umri mkubwa (miaka 50, 60 au 70) hawaijui kwamba ili kuwa na maisha mazuri ya kimapenzi (sexual) wanahitaji kujihusisha na tendo la ndoa mara kwa mara (mara moja kwa wiki) utaweza kupata lubrication zaidi kuliko kutojihusisha kabisa.

Hapo ndo utasikia ule msemo kwamba;

“Use it or lose it”

3 comments:

Anonymous said...

Nikweli, umri huu ni mzuri sana kwani hakuna usumbufu wa watoto so kila siku ni raha, ila setback kubwa ni kwamba mnakuwa mna pesa, mna muda ila energy hakuna.

Kila jambo la wakati wake

Anonymous said...

mh!jamani sasa kaka uatusha sisi ambao tunaingia 30 na hakuna mpango wowote wa kuingia katika ndoa wala kuzaa,maana hofu imenishika kwani mpaka sasa siajajua ni lini nitaanza kuzaa

Lazarus Mbilinyi said...

Haaaaaaaa, dada haina haja kubabaika, miaka 30 ni namba ndogo sana na bado binti mbichi kabisa na huo ndo umri sahihi wa kuolewa na kuzaa watoto na huwezi jua kwani kesho inaweza kuwa siku yako ya kukutana na mwanaume ambaye atabadili sexuality yako.
Ungekuwa una miaka 48 kwenda mbele hapo sawa inabidi uanze kujipanga maana kuanzia hapo system ya mwili huanza ku-shut down, vinginevyo furahia maisha, tafuta marafiki wapya wa kike na kiume na jiamini, jipambe na usisahau kuhakikisha uso wako unakuwa na smile muda wote.
Pia mwamini Mungu kwamba anaweza kufanya muujiza muda wowote.

Ubarikiwe