"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, July 27, 2010

Wanapenda Vitu Tofauti


Watu wengi hujiuliza kwa nini likija suala la nguo na viatu wanawake au mke huwa na nguo nyingi na viatu vingi na aina tofauti kwenye closet tofauti na mwanaume.
Mfano; ames anakiri kwamba mke wake ana zaidi ya pair 50 za viatu wakati yeye ana pair tatu tu, na linapokuja suala la nguo basi atahitaji calculator ili kujua idadi ya nguo za mke wake wakati yeye atatumia vidole vya mikono yake miwili kuhesabu ili kufahamu nguo alizonazo.
Swali la kujiuliza hivi hili suala linatufundisha kitu gani kuhusiana na mwanamke katika ndoa?
Hasa linapokuja suala la sex?
Linatufundisha kwamba katika yote hana nguo muhimu ambazo ni rasmi kwa ajili ya sex; si kweli.
Ukweli ni kwamba mwanamke au mke hupenda vitu tofauti (variety) linapokuja suala la sex. Ndiyo maana hawezi kuvaa nguo ile ile moja kila jumatatu au jumanne au jumatano au jumatatu inayofuaata anahitaji kitu kitofauti (variety).
Hata hivyo linapokuja suala la sex kwa mwanaume mara nyingi tunafanya bila kuhitaji utofauti wowote, tunajua nini tunaenda kufanyia, namna tunaenda kufanyia na tutaishia wapi.
Tatizo ambalo hujitokeza ni kwamba mke huwa bored na huo utaratibu (routine). Inafika mahali mke anafahamu au predict nini mume atafanya kwa sekunde tu, mke anaweza kutabiri mume atatumia muda gani huko upstairs kabla ya kwenda down stairs; mke wako anahitaji zaidi ya hapo anahitaji kitu kipya baada ya muda ndo maana havai nguo zilezile na viatu vilevile kama wewe.
Ukweli ni kwamba kama wewe ni mwanamke ni muhimu sana kufahamu kwamba mke wako alivyokuwa jana sivyo atakavyokuwa kesho linapokuja suala la sex, anavyojisikia jumamosi si vile atajisikia jumatatu au jumatano kila siku ni tofauti na mood tofauti.
Usiku mmoja anaweza kukuhitaji wewe umkumbatie tu usiku mzima, siku nyingine atataka muwe na adventure au just for quickie, usiku mwingine slow sex, usiku mwingine atatamani kurukia kila anachooa kina move chumbani pamoja na wewe nk.
As husband; your job is to figure out which direction the wind is blowing each particular day.
Siku njema

Wednesday, July 21, 2010

Anajua Anachokifanya!

Mara nyingi siyo (mara chache) mume au mke hujikuta mwenzake ni msumbufu kwa kuuliza maswali ambayo hayana msingi kwa kuwa kinachoulizwa ni kile ambacho mume au mke huwa anafahamu namna ya kukifanya.

Nahisi bado hujanielewa naongea kitu gani labda nikupe mfano.

Siku moja Jane na mume wake James waliamua kwenda kuwatembelea wazazi wa John ambao wapo nje kidogo ya mji wanaoishi.

Hata hivyo baada ya kufika nyumbani kwa wazazi wao wakaambiwa kwamba wazazi wao nao walipanga kwenda kutembelea shamba.

Wote kwa pamoja yani Jane, James, mama yake James na baba yake James wakapanda gari moja na kuanza safari ya kuelekea shamba.

Jane alikaa kiti cha mbele na baba yake James (mkwe) ambaye ndo alikuwa dereva na James alikaa kiti cha nyumba pamoja na mama yake.

Baada ya kusafiri kwa muda fulani James akahisi baba yake anaenda au kuelekea njia ambayo si yenyewe hivyo akamnong’oneza mama yake kwamba baba yake anaenda njia ambayo si yenyewe

(aliamini kwa kumwambia mama yake basi mama yake ataropoka maneno yasiyopimika kumsema baba yake kwa kitendo cha kuendesha gari kwenda njia ambayo si sahihi).

Cha ajabu mama yake akamjibu James kwamba “Baba yako anajua anachokifanya” kitu ambacho kilimfanya James ajiulize kwani angekuwa ni yeye anayepotea na kuelekea mahali siko mke wake angemsema kwa fujo kama kawekewa vuvuzela mdomoni.

Ni kweli baba alipotea njia hata hivyo baada ya muda akakumbuka kwamba amekosea hivyo akageuza gari na kuelekea kule ambako ni sahihi.

(alikuwa anajua anachokifanya)

Walipofika shamba baba yake aliiweka kofia yake juu ya kiti na baada ya muda akaamua kukaa na akawa kasahau kwamba anaikalia kofia na kuikunja kunja; ndipo James akamwambia mama yake

“Unamuona baba anakalia kofia na kuikunja si mwambie anakalia kofia yake?”

mama yake akamjibu James kwamba

Baba yako anajua kile anakifanya

jibu ambalo pia lilimfanya James afikirie upya kuhusiana na mahusiano yake na mke wake hasa suala la kukosoana vitu vidogo vidogo kama hivi.

Inawezekana umemwambia mume wako anatakiwa kupaka rangi nyumba na kila siku unarudiarudia kumsema ukiamini kwa kumpigia kelele basi ataanya kile unasema, Mumeo anajua kile anakifanya ndiyo maana pamoja na kumsema nyumba bado haijapakwa rangi!

Inawezekana kila siku unamwambia mke wako anatakiwa kuhakikisha drawer za makabati zinafungwa kila akifungua hata hivyo kila siku unazikuta zipo wazi, ukweli ni kwamba mke wako anajua kile anakifanya.

Ni kweli inawezekana umeshamwambia mpenzi wako akufanyie kitu Fulani na ni muda sasa umepita na bado hajatimiza au hajafanya, umeamua kumsema kila siku ili afanye au kutimiza ahadi yake, hata hivyo ukweli ni kwamba yeye ni mtu mzima na anajua kila anakifanya.

Kumbuka kuwa kwenye ndoa ni kuwa mtu mzima na mtu mzima hapigiwi kelele kama mtoto kwani kila mtu mzima anajua anachokifanya na hakuna kitu mwanaume hapendi kama mwanamke ambaye kila wakati ni kukosoa na kusema sema tu (kefyakefya) na kumuweka kundi moja na watoto;

Ukweli ni kwamba mume wako anajua anachokifanya pia mke wako anajua anachokifanya.

Wengi tumegundua hii siri hatupigishani kelele kwani nikimwambia mke wangu leo nitaosha dishes zote au nitakusaidia kufua nguo hana haja ya kuniliuza au kunikazania utafanya saa ngapi hiyo kazi badala yake anatakiwa kurelax na kuenjoy maisha kwani mume wake ninajua ninachokifanya na ninafahamu nitafanya wakati gani period.

Usiumize kichwa chako, anajua anachofanya!

Monday, July 19, 2010

Likizo

Kwa wasomaji wote wa blog hii, napenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha kwamba nitaanza likizo ya mwezi mzima na sitaweza kupatikana mara zote kama kawaida hasa kutokana na kutumia muda mwingi na familia katika mapumziko.
Kama una swali unaweza kunitumia hata havyo majibu yanaweza kuchelewa kutokana na kukosa muda.
Zaidi nashukuru sana kwa namna ulivyofanyika baraka kwangu na familia yangu maana bila wewe kuja kusoma hapa nisingeweza kujifunza na hatimaye kukua katika fikra na kuwa mtu anayefaa katika jamii.
Safari yangu na familia itaanzia Toronto tarehe 19/07/2010 kwenda Dubai na hatimaye Dar es salaam na baada ya hapo tutakuwa Njombe hadi tarehe 15/08/2010
Mungu akubariki sana

Friday, July 16, 2010

Kumlinda Mr. Happy


Afya ya mwanaume ni kitu muhimu sana na ni kitu kizuri.
Je, umewahi kusikia usemi kwamba mwanaume mwenye afya ni yule ambaye anaweza kusimamisha uume wake bila matatizo?
Hii ina maana kama wewe ni mwanaume, afya ya uume wako ni kitu muhimu sana, wanaume wengi hawana mpango wa kujali afya ya kiungo hiki chenye thamani.
Ni jambo la kawaida kwa mwanaume kuhakikisha unakuwa na erection kila siku.
Je, Mr. Happy wako kila asubuhi huamka huku amekupigia salute?
Kama Mr. Happy anakusalimia kila asubuhi basi afya yake ipo fantastic.
Je, ni namna gani unaweza kumlinda Mr. Happy kuwa imara na mwenye afya tele kila wakati?
MOJA: UWE MAKINI NA VYAKULA
Mlo ambao haufai kwa moyo pia ni hatari kwa Mr happy kupata erections.
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba kula vyakula ambavyo husababisha heart attack pia huweza kuzuia flow ya damu kwa Mr. Happy kule south pole.
Wanaume wambao wanakula matunda, mboga za majani, nafaka kamili, na mafuta ambayo hayana fatty kama vile olive oil na samaki wanauweza wa kuwa na erections bila matatizo.

MBILI: UZITO WAKO

Mwanaume ukiwa overweight unajikusanyia matatizo mengi sana ya kiafya.

Hii ni pamoja na diabetes (hasa type 2) ambayo husababisha kuharibika kwa nerves mwilini na nerves zikiharibika huko kwa Mr. Happy basi inakuwa ngumu sana kuwa na erections.

Ndiyo maana wagonjwa wa kisukari hujikuta wanakwepa kwepa chumbani mama akishamvalia kipande cha kagha kwani Mr. Happy huanza kufanya yale ambayo hajatumwa (anagoma)

TATU: SHINIKIZO LA DAMU

Kuwa na kiwango cha juu cha cholesterol na shinikizo la damu huweza kuharibu mishipa ya damu na hii ni pamoja na huko chini kwa Mr. Happy na hii hupelekea kukosa erections.

NNE: KILEVI

Walevi wa pombe wengi huishia kuharibu maini, nerves na hali zingine ambazo hupelekea kukosa erections.

Chapombe wengi hujikuta wanashindwa kuwa na erections ili kuwaridhisha wake zao.

Hivyo kama ni mlevi acha pombe

TANO: MAZOEZI
Kuna ushahidi ulio wazi kwamba wanaume wengi ambao maisha yao ni sedentary (kulaza damu, kukaa tu kizembezembe) hushindwa kuwa na erections.
Mazoezi ya kukimbia, kuogelea husaidia kuimarisha erections.
Pia kuendesha baiskeli kwa muda mrefu huweza kusababisha kukosa erections, ingawa kuendesha baiskeli kwa safari fupifupi haina shida, pia ni muhimu kuvaa pants nzuri na pia kusimama kwenye baiskeli mara kwa mara, pia uwe makini na aina ya seat ya mkweche wako kwani kuna seat husababisha genital numbness.
SITA: TESTOSTERONE
Hata mwanaume mwenye afya njema, anapofika umri wa miaka 50 kiwango cha homoni ya testosterone huanza kupungua na dalili mojawapo ni kukosa hamu ya sex, kuwa na mood tofauti tofauti, kukosa stamina, au kushindwa kutoa maamuzi haraka, ukiona hivi wasiliana na daktari wako aangalie ni vipi anaweza kukusaidia.
SABA: OGOPA STEROIDS
Haya madawa hutumiwa na wanamichezo ili kuongeza nguvu au kwa mabaunsa (body builders).
Tatizo la haya madawa huweza kuzikamata na kuzibana balls kiasi cha kushindwa kutengeneza testosterones.
NANE: ACHANA NA SIGARA
Kuvuta sigara huweza kuharibu mishipa ya damu na huzuia damu kumfikia Mr. Happy pia nicotine ndani ya sigara huweza kufanya mishipa ya damu kusinyaa na huzuia damu kwenda bondeni na matokeo hakuna erections.
TISA: CHUNGA SANA NAMNA MR. HAPPY ANAVYOJIDAI
Baadhi ya matatizo ya kukosa erection hutokana na injuries za Mr. Happy wakati wa sex.
Kuzuia Mr. Happy asiiname kwa maumivu ni muhimu kuhakikisha kwamba kabla ya kuingia kwenye uke, uke unakuwa wet na lubricated kiasi cha kutosha.
Na kama mwanamke anajizungusha kiasi cha kumpindisha Mr. Happy hadi unajisikia maumivu ni vizuri kujipa stop palepale au kutafuta style nyingine ambayo Mr happy atajisikia comfortable.
Kama mwanamke yupo on top na wakati anajipendelea na downward and upward movement na Mr. Happy halengi uke na kuingia sawasawa, maana yake Mr. Happy anaweza kuwa crushed na hakuna uume duniani unaweza kuhimili hicho kitendo.
KUMI: ZUIA MSONGO WA MAWAZO
Ukiwa na msongo wa mawazo (stress) maana yake kiwango cha adrenaline mwilini kinakuwa tofauti na matokeo yake mishipa ya damu husinyaa na damu haitaweza kwenda kwa Mr. Happy na kama kawaida Mr. Happy akikosa flow ya damu basi hawezi kuwa na erections.
Kuwa bora emotionally ni kuipa sex boost.

Unanipendaje Hasa?

Tukubaliane kwamba kuna vitu ambavyo mke au mume ukifanyiwa na mume wake au mke wake hujisikia anapendwa au kwamba mke wake au mume wake anakujali.

Wote tunapenda kupokea zawadi kutoka kwa wapenzi wetu ila kuna wengine akipokea zawadi hujisikia anapendwa zaidi na mwingine huona ni kawaida, wote tunapenda kukaa na wapenzi watu na kutumia muda pamoja (quality time) hata hivyo kuna wengine bila kukaa na kuongea na mume wake au mke wake anajisikia hapendwi hata kama amenunuliwa gari nk.

Wengine kupendwa ni kusaidiwa kazi au kufanya kazi pamoja, wengine kupendwa ni mguso (touch) bila kukumbatiwa, busu au sex kwake hajapendwa.

Kwa maelezo zaidi soma hapa.

MFANO

Jane amezaliwa katika familia ambayo mama yake alikuwa anapika chakula kitamu sana kiasi kwamba baba yake alikuwa anamsifia mama yao kila wakati kwa huo uhodari wa kuandaa misosi ya nguvu, baada ya Jane kuolewa naye hutumia muda mwingi kuandaa chakula cha nguvu ili mume wake James afurahi kama alivyokuwa anafurahi baba yake kutokana na mapishi mazuri ya mama yake.

Hata hivyo James yeye anasema hajali sana suala la chakula kwani kwake chakula chochote sawa tu na anamshangaa sana mke wake Jane ambaye hutumia muda mwingi kupika badala ya kutumia huo muda kufanya mambo mengine.

Jane hujisikia vibaya kwa sababu pamoja na kupika chakula kitamu na cha uhakika mume wake James huwa hatoi sifa zozote wala kumtia moyo na badala yake anakatishwa tamaa na kujiona hapendwi.

James naye anaona mke wake hana heshima kwa kuwa anapenda kupika tu na hilo haligusi moyo wake na kujiona kweli ana mke anayemjali.

Tatizo ni kwamba Jane hajaolewa na baba yake bali ameolewa na James, linapokuja suala na kupendwa kwa mume wake misosi haina maana yoyote bali kukumbatiana, kupeana busu na kukaa chumbani na kufurahia raha ya kuwa mke na mume.

James anakiri kwamba mke wake anapokuwa active kimapenzi na kuwa karibu kimapenzi hujisikia anapendwa na mke wake kuliko suala la chakula kitamu.

++++++++++++++++++++++++

Jacqueline na John sasa ni miaka 35 kwenye ndoa yao; Jacqueline anajisikia afadhari kuachana na John kwa kuwa hakuna jipya kwani moto wa mapenzi katika ndoa umezima kabisa.

Jacqueline anakiri wazi kwamba yeye na mume wake hawana tatizo lolote la kifedha wala hakuna siku wamejikuta wanagombana hata hivyo anajisikia hakuna upendo wowote kutoka kwa mume wake.

John alipoulizwa unafanya kitu gani kuhakikisha mke wako Jacqueline anafurahi na kujisikia anapendwa.

John alieleza kwa mshangao kwamba hamuelewi mke wake anataka kitu gani kwani amejitahidi kufanya kila kitu ambacho mwanaume anaweza kufanya ili mke ajisikie happy lakini mke anaendelea kulalamika kwamba anajisikia hapendwi.

John anasema anajitahidi kuhakikisha anapika chakula cha usiku (dinner) mara 4 kwa wiki, siku mbili zinazobaki wanaenda out na rafiki zao, anaosha dishes hizo siku nne kwa wiki, anasafisha nyumba kila siku kwani mke wake analalamika kwamba mgongo unamatatizo, anajitahidi kusafisha mazingira nje ya nyumba na pia kufua nguo na kuzinyosha nk

Unaweza kujiuliza sasa huyu mwanamke analalamika kitu gani kama mwanaume anaweza kujishusha na kufanya hayo yote na bado mwanamke anaendelea kulalamika.

Jacqueline alipiulizwa je, ulitaka mume wako afanye kitu gani ili ujisikie unapendwa akajibu kwamba angefurahi kama ingetokea siku moja mume wake akaketi kwenye kochi na yeye na wakakaa na kuanza kuongea pamoja, kusikilizwa huku wakiongea mambo mbalimbali yanayohusu ndoa na maisha yako hapo Jacqueline angejisikia kupendwa kwani kila wakati mume wake ni kuzunguka huko na huko mara kupika mara kusafisha nyumba mara nje (yard) yaani yeye na kazi tuu na mke hana nafasi.

Jacqueline anasema anachotaka ni mume wake kukaa chini na yeye angalau dakika 20 kwa siku, waangaliane usoni, waongee mambo yanayowahusu wao na maisha kwa ujumla, huko ndo Jacqueline anaona ni kupendwa (quality time)

Hii ina maana kwamba kwa John kubwa busy hata kama ni kumsaidia kazi mke wake bado hakuweza kutimiza hitaji la emotions kwa mke wake.

Bado love tank la mke wake lilikuwa empty na kujazwa ni pale wakiwa pamoja, kukaa pamoja, kuongea pamoja.

Sasa John anakiri kwamba kwa miaka yote 35 alikuwa hajajua kwa nini mke wake alikuwa analalamika kwamba hawaongei, anakiri aliamini akimuuliza mke wake umeamkaje basi huko ndo kuongea, hakujua kuongea ni kukaa chini, kutazamani na kuongea na mmoja akisikiliza kwa dakika 20 au 30 na ndicho mke wake alikihitaji.

Mara nyingi wanaume tunapoona nyumbani kuna chakula, kuna fedha kuna kila kitu tunaamini basi mke atakuwa ameridhika kihisia kitu ambacho si kweli kwani kila mwanamke ana aina yake hasa ambayo kwake ni kupendwa.

Thursday, July 15, 2010

When asked his secret of love, being married fifty-four years to the same
person, Bill Graham said,

"Ruth and I are happily incompatible."

Wednesday, July 14, 2010

Wanaume bwana!


Kwa nini wanaume wanahitaji sex na wanawake wanahitaji upendo.
wanaume huwa frustrated na wanawake kwa kuwa hawapendi sex na wanawake huwa frustrated na wanaume kwa kuwa kila mara wao ni sex tu.
Wanawake wanawalaumu sana wanaume kwa kuwa hawajui kupenda na wanaume wanawalaumu sana wanawake kwa kuongea tu kuhusu upendo lakini hawataki kuonesha vitendo (kufanya mapenzi).

Sababu inayofanya binadamu kujihusisha na sex ni kutokana na hormone ya testosterone, ambayo kwa kiwango kikubwa ni hormone ya wanaume.
Mwili wa kawaida wa mwanaume huzalisha mara 20 zaidi ya mwili wa mwanamke.
Kwa maneno mengine, hamu ya sex kwa mwanaume katika siku moja ni sawa na hamu ya sex kwa mwanamke baada ya kukosa sex kwa siku 20 au hamu ya kuhijitaji sex kwa mwanaume katika siku 20 ni sawa na hamu ya mwanamke kukosa sex kwa mwaka mzima.

Kwa kufahamu hizo tofauti hadi hapa unaweza kufahamu maumivu ambayo jinsia nyingine inayapata.
Kumbuka wanaume kuhitaji sex hadi kupitiliza hawajasababisha wao au ni kitu wanajitakia bali ndivyo wameumbwa na hizi ni sababu zinazofanya mwanaume kuwa mwanaume na mwanamke kuwa mwanamke.
Wanaume na wanawake ni tofauti.
+++++++++++++++++++++++

Mwanaume anaweza kuzalisha au kusababisha mimba kwa mwanamke kila anapofanya sex, lakini mwanamke anaweza kuzaa mtoto kila baada ya miaka 2; hii ina maana mwanamke lazima awe makini kuchagua sana (picky) mwanaume wa kuoana naye ili kuzaa naye watoto.
Lazima achague the best seed.
Kwa miaka mingi (generations) wanawake wamekuwa wakilipa gharama (price) kutokana na kuchagua wanaume wasiofaa (mbegu dhaifu); kwani wanawake waliochagua wanaume wenye udhaifu wa genes wamesababisha kuwa na watoto (offspring) ambao imekuwa si rahisi kuishi (survive); wanawake waliochagua wanaume wenye genes imara wamezaa watoto imara ambao waliishi, na hawa ndio wanabeba genes za mama zao za kuwa wachaguaji wa kupitiliza (picky) linapokuja suala la kuoana hadi leo, na moja ya hao offspring ni wewe.

Kwa asili wanaume huhitaji sex mara kwa mara ili kusambaza kizazi wakati wanawake huhangaika kutafuta the best seed ili kuwa na maamuzi bora ya kupata mbegu bora ya kuwa na kizazi bora.

“Men seek quantity - women seek quality”
Ndiyo maana wanaume wanahitaji sex na wanawake wanahitaji upendo.

Upendo ni uhakika ambao wanawake huhitaji kwa mwanaume ili kuhakikisha atashikamana naye kusaidia kulea watoto na kuhakikisha wanakua, na sex kwa mwanamke ni kitu cha ziada anachotoa kwa mwanaume ili awe committed kwake.

Kwa mwanaume sex ni kitendo cha kimwili ambacho husaidia kupunguza msukumo wa hormone ya testosterone ndani ya mwili wake na baada ya kufanikisha ndipo mwanaume huanza kuhisi upendo kwa mwanamke au hujikuta mwanamke huyo hana thamani tena kama hakuna commitment (ndoa)
Ndiyo maana wanaume wengi hupotea baada ya kukipata kile walikuwa wanakitafuta kwa mwanamke kwa kuwa issue nzima ilikuwa ni testosterone na si upendo.
Ndiyo maana mwanamke kumpa mwili mwanaume mapema kabla ya ndoa ni hatari sana kwani wanawaume wengi huwa hawajawa tayari kupenda (huwa anakuwa bado hajampenda mwanamke bali ni msukumo wa testosterone).
Mwanaume huhitaji muda ili feelings zake ziwe developed na njia sahihi ambayo mwanamke anaweza kufanya ni kukaa mbali na maombi yake ya sex.
Kama ataweza kujizua kufanya sex maana yake ataweza kujenga upendo wa kweli ambao ndiyo msingi wa mahusiano, kinyume na hapo baada ya sex ataishia na mwanamke atajikuta anakuwa mtumwa.

sababu ya wewe kuwepo hapa leo ni kwa vile ancestors, wanaume na wanawake walifanya maamuzi sahihi na wakaweza kuvutia partner sahihi (best seed) ambaye leo wewe upo.
Hivyo haina haja kujisikia uchungu sana kwa mume kuhitaji sex mara kwa mara na mke kuhitaji upendo au kupendwa mara kwa mara.

Tuesday, July 13, 2010

Tatu Bora kwa Mke!


Happy wife; happy life
Tafiti nyingi zinaonesha kwamba usemi wa hapo ni kitu cha kweli; pia tafiti nyingi zinaonesha kwamba unapomchagua partner wa kuoana naye maana yake unachagua tatizo la kudumu nalo au raha ya kudumu nayo miaka 10, 20 au 30, 40, 50 ijayo.
“You can run; but you can’t hide”
Hata hivyo pamoja na hayo suala la kuwa na ndoa inayoridhisha haliji automatic ni suala la kuwekeza kujitoa na kufanyia kazi kuanzia mambo madogo madogo ambayo mwenzi wako anahitaji kutimiziwa.
Mume anapotoa maisha yake kwa mke wake maana yake ni hawi selfish na kutokuwa selfish ni jambo zuri ambalo linaweza kumfanya mke kuwa na furaha katika maisha na ndoa kwa ujumla.
Pia mume anapoishi vibaya na mke wake, hata akiomba maombi yake hayana maana, hii ina maana ili mume apate kibali cha maombi yake ni muhimu kuishi vizuri kwa kumpenda mke wake.
Je, ni mahitaji gani ya msingi kwa mke katika ndoa?
1. MAWASILIANO
Ni muhimu mno kwa mume kuamua au kuchagua kuwasiliana na mke wake, kuwasiliana na mke maana yake kumpa muda wa kuongea naye (quality time).
Pia si ustaarabu kwa mume kutumia neno “safi tu” au “fine” pale akiulizwa kuhusiana na kazi au vile anajiskia.
Fikiria mume unarudi kazini na ile kufika nyumbani mke wake anamuuliza
vipi honey habari za kazi?”
Na mume anajibu “safi tu
then anaendelea na ratiba zake za kusoma gazeti au kuangalia TV.
Kumbuka mwanamke hahitaji headlines au bottom lines; anahitaji full story, anahitaji habari kamili.
Ndiyo maana wanawake wengi huonekana ni the noisiest human being (vuvuzelas) kwa kuuliza maswali mengi huku wakijua mume hana hamu na kuongea, hata hivyo kwao ni kilio cha kutaka kusikilizwa, mtu wa kuwasiliana naye ambaye ni wewe mume.
Ni kweli wanaume wengi baada ya kazi na mihangaiko ya maisha kwa siku nzima anaporudi nyumbani huwa ameishiwa maneno ya kuongea hata hivyo ni muhimu sana kumpa mke angalau dakika 15 kuongea naye tu habari za kazi na maisha kwa ujumla kwani anahitaji connections kutoka kwa mume.
Mke anahitaji neno kwa neno kila kile unafikiria, mke anahitaji connections na mume wake angalau dakika thelathini kwa siku; mawasiliano kati ya mke na mume ni hitaji la msingi la mke katika ndoa.
Kuwasiliana ni feelings na wanawake wanapenda neno feelings ndiyo maana hujikuta wana-fall in love.
Kawaida wanaume wengi wakiulizwa na wake zao wanajisikiaje kutokana na kuonesha felings za kuwa kunaatizo, chakushangaza ni kwamba wanaume wengi hujibu “hawajui”. Wanaume wengi hawajui vile wanavyojisikia kwa sababu siyo watu wa hisia.
“Men came from the factory emotionally unassembled; all emotional wires are not connected”
Wanaume hutoka nje ya ndoa zao, kwa sababu hao wanawake huwapa heshima hao wanaume kwa kuwapa sex.
Wanawake hutoka nje ya ndoa kwa sababu hao wanaume huwajali kwa kuwasikiliza ku-connect na hisia zao.
2. KUONGOZA
Ndoa nyingi zimeharibika kwa sababu mwanandoa mmoja anakuwa amemkalia mwenzake (dominate); kuongoza maana yake kuanzisha jambo lolote katika ndoa ili kulifanyia kazi na kuwajibika (initiate).
Wanawake katika ndoa hulalamika kwamba waume zao wanashindwa kuongoza nyumba zao matokeo yake wanawake wengi wamekuwa ni watu wa kulaumu na kulalamika.
Mke huitaji mume kuwa kiongozi katika maswala ya kiroho (maombi, kusoma neno), watoto (shule, michezo, nidhamu), mahaba (birthday, tendo la ndoa, anniversary) nk.
Pia mume anahitajika kuwa kiongozi mzuri linapokuja suala la pesa (pia ni vizuri kukumbuka kwamba maamuzi ya fedha ni mahesabu [math) siyo hisia ambapo Mr. Bajeti hupewa kipau mbele).
3. UHAKIKA (SECURITY)
Mke anahitaji kuwa na uhakika kwamba mume wake anampenda anamjali, ni yeye peke yake na anasikilizwa.
Mke anahitaji kuwa na uhakika kwamba mume hatamuacha atakuwa na yeye siku zote.
Mke ambaye hana uhakika na upendo wa mume wake anakuwa hajiamini, anajiona hana thamani, anajiona hapendezi na anakuwa hasikii vizuri kwa kuwa kila wakati anajawa na mawazo.
Ubarikiwe!

Monday, July 12, 2010

Tatu Bora kwa Mume!


Happy Husband; Happy Home:
Wanawake wengi leo wapo independent na inafika mahali wanajisahau kuwajali waume zao, ni muhimu sana kwa mwanamke kuwa na taaluma yake na pia ni muhimu sana kwa mke kukumbuka kwamba mume akifurahi nyumbani kunakuwa na furaha.
Mume akifurahi nyumbani kunakuwa na furaha, mke akifurahi maisha yanakuwa ya furaha na watoto wakifurahi nyumba inakuwa na furaha pia.
Leo tuangalia mahitaji matatu ya msingi ambayo mume akiyapata basi atafurahi na nyumbani patakuwa mahali pa furaha kwa mke na watoto.
Kumbuka mwanandoa akisema ndoa yake ina furaha na inaridhisha maana yake anatimiziwa mahitaji yake ya msingi katika ndoa au mahusiano na kama haridhiki na hana furaha maana yake hatimiziwi mahitaji yake muhimu.
Je, mahitaji ya msingi ya mwanaume kwa mke wake ni yapi?
Kuna mahitaji 3 ya msingi ambayo mwanaume huhitaji kutoka kwa mke wake nayo ni
1. MWENZA (Companionship)
Baada ya Adamu kuumbwa na Mungu alionekana ni mpweke hata baada ya kujichanganya na wanyama wengine; Mungu akaona haipendezi, akamuumba Hawa kwa ajili ya Adamu na akasema inapendeza.
Kwa nini mume anakuhitaji wewe mke kama mwenzi wake?
Ili uwe mtu wa kuwa naye, unayemfaa, mtu wa kucheza naye, kumbuka Adam alicheza sana na monkeys, samba, mbuni, Ng’ombe, kuku nk na vyote havikuweza kufanya ajisikia vizuri hadi Mungu alipomuumba mwanamke.
“Men love to have fun”
Ni muhimu sana Wake kufahamu kwamba waume zenu wanapenda kucheza na kwamba mume wako anapenda sana kucheza na wewe, kuwa na wewe, hivyo tafuta kitu chochote ambacho mume wako anakipenda, then fanya naye.
Kama humpi muda wa kuwa na wewe, kucheza na wewe basi atampata mwingine wa kuwa naye au kucheza naye, ndipo kilio huja...................
Pia jiulize kama mume wako hayupo kazini, au mahali unakofahamu yupo; je, atakuwa na nani? Wewe uliumbwa kwa ajili yake ili kuwa naye, kucheza naye na si kuwa vuvuzela!
(Mwanzo 2:18)
2. TENDO LA NDOA
Sex ni neno zuri ambalo si chafu kama wengine wanavyoamini na kulitumia hata kama litatajwa kanisani; kwani Mungu aliumba sex kwa ajili ya mke na mume kufurahia uumbaji wake.
Hata hivyo linapokuja suala la sex wanaume wengi ni hitaji la pili katika mahusiano ya ndoa wakati wanawake ni hitaji namba 13 kwa kufuata umuhimu.
Mwanaume yeyote katika ndoa, hitaji la sex kwake ni msingi na bahati mbaya ni kwamba asipopata sex kwa mke wake dunia inaweza kumuuzia.
Hata hivyo nasisitiza kwamba sex nje ya ndoa huweza kumuongoza mtu kwenye kifo
(Yakobo 1:14)
“Men get in touch with their emotions through sex, while women get in touch with sex through their emotions.”
3. HESHIMA (Respect)
Ukweli ni kwamba jambo la msingi kwa mume wako si kile unaongea kwake bali ni namna unavyongea kwake.
Inawezekana mume wako anao uwezo (potential) mkubwa sana kufanikisha maisha hata hivyo kutokana na ulivyo critical, blaming, kosa heshima na adabu kwa mumeo imekuwa ngumu sana yeye kupiga hatua.
Hitaji la kwanza la msingi kwa mwanaume yeyote ni heshima.
Kila maamuzi yanayofanyika katika ndoa yanahitaji kufanyika kwa ushirikiano wa mke na mume.
Kutoa sifa kwa mume wako ni njia ya maisha ya ndoa.
Behind every successful and great husband, there is an honouring and praising wife.
Kumbuka Baba akifurahi, nyumbani kunakuwa na upendo, furaha na amani na pia nyumbani kunakuwa mahali salama kwa kukimbilia.
Waefeso 5:21 – 24, 33
Kwa maelezo zaidi soma hapa