"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, July 5, 2010

Anajifunika Shuka!

Ana umbo ``size 14``

SWALI

Kaka Mbilinyi nilikuwa naomba msaada, ni miezi 8 sasa tangu nimeoana na huyu mwanamke ambaye kwa kweli nina mpenda kwani ana umbo zuri (size 14) na ninampenda kila sehemu ya mwili wake.

Hata hivyo tunapojiandaa na kuwa kwenye tendo la ndoa anachofanya ni kuziba taa na kujifunika mashuka hadi kwenye kidevu na tunakuwa ndani ya shuka gubigubi na kuendelea na tendo la ndoa.

Mimi napenda sana kumuona, natamani sana kumwangalia yeye na kila sehemu ya mwili wake kwa kuwa ndio hunisisimua zaidi kimapenzi kwani ni kweli ni mwanamke mrembo ambaye Mungu amenipa yeye ni zawadi kwangu.

Je, nifanyeje afahamu kwamba nampenda na ninahitaji kumwangalia mwili wake mzuri ambao kila siku nauona ni sexy?

MAJIBU:

Kaka, asante sana kwa swali zuri na hongera sana kwa kuwa mwanaume mwenye busara kuhitaji msaada ili kuhakikisha wewe na mke wako wote mnaridhishana vizuri katika ndoa yenu.

Pia hongera sana kwa kupata kitu chema, mwanamke ambaye anakuvutia na unampenda.

Ukweli ni kwamba jambo la msingi ambalo unaweza kufanya ni kumwambia wazi namna unampenda hasa kuona mwili wake mkiwa wawili chumbani.

Inawezekana kutokana na malezi yake bado hajisikii huru sana kujiweka naked, hajazoea ila ukishirikiana naye katika kumjenga kujiamini kuwa huru kwako itawezekana.

Je, ni mara ngapi umemkumbatia (caress) na kumnong’oneza kwamba yeye ni mwanamke mrembo sana na unavutiwa sana na (taja sehemu za mwili wake ambazo zinakupa msisimko na kwamba mkiwa wawili chumbani utafurahi kama unaweza kuona kwani unampenda na ungependa kuona).

Unatakiwa kumsifia asubuhi, mchana na jioni kila siku namna unavutiwa na umbo lake.

“Romance her like a crazy”

Mwambie unampenda kama alivyo hata kama ajihisi kuongeza uzito au wasiwasi tu kwamba havutii kwani urembo wa mwanamke ni kwa anayemtazama.

Pia kama una fedha za ziada (ni muhimu pia kuwa nazo) unaweza kwenda naye shopping na kumpa nafasi anunue “hot new dress and romantic” ambazo anaweza kuvaa kwa ajili yako.

Lengo ni kumfanya mke wako ajisikia comfortable na mwili wake anapokuwa na wewe chumbani.

Akijisikia comfortable na wewe anajiona yupo relaxed na atakuwa huru na wewe na kukupa chochote unahitaji kwake kwani anajisikia salama.

NB:

Tumia maneno yote yaliyopo duniani kumpa sifa kuhusiana na mwili wake hadi ajisikie comfortable hadi kufikia kuwa naked chumbani na mbele yako bila hofu na mashaka.

Siku nyingine unaweza kumuomba umfanyie massage mwili mzima, siamini kama atakuruhusu umfanyie massage huku taa zimezimwa.

Naamini hizo tips zinatosha kwa leo.

No comments: