"Marriage is our last, best chance to grow up."

Wednesday, July 21, 2010

Anajua Anachokifanya!

Mara nyingi siyo (mara chache) mume au mke hujikuta mwenzake ni msumbufu kwa kuuliza maswali ambayo hayana msingi kwa kuwa kinachoulizwa ni kile ambacho mume au mke huwa anafahamu namna ya kukifanya.

Nahisi bado hujanielewa naongea kitu gani labda nikupe mfano.

Siku moja Jane na mume wake James waliamua kwenda kuwatembelea wazazi wa John ambao wapo nje kidogo ya mji wanaoishi.

Hata hivyo baada ya kufika nyumbani kwa wazazi wao wakaambiwa kwamba wazazi wao nao walipanga kwenda kutembelea shamba.

Wote kwa pamoja yani Jane, James, mama yake James na baba yake James wakapanda gari moja na kuanza safari ya kuelekea shamba.

Jane alikaa kiti cha mbele na baba yake James (mkwe) ambaye ndo alikuwa dereva na James alikaa kiti cha nyumba pamoja na mama yake.

Baada ya kusafiri kwa muda fulani James akahisi baba yake anaenda au kuelekea njia ambayo si yenyewe hivyo akamnong’oneza mama yake kwamba baba yake anaenda njia ambayo si yenyewe

(aliamini kwa kumwambia mama yake basi mama yake ataropoka maneno yasiyopimika kumsema baba yake kwa kitendo cha kuendesha gari kwenda njia ambayo si sahihi).

Cha ajabu mama yake akamjibu James kwamba “Baba yako anajua anachokifanya” kitu ambacho kilimfanya James ajiulize kwani angekuwa ni yeye anayepotea na kuelekea mahali siko mke wake angemsema kwa fujo kama kawekewa vuvuzela mdomoni.

Ni kweli baba alipotea njia hata hivyo baada ya muda akakumbuka kwamba amekosea hivyo akageuza gari na kuelekea kule ambako ni sahihi.

(alikuwa anajua anachokifanya)

Walipofika shamba baba yake aliiweka kofia yake juu ya kiti na baada ya muda akaamua kukaa na akawa kasahau kwamba anaikalia kofia na kuikunja kunja; ndipo James akamwambia mama yake

“Unamuona baba anakalia kofia na kuikunja si mwambie anakalia kofia yake?”

mama yake akamjibu James kwamba

Baba yako anajua kile anakifanya

jibu ambalo pia lilimfanya James afikirie upya kuhusiana na mahusiano yake na mke wake hasa suala la kukosoana vitu vidogo vidogo kama hivi.

Inawezekana umemwambia mume wako anatakiwa kupaka rangi nyumba na kila siku unarudiarudia kumsema ukiamini kwa kumpigia kelele basi ataanya kile unasema, Mumeo anajua kile anakifanya ndiyo maana pamoja na kumsema nyumba bado haijapakwa rangi!

Inawezekana kila siku unamwambia mke wako anatakiwa kuhakikisha drawer za makabati zinafungwa kila akifungua hata hivyo kila siku unazikuta zipo wazi, ukweli ni kwamba mke wako anajua kile anakifanya.

Ni kweli inawezekana umeshamwambia mpenzi wako akufanyie kitu Fulani na ni muda sasa umepita na bado hajatimiza au hajafanya, umeamua kumsema kila siku ili afanye au kutimiza ahadi yake, hata hivyo ukweli ni kwamba yeye ni mtu mzima na anajua kila anakifanya.

Kumbuka kuwa kwenye ndoa ni kuwa mtu mzima na mtu mzima hapigiwi kelele kama mtoto kwani kila mtu mzima anajua anachokifanya na hakuna kitu mwanaume hapendi kama mwanamke ambaye kila wakati ni kukosoa na kusema sema tu (kefyakefya) na kumuweka kundi moja na watoto;

Ukweli ni kwamba mume wako anajua anachokifanya pia mke wako anajua anachokifanya.

Wengi tumegundua hii siri hatupigishani kelele kwani nikimwambia mke wangu leo nitaosha dishes zote au nitakusaidia kufua nguo hana haja ya kuniliuza au kunikazania utafanya saa ngapi hiyo kazi badala yake anatakiwa kurelax na kuenjoy maisha kwani mume wake ninajua ninachokifanya na ninafahamu nitafanya wakati gani period.

Usiumize kichwa chako, anajua anachofanya!

7 comments:

Anonymous said...

yes good lesson, kuangazia leo hata nikiomba ela ya kusuka nisipopewa mwaka mzima sirudii tena. maana kweli nayo ni kero kumkumbusha mtu mzima kila mara. asante kwa somo mkubwa

Mercylina said...

pole kwa majukumu naomba nitoke nje ya mada huwa napenda kusoma ktk blog yako mara nyingi nashindwa kusoma hayo maandishi ombi ni kuwa badilisha rangi ya background au ya maandishi.
natanguliza shukrani zangu.

joven said...

beautiful blog..pls visit mine and be a follower.. thanks and God bless..

http://forlots.blogspot.com/

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Mercyline,
Sijajua kama ni kweli suala la background ni tatizo kwa watu wote kwani wewe ni mtu wa kwanza kulalamika so nasubiri wengine watoe maoni yako kwani isije kuwa tatizo ni wewe na macho yako ndiye mwenye tatizo kwani wengine tunasoma bila tatizo.

Samahani kama nimekukwaza na ukiona ngumu zaidi nipe email yako niwe nakutumia moja kwa moja kwa inbox kitu ambacho haitasumbua kuja kusoma hapa.

Upendo daima

Lazarus Mbilinyi said...

Dada Mercyline,
Sijajua kama ni kweli suala la background ni tatizo kwa watu wote kwani wewe ni mtu wa kwanza kulalamika so nasubiri wengine watoe maoni yako kwani isije kuwa tatizo ni wewe na macho yako ndiye mwenye tatizo kwani wengine tunasoma bila tatizo.

Samahani kama nimekukwaza na ukiona ngumu zaidi nipe email yako niwe nakutumia moja kwa moja kwa inbox kitu ambacho haitasumbua kuja kusoma hapa.

Upendo daima

Anonymous said...

kweli mwenzangu tunakaa tunabishana na mchumba harusi lini mwisho tunaishia kugombana,kuanzia leo kama atalisikia swali hili kwangu nadhani atashanggaa harusi inafungwa tu hta kama si yeye bwana harusi,somo zuri.

Lazarus Mbilinyi said...

Kama kweli ni mtu mzima na akili zake na kila ukiongea kuhusu harusi hamfiki popote, ukweli ANAJUA ANACHOKIFANYA so wewe tulia then fanya kweli.

Naamini umeelewa ingewezekana unnge print hii article na umpelekee asome ili siku akiona umefanya kweli ajue nani mwenye makosa kwani watu wazima si watoto.

Upendo daima