"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, July 1, 2010

Hadi Lini?


SWALI
Nimefiwa na mume wangu miezi kadhaa iliyopita, je nisubiri kwa muda kiasi gani ili niweze kuolewa tena?
Je, kibiblia ni muda kiasi gani?
Ni mimi mama BM
JIBU
Asante kwa swali zuri ambalo ni kweli huleta utata sana katika jamii zetu hasa kutokana na mapokeo tofauti.
Ukweli kama ni Kibiblia basi unaruhusiwa kuolewa muda wowote baada ya kifo cha mume wako au mke wako kutokea, iwe siku mbili, wiki mbili, miezi miwili miaka miwili au hata miaka 20.
Ukweli ni kwamba hakuna kipindi maalumu kibiblia ambacho kinaeleza muda kamili unaotakiwa mwanandoa kusubiri ili aoe au kuolewa baada ya mume au mke kufa.
Hivyo mume au mke anayebaki anao uhuru wa kuoa au kuolewa muda wowote anaotaka yeye kwani yupo huru.
Mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mumewe wakati akiwa hai, lakini yule mume akifa, yule mwanamke amefunguliwa kutoka katika sheria ya ndoa. Hivyo basi, kama huyo mwanamke ataolewa na mwanaume mwingine wakati mumewe akiwa bado yuko hai, ataitwa mzinzi.
Lakini kama mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa.
(Warumi 7:2-3)

Pale mwanaume na mwanamke wanapooana, Mungu huwaunganisha na kuwafanya kuwa mwili mmoja (Mwanzo 2:24, Mathayo 19:5-6) na kitu ambacho huweza kuwatenganisha ni kifo na kifo kinapotokea yule mwanandoa anayebaki anaruhusiwa kuoa au kuolewa.
Hata mtume Paulo katika nyaraka zake anaeleza wazi suala la wajane kuolewa (1Wakorintho 7:8-9, 1Timotheo 5:14)
Sasa tuje in real life, ukweli ni ngumu sana kuhimili tukio la kufiwa na mume au mke na lini uoe au uolewe inatokana na namna mlivyokuwa mnapendana kwani kama mlikuwa na migogoro kila siku na mmoja akifa anayebaki unadhani atajisikiaje?
Kama umefiwa na mume au mke ambaye ulikuwa unampenda kuliko kitu chochote katika dunia hii; kuendelea na maisha yako kama kawaida huwa ngumu sana na huonekana ni kitu kisichowezekana.
Itachukua muda mrefu sana hata kufikiria tu namna utaweza kuendesha maisha yako mwenyewe.
Mume au mke anapofariki iwe ajali au kifo cha kawaida ukweli ni kitu ambacho huumiza sana kuliko kawaida, kuishi bila yule ambaye ulikuwa unampenda kuliko kitu chochote duniani ni kitu ambacho huonekana ni impossible.
Hata hivyo kuna wakati utafika utaanza na kuweza kuendelea na maisha na muda kama huu ukifika haina haja kujiona una hatia, ni kawaida wewe kuendelea na maisha yako.
Inawezekana hata mume wako au mke wako baada ya kufa anapenda sana wewe uendelea na maisha yako kama kawaida.
Kuoa tena baada ya mke kufa ni jambo la kawaida sana kwa wanaume na kuolewa tena baada ya mume kufa limekuwa gumu kidogo kwa wanawake kwani inakuwa ngumu kidogo kumpata mwanaume wa kuolewa naye kutokana na tofauti ya umri hata hivyo sasa wanawake wameanza kuona ni kitu cha kawaida kwani wanawake kuolewa.
Kawaida wengi ambao wamepita njia hii wanakiri kwamba unapopata wazo la kuoa au kuolewa tena baada ya mke au mume kufariki hujisikia kama vile unamsaliti mume wako au mke wako ambaye amefariki, hata hivyo hii si kweli kwani mwisho wa ndoa yoyote ni kifo.
Kama umempata mtu ambaye anakupenda na wewe unampenda kwelikweli maana yake umepata neema ambayo wengi hawajaipata yaani kuolewa na kuwa katika penzi siyo mara moja bali mara mbili katika maisha yako, ni watu wachache sana wanaweza kuwa na jambo kama hilo, kama kweli muda wa kuomboleza umeshapita na una uhakika upo salama, why not?
Mtafute huyo special one wako wa mara ya pili katika maisha na hiyo kweli ni zawadi.
Kufurahia maisha yako kwa sasa huku umeoa au kuolewa na mtu mwingine ni uamuzi wa busara zaidi, so go for it!
In Short:
Lini niolewe au kuoa baada ya mume au mke kufa?
Ni pale unapojisikia umeomboleza vya kutosha na umemfahamu vya kutosha yule unataka kuoana naye.

7 comments:

Anonymous said...

Jamani kaka Mbilinyi,mada ya leo nzuri lakini haisomeki vizuri tafadahali rekebisha font colour.
Thanx.

Lazarus Mbilinyi said...

Samahani sana,
Hata sijafahamu ilikuwaje hadi fonts zikawa hafifu kiasi hicho hata hivyo nimerekebisha.

Pole sana kwa usumbufu maana naamini wengi mngezeeka kwa kukomalia fonts kuzisoma ili upate ujumbe mzima.
Asante kwa kunistua.

Upendo daima

Anonymous said...

Nakiri, sikufahamu kuoana na widow huwa na kazi kiasi hiki kwani pamoja na mimi kumuona yeye ndo mtu wa maana kuliko mtu yeyote katika maisha yangu hapa duniani bado yeye anamkumbuka mume wake wa zamani wakati hayupo.
Ameshindwa kabisa kunipa respect na inaniumiza sana.

Kabla ya kuoana na mtu ambaye amefiwa na mke au mume ni muhimu sana kujihoji kwani bila kuwa makini you will pay the price kwa ndoa yake ya kwanza.

Ni maoni yangu tu
BA

Anonymous said...

Hata hivyo ukweli unabaki palepale kwamba kama unachumbia au chumbiwa ili kuolewa mara ya pili maana yake sasa mambo ni tofauti, inawezekana unaingia kwenye mahusiano na memories mpya za mambo mazuri au mabaya kwenye mahusiano yaliyopita na inabidi uwe makini na kuhakikisha vidonda vyote vimeponywa sawasawa.

Anonymous said...

kama ni mada sawa,lakini kama ni uhalisia ni kwamba huyo mwanamke ana ka boyfriend kake pembeni ka siku nyingi ,hivi kweli mwanamke umepoteza mume hajakaa vizuri unataka kuolewa tena,haijawahi tokea kwani wanawake sisi ni vigumu kumtoa mume moyoni ila kama ulikuwa umelazimishwa kuolewa naye hapo sawa.huu ni utata

Anonymous said...

kama ni mada sawa,lakini kama ni uhalisia ni kwamba huyo mwanamke ana ka boyfriend kake pembeni ka siku nyingi ,hivi kweli mwanamke umepoteza mume hajakaa vizuri unataka kuolewa tena,haijawahi tokea kwani wanawake sisi ni vigumu kumtoa mume moyoni ila kama ulikuwa umelazimishwa kuolewa naye hapo sawa.huu ni utata

Lazarus Mbilinyi said...

Swali lilikuwa usubiri hadi lini ili kuolewa tena, Biblia haina muda maalumu kwamba ni siku kadhaa au miezi kadhaa bali tunachojua ni kwamba baada ya kifo cha mmoa wa wanandoa hapo ni mwisho wa hiyo ndoa na anayebaki yupo huru.

Issue inakuja katika real life si kawaida na haiwezekani unaona masaa machache au siku chache au hata ndani ya mwezi kwani ili kumpa mchumba mwingine lazima kuwe na muda wa kwanza kufahamiana, pia taratibu za kuoana ambazo hata kama ni haraka haraka haiwezi kuwa ndani ya mwezi mmoja hadi miezi mitatu, hivyo katika tamaduni nyingi angalau miezi 6 na kuendelea.
Ingawa inatokana na ndoa yenyewe je wahusika walikuwa wanapendana au ndo ilikuwa battlefield.
Kufika na mke au mume ni jambo gumu sana na huumiza sana kiasi cha kusababisha kuchelewa kufanya maamuzi ya kuoa tena, jambo la msingi anayebaki yupo huru.
Tumeona mifano mingi ya wanandoa ambao baada ya mmoja kufanya wao inakuwa kama sherehe fulani na anaoa au kuolewa baada ya muda mfupi hadi kunazuka maswali yasiyo na majibu.

Anyway kila ndoa ipo tofauti.