"Marriage is our last, best chance to grow up."

Friday, July 2, 2010

Kukosa Uzazi

James na Jane walimtembelea Daktari ili kupata ukweli kwa nini Jane hashiki mimba. Walishangazwa sana na ripoti ya Daktari kwamba James ana tatizo ambalo ni tangu kuzaliwa kwamba hawezi kuzalisha sperms.

James hawezi kumfanya mke wake kupata mimba (sterile).

Linda aliugua kidole tumbo (appendicitis) na kwa makosa Daktari alidhani anaumwa Flu, matokeo yake kidole tumbo (appendix) kilichanika na kusababisha maambukiza ya ndani hadi kwenye viungo vya uzazi.

Sasa Linda hawezi kushika tena mimba (infertile) na hataweza tena kuzaa hadi msaada wa kitaalamu (medical help).

Rehema na Jackson wamebarikiwa kuzaa mtoto wa kike muda mfupi baada ya ndoa yako. Wakapanga kuzaa mtoto mwingine, hata hivyo iliwachukua miaka 9 kuhangaika kwa maumivu na uchungu kuhakikisha wanapata mtoto mwingine.

Kitaalamu wanaita walikuwa na secondary infertility.

Kuna aina nyingi sana za kukosa uzazi na kawaida kama mke hataweza kushika mimba (baada ya mahusiano ya kimapenzi ya kutafuta mtoto) kwa mwaka mmoja basi mwanamke mume atajulikana kama amekosa uzazi (infertility), hii ni pamoja na mwanamke ambaye kila akishika mimba hutokea miscarriage.

Wakati mwingine tatizo la kukosa uzazi huweza kuondolewa kwa wanandoa kubadilisha tabia au taratibu kama vile, kama mwanaume anazalisha sperms kidogo basi anaweza kusubiri kwa muda wa kutosha ili kuweza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wake au mume anaweza kuhakikisha anajihusisha na mapenzi (sex) wakati kamili ambapo mke anakuwa fertile.

Umri pia unaweza kuwa ni factor linapokuja suala la kukosa uzazi, kawaida mwanamke huwa katika kiwango cha juu kabisa cha kushika mimba akiwa kwenye umri wa miaka 24 – 28 na baada ya miaka 30 uwezekano wa kuweza kushika mimba huanza kupungua.

Pia kukosa vyakula bora huweza kuchangia, pia matumizi ya pombe (ulevi) na madawa ya kulevya, magonjwa ya zinaa huchangia kukosa uzazi.

Wapo wanandoa ambao kuwa na watoto ni kama suala la hewa tunayovuta na kupumua.

Kama hujafanikiwa kupata mtoto bado unaweza kujisikia mwili umekusaliti, umekudanganya na ndoa inaweza kuonekana inaelekea mahali kusiko na njia ya kutokea.

Unaweza kujiona upo frustrated na kila maamuzi ya maisha ya kila siku.

Pia inaweza kutokea mume na mke kuanza kulaumiana kila mmoja akimlaumu mwenzake kitu ambacho si busara njema kwani huweza kuongea maumivu zaidi.

Ni kweli kukosa uzazi huumiza unaweza kujiona mpweke na kukatishwa tamaa.

Kwa maelezo zaidi soma hapa


No comments: