"Marriage is our last, best chance to grow up."

Monday, July 19, 2010

Likizo

Kwa wasomaji wote wa blog hii, napenda kuchukua nafasi hii kuwajulisha kwamba nitaanza likizo ya mwezi mzima na sitaweza kupatikana mara zote kama kawaida hasa kutokana na kutumia muda mwingi na familia katika mapumziko.
Kama una swali unaweza kunitumia hata havyo majibu yanaweza kuchelewa kutokana na kukosa muda.
Zaidi nashukuru sana kwa namna ulivyofanyika baraka kwangu na familia yangu maana bila wewe kuja kusoma hapa nisingeweza kujifunza na hatimaye kukua katika fikra na kuwa mtu anayefaa katika jamii.
Safari yangu na familia itaanzia Toronto tarehe 19/07/2010 kwenda Dubai na hatimaye Dar es salaam na baada ya hapo tutakuwa Njombe hadi tarehe 15/08/2010
Mungu akubariki sana

6 comments:

mahembega said...

All the best bro,nimejifunza mengi sana hapa nashukuru sana,namuomba mungu ili nienende vyema ktk safari ya maisha yangu.

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli mimi na familia yangu twapenda kuwatakieni SAFARI na LIKIZO njema sana. Mungu awe nanyi katika kila mufanyalo. Na tutawa-miss. SAFARI NJEMA NA MUWE NA WAKATI MZURI:-)

Anonymous said...

Hello kaka Mbilinyi,
Ninapenda kuwatakieni likizo njema na yenye furaha. Naomba Mungu awapelekee jeshi la malaika wawalinde safarini na kuwafikisha salama kila kituo cha safari yenu.

Likizo njema.

Fay

Daniel said...

Amen Familia ya Bwana Mbilinyi, Bwana Yesu awalinde safarini na awape muda mzuri wa kuwa Africa bara la asili , nimekuwa sana nikifuatilia makala zako kwenye blog hii , kiasi kwamba mara tu nikiingia kwa ofisi asbh blog yako inakuwa site page ya pili kufungua baada ya kufungua mail zangu za ofisi kujua siku /week inakwendaje, Kaka neema na kipawa alokupa Mungu katika eneo hili yeye tu azidi kukikuza zaidi kwa ajili ya utukufu wake
karibu Africa, Tanzania, Dar, kisha Njombe
Daniel.

Anonymous said...

Karibu Tanzania

Lazarus Mbilinyi said...

Asante sana kwa maombi yenu. Tumefika salama kabisa Tanzania na kila kitu kipo shwari.

Upendo daima