"Marriage is our last, best chance to grow up."

Tuesday, July 6, 2010

Nimekudondokea!

"Nimefurahi; kwani sasa naolewa"

Jane sasa ana miaka 36 na bado hajaolewa, ameshawahi kuwa na uhusiano na wanaume tofauti mmoja kwa miaka 6 hata hivyo hawakuoana na mwingine miaka 3 na wengine wengi chini ya mwaka mmoja kila baada ya muda fulani.

Kila uhusiano aliokuwa nao aliona kuna tatizo ambalo lilisababisha kuuvunja hata kabla ya kufunga ndoa.

Kwa asili Jane ni mwanamke mwenye discipline, mwangalifu, organized, mwenye mawazo mazuri na yupo caring.

Siku moja alikutana na James na katika ongea ongea kila mmoja akavutiwa na mwenzake na wakajikuta wanapanga wakutane jioni moja sehemu kwa dinner na baada ya dinner ya kwanza ikaja ya pili na then ya tatu.

Baada ya wiki tatu akakutana na mama yake ili kumueleza kile wameongea na James na matarajio yao:

MAMA: Mwanangu Jane, karibu naona leo una uso wa furaha nahisi una habari njema!

JANE: Hakuna wakati najisikia vizuri kama sasa hivi kwani mama sasa nimepata mume wa kweli wa kuoana naye, nafurahi sasa naolewa!

MAMA: Unaolewa na nani?

JANE: Naolewa na James

MAMA: Hongera, umefahamiana naye kwa muda gani mwanangu?

JANE: Wiki tatu zilizopita, najua huwezi amini, hata hivyo, ila najua James ni kwa ajili yangu, tangu siku ya kwanza tulipokutana wote tulijua hilo, hata kama hatukuongelea, baada ya wiki tukaelezana ukweli, nilijua ataniomba tuoane, na nilijijua nitasema ndiyo, sijawahi kujisikia raha kama wakati huu. Mama unafahamu mahusiano niliyokuwa nayo huko nyuma ni kweli kila mahusiano kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa si sahihi lakini kwa James kila kitu kipo sawa.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Pamoja na furaha na vicheko ambavyo Jane anavionesha ukweli ni kwamba amemdondokea James (fall in love).

Kwenye moyo wake anaamini kwamba James ni wonderful man on earth surface, ni mwanaume perfect kila eneo.

Anaamini James atatimiza ndoto zake za kuwa na mwanaume ambaye hataumiza moyo wake.

Ingawa James amemweleza wazi Jane kwamba alishawahi kuoa mara tatu na ana watoto watatu kila mtoto na mama yake.

Na kwamba alishaacha kazi mara tatu kwa kushindwa kuelewana na mabosi wake.

Bado Jane anajiona maisha ya James yatakuwa ya furaha forever kwani wanapendana (ame-fall in love).

Wengi hujikuta wanaingia kwenye ndoa kwa kupitia mlango wa (fall in love, in love). Unakutana na mtu ambaye sifa zake za mwonekano na haiba huweza kuumba electric shock na kuamsha upendo ndani yako.

Akili (logic) zinakuwa off, na unajikuta upo kwenye motion kutaka kumjua zaidi, na unajukuta mpo pamoja katika kula chips na kuku na soda mara ya kwanza ingawa interest si chips na kuku bali kuvumbua penzi jipya.

Je, unadhani hilo penzi motomoto na linalonyegesha ni kitu sahihi?

Unajikuta ukienda kulala una muwaza yeye, na unapoamka asubuhi waza la kwanza ni kuhusu yeye. Unakuwa na hamu ya kuwa na yeye, na ku-spend muda na yeye ni kama kuwa mbinguni, na mkishikana mikono unajihisi damu inaingiliana.

Unatamani kuendelea kupeana kisses kiasi cha kupenda kusingekuwa na kwenda kazini au shuleni.

Kukumbatiana kunawakumbusha kuoana na kuishi kama mke na mume.

Mtu ambaye yupo “in love au fallen in love” anakuwa kwenye udanganyifu (illusions) kwamba mpenzi wake ni perfect.

Mama yake anaweza kuona kasoro za mpenzi wa mtoto wake na mtoto hawezi kuona. Mama atamwambie mwanae hivi unajua huyo mwanaume alikuwa amelazwa Hospitali ya Milembe Dodoma kwa miaka 3, atamjibu mama mbona alisharuhusiwa kutoka miezi 3 sasa na yupo salama kabisa.

Rafiki zake wanawake kuona hizo kasoro wa huyo mpenzi wake na hata kama wanafahamu wanasubiri awaulize na hawezi kuwauliza kwa sababu katika moyo wake anaona mpenzi wake ni perfect na kile wengine wanafikiria kuhusu mpenzi wake hakina maana yoyote.

Suala ma “fall in love” ni kitu cha kufikirika si kitu halisi.

Dr. Dorothy Tennov (mtaalamu wa saikolojia) ametoa conclusion kwamba penzi la aina hii (fall in love) huweza kudumu kwa miaka 2 tu ndipo huanguka kutoka mawinguni hadi ardhini ndipo macho hufunguka na kila mpenzi huanza kuona uozo wa mwenzake.

Ndipo kila mmoja huanza kugundua kwamba baadhi ya tabia za mpenzi wake zinaudhi kupindukia (irritating & annoying) na kwamba kumbe mwenzake anaweza kuumiza na kuwa na hasira na maneno makali na magumu.

Anaanza kujiuliza hivi ilikuwaje nikawa foolish kiasi hiki?

Kwa maelezo zaidi soma hapa

No comments: